Jifunze kutengeneza chakula cha kuku mwenyewe

Wakati wa kufuga ni muhimu kuku wapate sehemu ya wazi wanayoweza kutembea kwa uhuru. mfugaji mwenye lengo la kufuga kuku wengi wenye umri mmoja na kupata mayai mengi au aweze kuuza kuku wengi kwa wakati mmoja wenye umri unaolingana inabidi uwe na vifaranga wengi wa umri mmoja.

Kuwa na vifaranga wengi wa umri mmoja kuna faida nyingi ikiwa ni pamoja, kupunguza gharama za ufugaji kwa mfano chanjo na tiba, kutunza kuku kitaalamu kwa urahisi, kupata mayai mengi kwa wakati mmoja, kuuza kuku wengi kwa wakati mmoja, na kuwapa uhakika wateja.

kuna njia kuu mbili za upatikanaji wa vifaranga wengi kwa wakati mmoja nazo ni;

Kwa kuwaatamisha kuku wengi kwa wakati mmoja Kwa njia ya mashine ya kuangulia (incubator) Njia hizo zinaweza kumwezesha mfugaji apate vifaranga bora. Uchaguzi wa njia ipi itumike utatokana na mtaji wa mfugaji na mahali alipo. Njia ya kuatamisha inatumika kwa tetea wengi kuatamishwa kwa wakati mmoja hivyo mfugaji anatakiwa achague mitetea, mayai, aandae viota, maji na chakula bora.

       

Sifa za tetea wa kuatamia

Kuku mwenye umbo kubwa Mwenye uwezo na historia nzuri ya kuatamia na hatimaye kutotoa vifaranga.

      

Sifa za mayai ya kuatamisha

Mayai ya siku ya mwisho kutagwa ndio yawe ya kwanza kuwekwa yafuatiwe na ya siku zinazofuata yasizidi wiki mbili tangu kutagwa. Lisiwe kubwa sana au la duara, lisiwe na uvimbe. Yasiwe machafu wala yasiwe na nyufa.

Sifa za kiota na chumba cha kuatamia Kuku wanaoatamia watengwe katika chumba ili kuondoa tatizo la kutagiana. Mlango na dirisha viwekwe wavu ili muda wa mchana mwanga na hewa viweze kuingia.

Chumba kiwe na nafasi ya kutosha kuweka viota, chakula na maji. Ili kutumia eneo vizuri viota vinaweza kutengenezwa ukutani kama mashelfu. Viota viundwe vizuri kwa nyasi, maranda makavu ya mbao, au nguo ya pamba lakini isiyo tetroni. Viota visiwe sehemu yenye unyevunyevu.

Idadi ya viota vilingane na idadi ya tetea waliochaguliwa kuatamia. Vinyunyiziwe dawa ya kuuwa wadudu {Akher powder} ukiwemo utitiri kwa kuwa ni wasumbufu hivyo husababisha kuku kutokatoka nje na kupunguza uwezekano wa mayai kuanguliwa yote.

Kuku wanaoatamia wapewe chakula cha kutosha cha kuku wakubwa wanaotaga. Majani, mboga na maji ya kunywa ni muhimu kwa kuku hao. Vyote hivyo viwekwe kwenye chumba kinachotumika kuatamia kuku asiende umbali mrefu kutafuta chakula na kuyaacha mayai kwa muda mrefu.

       

Hatua za kuatamisha kuku

Kuandaa viota, uchaguzi wa tetea bora na kuandaa mayai. Tetea wa kwanza akianza kuatamia muweke mayai yasio na mbegu ama viza( nakumbuka nilisha zungumziaga hili hapa hapa jf) . Rudia zoezi hilo mpaka itakapofikia idadi ya kuku unaowahitaji. Baada ya kupata idadi ya kuku wawekee mayai yenye mbegu. Kuku wote waliochaguliwa kwa ajili ya kuatamia wawekwe wakati wa usiku kwa sababu ya utulivu uliopo. Kwa kupitia njia hiyo kuku mmoja anaweza kuatamia hadi mayai 20 kwa kuzingatia sifa zake.

Baada ya kutotoa hatua ya awali ni uleaji wa vifaranga. Kuku wazazi hutengwa na vifaranga. Vifaranga hupewa joto na mwanga kwa kutumia taa ya umeme, jiko au kandili. Maji yenye glucose kwa ajili ya kuongeza nguvu, na chakula ni muhimu kwa vifaranga hao.

Changamoto Huhitaji sehemu kubwa kwa sababu ili upate vifaranga wengi unahitaji kuku wengi wanaoatamia. Kuwepo kwa wadudu kama utitiri na kutopatikana kwa chakula cha kutosha husababisha kuku kutoka toka nje na kusababisha mayai kuharibika.

 

        Kuku kupata magonjwa wakati wanapoatamia

Kutokuwa na kipimo cha kupimia mayai yaliyo na mbegu Jambo lingine muhimu kuzingatia ni chanjo. Wakati wa kutayarisha mpango wa kuchanja kuku kwa ajili ya kinga dhidi ya magonjwa kuna vipengele sita vya kuzingatiwa.

 

  1. Vifaranga vinavyoanguliwa kwa pamoja:

Iwapo kuna kundi zaidi ya moja la vifaranga wanaoanguliwa, mfugaji aweke utaratibu wa chanjo utakaopunguza uwezekano wa kuenea magonjwa.

  1. Umri wa kuchanja kuku:

Kwa kuku ambao wanatarajiwa kutaga mayai au kuwa kuku wazazi, chanjo nyingi hutolewa si zaidi ya mwezi mmoja kabla ya kuku kuanza kutaga.

  1. Magonjwa makuu katika eneo husika:

Ni muhimu sana kuelewa magonjwa ya kuku yaliyopo katika eneo lako kabla ya kuandaa programu ya uchanjaji, kwa magonjwa ambayo chanjo zenye vimelea hai hutumika.

  1. Hali ya kiafya ya kuku watakaochanjwa: Usiwape chanjo kuku ambao wanaonesha dalili za kuathirika kwa mfumo wa hewa au wanaonesha kuwa na minyoo au wadudu wengine. Kwa kuku walio na dalili hizo chanjo zinaweza kuleta madhara.
  1. Aina ya kuku watakaochanjwa:

Kuku wanaofugwa kwa ajili ya nyama wanahitaji kinga ya muda mfupi, hivyo chanjo moja inaweza kutosha. Kuku wa mayai na kuku wazazi wanahitaji mpango wa chanjo itakayowakinga na magonjwa kwa kipindi chote wanapokua na kutaga.

Historia ya magonjwa katika banda Kabla ya kuandaa mpango wa chanjo, lazima ufahamu ni magonjwa gani yaliyoenea katika shamba. Kama unataka kuingiza kuku wapya kutoka mahali ambako ugonjwa umeshawahi kutokea, kuku hao wachanjwe wiki 3 kabla ya kuwaingiza bandani. Iwapo utatumia chanjo yenye vimelea hai, hakikisha kwamba magonjwa hayo yameshawahi kutokea katika banda husika.

Usitumie chanjo hizo katika shamba ambalo ugonjwa huo haujawahi kutokea au kutambuliwa. Wasiliana na wafugaji jirani kufahamu iwapo wanatumia chanjo zenye vimelea hai.

  • Hakikisha unazingatia kwa makini masharti ya mtengenezaji wa chanjo: Jinsi ya kuhifadhi, kutayarisha na njia inayotumika kumchanja kuku. Wakati wote zingatia masharti ya mtengenezaji kuhusu uhifadhi wa chanjo ili isipoteze nguvu.
  • Fuata ushauri wa daktari wa mifugo unapoandaa mpango wa chanjo
  • Watumie wataalamu waliopatiwa mafunzo ya utoaji chanjo
  • Chagua aina ya chanjo kulingana na umri na hali ya kiafya ya kuku
  • Fanya usafi wa mara kwa mara katika mabanda ili kupunguza wingi wa vimelea kwenye mazingira
  • Tumia maji ambayo hayajawekwa dawa au kemikali kwa ajili ya kuchanganyia chanjo, kwa mfano maji ya kisima, mvua na kadhalika. Maji ya kuchanganyia chanjo yawe na ubaridi, yasiwe moto.
  • Changanya chanjo kabla ya kutumia na iwekwe mbali na kuku.
  • Pata ushauri wa daktari wa mifugo kabla ya kuchanja kuku wagonjwa au wale ambao hawako katika muonekano mzuri.
  • Siku ya chanjo, usiwape kuku maji kwa saa 3 – 4 ili waweze kunywa maji yaliyowekwa chanjo kwa haraka.
  • Zoezi la uchanjaji lifanyike haraka ili kupunguza usumbufu kwa kuku.
  • Tenganisha kuku waliochanjwa na wale ambao hawajachanjwa.
  • Baada ya kuchanjwa, kuku wawekwe kwenye banda linalopitisha hewa vizuri.

Leave a Reply