You dont have javascript enabled! Please download Google Chrome!

CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) CHAZINDUA MTAMBO WA KUTENGENEZA LIQUID NITROGEN

Liquid Nitrogen ni Nitrogen iliyo katika hali ya kimiminika chenye joto la chini sana  la nyuzi joto −195.79 °C kinachozalishwa kwa mtambo maalumu. Liquid Nitrogen ina matumizi mengi sana baadhi yake ni kuhifadhia mbegu za wanyama, kuhifadhia seli hai na kuhifadhia sampuli za vimelea mbalimbali vya magonjwa ya mifugo na binadamu.

Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) tarehe 10/01/2020 kilizindua mtambo wa kutengeneze liquid Nitrogen. Mtambo huo upo kwenye Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za Binadamu (College of Veterinary Medicine and Biomedical Sciences). Mtambo huo utazalisha liquid Nitrogen kwa ajili ya kuhifadhi mbegu zitakazotumia kuboresha kosafu za ng’ombe.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo makamu mkuu wa chuo hicho Prof. Raphael Chibunda alisema mtambo huo ulenge kusaidia wafugaji zaidi husan wa mkoa wa Morogoro na mikoa inayopakana nayo na Tanzania kwa ujumla. Matumizi ya mbegu bora za ng’ombe yatasaidia kuboresha mifugo.

Aidha chuo kitafanya mawasiliano na kituo cha kuzalisha mbegu cha NAIC Arusha ili mbegu nazo ziweze kupatikana chuoni hapo. Hii ni fursa ya kuboresha ng’ombe hususan kwa Mkoa wa Morogoro.

 

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!
%d bloggers like this: