You dont have javascript enabled! Please download Google Chrome!

JE WAJUA MADHARA YA UPUNGUFU WA VITAMIN A KWA KUKU?

PAKUA APP YA TOVUTI HII YA UFUGAJI HAPA

Ndugu mdau na mfuatiliaji wa makala za Tovuti ya Ufugaji kwa lengo la kujielimisha mambo mbali yahusuyo ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali, leo nakueletea makala mahususi inayohusu upungufu wa vitamini A kwa kuku. Wafugaji wengi wamekuwa hawaweki mkazo kwenye aina na kiasi cha chakula wanachowapa kuku au mifugo yao na kuwapelekea kupata madhara ambayo wafugaji hawahusianishi na swala zima la chakula. Kitu cha kwanza watafikiria magonjwa yanayotokana na vimelea vya magonjwa na hata kuchukua hatua ya kuwapa tiba bila hata ya kupata ushauri wa wataalam wa mifugo. Jambo hili la kutibu bila kujua chanzo cha ugonjwa limekuwa na madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kutengeneza usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa mbalimbali. Lakini pia kusababisha ugonjwa uendelee kushamili na kupelekea madhara makubwa.

 

Leo nimeona niongelee madhara yanayotokana na upungufu wa vitamini kwa kuku na hasa nitajikita kwenye upungufu wa Vitamin A ambao una madhara makubwa kwa kuku na umekuwa ukiwachanganya wafugaji maana dalili zake zinafanana na ugonjwa mwingine. Fuatana nami ili uweze kufahamu namna ya kukabiliana na changamoto ya upungufu wa vitamin A.

 

Nini kinapelekea upungufu wa Vitamini A kwa kuku

Kuku wasipopewa vyakula vyenye chanzo cha Vitamini A kwa muda mrefu hupelekea kuku kukosa hii vitamini mwilini na kuwapelekea kupata ugonjwa unaojulikana kama ukosefu wa Vitamini A. Vyanzo asili vya vitamini A ni mboga mboga za kijani mfano mchicha, majani ya maboga, majani ya mikunde, mipapai, lusina na sukuma wiki au majani mabichi.

 

Umuhimu wa Vitamini A kwa kuku

– Husaidia katika ukuaji

-Husaidia chakula kisharabiwe vizuri

-Husaidia ukuaji na uimarishaji wa mifupa ya kuku na kumfanya atembee kwa uimara

-Humsaidia kuku kuona vizuri

-Hulinda mwili dhidi ya magonjwa na kupunguza vifo

-Humfanya kuku muda wote kuwa amechangamka

-Husaidia kuku kuwa mwenye afya.

-Huwezesha kuku kuwa mtagaji mzuri.

 

Madhara ya upungufu wa Vitamini A kwa kuku

Madhara ya upungufu wa Vitamini A hutokea hasa kwa kuku wadogo ndani ya wiki 3 hadi ya 4.

Dalili za mwanzo za upungufu wa Vitamini A ni;

-Kukosa hamu ya kula na kupungua kwa ukuaji

-Udhaifu wa jumla wa mwili

-Kukosa uimara wa kusimama

-Kupinda kwa manyoya ya sehemu ya nyuma (mkia)

-Ukuaji wa manyoya sehemu mbalimbali za mwili huwa hafifu na panga za kuku huonekana hafifu.

-Kuku hushambuliwa na magonjwa mengine kirahisi

Kupungua kwa utagaji na uanguaji wa vifaranga kwa kiasi kikubwa

-Kutoka ute puani na machoni

-Macho hujaa uchafu mzito ambao huziba macho kunakopelekea kuvimba na kukosa kuona kabisa. Uchafu huo unafanana na sabuni ya kipande iliyolowa maji.

-Mwisho kuku hudhoofika na kufa

Kuku wenye upungufu wa vitamin A wakiwa na mkia uliopinda

 

Macho yamevimba kwasababu ya kujaa uchafu mzito mithili ya sabuni iliyolowa maji

 

Jinsi ya kukabiliana na upungufu wa Vitamini A

Mara kwa mara ugonjwa hujitokeza wakati wa kiangazi na hii inatokana na kukosekana kwa majani/mboga mboga za kula kuku. Hivyo juhudi za makusudi za kuhakikisha wanaendelea kupata vitamin zinawekwa. Jitihada hizi ni pamoja na;

-Kuwapa chakula chenye mchanganyiko wa kutoa Vitamini A kwa kuku

– Kuwapa majani mabichi/mboga mboga kama mchicha, majani ya mikunde, lusina, mipapai

-Kuwapa dawa ya vitamin (Multivitamin) ili kuzuia kujitokeza kwa ugonjwa huu hasa wakati majani mabichi hayapo. Zipo aina nyingi za Mutivitamini zenye majina ya kibiashara unazoweza kuzitumia kukinga kuku wako

-Kuku wagonjwa hasa wenye shida ya macho wasafishwe vizuri na maji ya uvuguvugu yenye chumvi kiasi huku ukikamua uchafu wote hadi uchafu wote uiishe. Kisha wape vitamin za dukani kadiri utakavyoshauriwa na mtaalam.

 

Magonjwa yenye dalili zinazofanana na upungufu wa Vitamini A

  1. Mafua ya kuku (Fowl Coryza)

Dalili zaake: Kuku huvimba uso na macho, kamasi hutiririka toka puani na mdomoni, hukohoa, huhema kwa shida na kukoroma. Mayai hupungua asilimia 10 hadi 40

 

 

SOMA PIA HAPA

 

.

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!
%d bloggers like this: