You dont have javascript enabled! Please download Google Chrome!

KUELEKEA SIKU YA KICHAA CHA MBWA DUNIANI SEPTEMBA 28, MFUGAJI WA MBWA UMECHANJA MBWA WAKO?

KAULI MBIU YA MWAKA HUU «ELIMISHA, CHANJA, TOKOMEZA»

Kulingana na kauli mbiu hapo juu, Tovuti yako uipendayo ya Ufugaji inatekeleza kauli hiyo kwa kutoa elimu bure kwa wafugaji wote ili wajue namna bora ya kupambana na magonjwa mbalimbali ya mifugo. Sehemu ya pili na ya tatu ya kauli mbiu ya mwaka huu ni kuchanga mbwa wako kwa lengo la kutokomeza ugonjwa wa kichaa cha mbwa hapa nchini unaoleta madhara makubwa kwa mbwa na binadamu.

Pasi na shaka kila mtu mfugaji na asiye mfugaji anafahamu fika hatari ya ugonjwa huu hasa pale unapomfika binadamu kwa kutokutibika hasa dalili zinapojitokeza. Hivyo kinga ni bora kuliko tiba, ni msemo muhimu unapaswa kutekelezwa kwa vitendo kwa kila mfugaji na asiye mfugaji wa mbwa. Mfugaji ndiye mwenye nafasi kubwa ya kuokoa uhai wa binadamu kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa hasa kwa kuchanja mbwa wake kila mwaka.

Je, wewe umekwisha kuchanja mbwa wako kwa mwaka huu? Kama bado hujafanya hivyo, wahi sasa hujachelewa kutimiza wajibu huo ili tushirikiane kutokomeza ugonjwa huu hatari wa kichaa cha mbwa. Wasiliana na mtaalamu wa mifugo aliye karibu naye ili uweze kuchanja mbwa wako na kumbuka kufanya hivyo mwakani na kila mwaka. Usomapo ujumbe huu mwambie na jirani yako atimize wajibu huu muhimu wa kuchanja mbwa wake. Mimi nachanja mbwa wangu wewe je?

Endelea kujielimisha zaidi kuhusu ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwa maelezo ya kina kupitia viunganishi hivi hapa chini.

KUZUIA KICHAA CHA MBWA: MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA (MAELEZO YA KINA)

 

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!
%d bloggers like this: