You dont have javascript enabled! Please download Google Chrome!

KUZUIA KICHAA CHA MBWA: MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA (FAQS)

PAKUA APP YA TOVUTI HII YA UFUGAJI HAPA

Kichaa cha Mbwa ni nini?

Kichaa cha Mbwa ni virusi vinavyoambukizwa kutoka kwa mnyama hadi binadamu kupitia kwa mate. Mara vinapoingia kwa mwili hushikilia neva,na husafiri kwa njia ya mfumo mkuu wa neva mpaka kwenye ubongo. Dalili za kwanza za kichaa cha mbwa mara nyingi hazijulikani sana (kichwa kuuma, joto la juu, huzuni, homa) na inaweza kuwa rahisi sana kufanya kosa na kuchanganya na maambukizi mengine. Mara virusi vifikapo kwa ubongo, dalili mabaya huanza, na wakati huo utakua umechelewa kwa tiba. Na hakuna tiba ya kichaa cha mbwa.

 

Kuna aina mbili(2) ya kichaa cha mbwa:

  • FURIOUS RABIES– Aina hii ya kichaa cha Mbwa ndio kipo sana na ndicho kiwapatacho waathirika wengi. Hii ndiyo aina ya kichaaa cha mbwa hatari sana na mara nyingi mgonjwa hawezi pona. Huambatana na kuwa na hasira zisizoeleweka, kuchanganyikiwa, kupiga watu, joto kupanda, kutokwa na mate mengi,kutoka jasho,matatizo ya kumeza chakula, kuona vitu viwili viwili, kuogopa maji, kukakamaa na kupinda mgongo.
  • PARALYTIC RABIES -Aina hii mgonjwa huanza pale dalili za awali kama kawaida na baadae anaanza kuparalaizi/kupooza kuanzia miguuni kupanda kuelekea juu, maumivu ya misuli, baadae kushindwa tembea kabisa, kupumua na hata kifo.

Je, ni mbaya?

Kichaa cha mbwa ni ugonjwa hatari sana, lakini asilimia 100 waweza zuilika kupitia chanjo ya mbwa na matatibabu haraka. Ikienda bila kutibiwa itasababisha mtu kuanguka na kukosa fahamu na hatimaye kufa kutokana na kushindwa kwa mapafu au moyo.

Nawezaje pata kiichaa cha Mbwa?

Kichaa cha mbwa huambukiza kwa njia ya mate ya mnyama aliyeambukizwa,na inaweza kuhamishwa kwa binadamu kupitia;

  1. 1. Kuuma
  2. 2. Kulamba (mate kuingia majeraha yaliyowazi)
  3. 3. Kujikuna (chochote kinachosababisha ngozi kuwa nyekundu na kukulia)

Nini napaswa kufanya kama nimeambukizwa?

Ni muhimu kufuata hatua hizi za huduma ya kwanza ikiwa umejulikana kuwa umeng’atwa na mnyama anaweza kua mwenye kichaa cha mbwa:

1)     Osha jereha na sabuni kwenye maji yanayotiririka kwa dakika15.

2) Tumia antiseptic (Dettol, iodine, betadine) na kuruhusu jeraha kuwa kavu. USIFUNGE JERAHA, ikiwa utafunga jeraha kuna uwezekano mkubwa wa kuambukizwa

3) Kwenda hospitali na kupokea sindano 5 kwa siku 0 (siku ya maambukizi), 3, 7, 14 na 28. Uapaswa kuchukua sehemu kamili ya sindano 5.

 

Ninawezaje kujua kama mbwa ana kichaa?

Ni vigumu kutambua kichaa cha mbwa katika wanyama. Njia pekee ya kujua kama mbwa ana kichaa ni kwa kumpima kitaalamu kwa sampuli ya ubongo baada ya kufa. Mnyama anayeumwa kwa kichaa cha mbwa anaweza kuonesha:

  • Dalili ya kuwa na hasira-kutotulia kawaida, kupiga vitu visivyoonekana, kukimbiakimbia bila kusudi, kuuma, kutoka mate mengi, uchokozi na kupooza.
  • Dalili ya kupooza-kupungua kwa mate ,kuanguka kwa taya ya chini na kutokuwa na uwezo wa kumeza.

 

   Nifanye nini kama nahisi Mbwa ana kichaa?

Usikaribie mnyama au kujaribu kumzuia au kujaribu kumdhuru, hii ni hatari sana. Toa taarifa ya mbwa kwa mamlaka husika.

 

Je, watoto wanapaswa ogopa Mbwa?

Watoto hawapaswi kuogopa mbwa, hasa kama mbwa ni rafiki na wanashirikiana. Ni muhimu kwamba watoto wanapaswa kusubiri mbwa wawafikie. Ikiwa wanamsimamo wakashirikiana nao wanapiga mkia wao wanaweza kupigwa kwa upole.

 

Uchokozi ni sehemu ya mawasiliano kwa mnyama yeyote, hata binadamu.Unahitaji tu kuwa na tahadhari ya mbwa ikiwa inakua na mkao mwingi na meno yaliyotokea wakati wapoonya kwamba wanahasira na kwamba wanaweza kukung’ata.

 

Kwanini chanjo kwa mbwa na sio kwa Binadamu?

Mbwa wanaweza eneza ugonjwa huu kutoka kwa mbwa mmoja hadi mwingine ndani ya idadi ya mbwa na wanadamu. Mbwa kuumwa ni wajibu wa asilimia 99 ya kesi ya kichaa cha mbwa kwa sababu ya ukaribu na uhusiano na binadamu. Ni muhimu kukumbuka kuwa si mbwa wote wanakichaa, lakini mbwa wote wanaoumwa wanapaswa kutibiwa isipokua wajue kwamba amekua akipata chanjo ya Mwaka.

Kutoa chanjo kwa Binadamu ni gharama kubwa sana na inahitaji sindani tatu kwa kipindi cha mwezi mmoja. Tayari wote waliopata chanjo bado hawajalindwa na 100% kutoka kwa kichaa cha mbwa,na wanahitajika kypata chanjo mbili baada ya kukumbana na mnyama mwenye kichaa.

Chanjo ya mbwa ni njia ya haraka na haraka zaidi ya kulinda watu na kuacha virusi kwenye chanzo. Mbwa anahita chanjo moja tu   na hulindwa kwa mwaka mzima. Ni jukumu la kila mmiliki wa mbwa kulinda familia na jamii zao kutopata kichaa cha mbwa kwa kuwapa chanjo mbwa kila mwaka.

Je, ni kwavipi chanjo ya mbwa hulinda watu?

Shirika la Afya Duniani (WHO) lilipendekeza kuchanja 70% ya mbwa katika jamii. Hii inafanya kuwa vigumu zaidi kwa virusi  vya kichaa cha mbwa kuenea kwa mbwa ambao hawajapataa chanjo katika eneo hilo.

Je, chanjo hii ni hatari kwa Mbwa wangu ?

Chanjo ni salama kwa mbwa wa umri wowote,pamoja na wenye mimba. Chanjo tunayotumia ni brand itambulikayo kimataifa (MSD Afya ya Wanyama) ambayo imekua kipimo kikubwa na salama. Hatari na madhara ni kidogo sana. Ingawa chanjo hii inalinda mbwa dhidi ya kichaa, hailindi mbwa kutopata magonjwa mengine au ugonjwa ambao unaweza sababisha kifo.

 

Kwanini tusiue mbwa?

Uuaji wa mbwa hautazuia kuenea kwa kichaa Cha mbwa. Maana katika jamii mbwa wanapouliwa,idadi  inaongezeka kwa haraka na wengine kutoka eneo lingine la karibu na pia watoto wa mbwa wengine watazaliwa ambao wanaweza kuwa wameambukizwa kichaa cha mbwa.

 

CHANZO: MBWA WA AFRIKA

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!
%d bloggers like this: