Nguruwe huhitaji kulishwa vizuri ili waweze kukua haraka na kufikia uzito wa kuchinjwa mapema.

Ikiwa watatunzwa vizuri watafikia uzito wa kilo 60 hadi 90 wakiwa na umri wa miezi sita hadi tisa.

Nguruwe ana uwezo wa kula vyakula vya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na mabaki ya vyakula vya nyumbani, shambani na viwandani.

Pamoja na vyakula hivyo, ni muhimu kumlisha chakula cha kutosha, bora na chenye viinilishe vyote vinavyohitajika mwilini. Hata hivyo ili kupunguza gharama mkulima anashauriwa kumlisha vyakula vinavyopatikana katika mazingira yake.

Mfugaji anaweza kuchanganya chakula mwenyewe au kununua kutoka kwenye maduka yanayouza vyakula vya mifugo. Mchanganyiko huo uwe na makundi mbali mbali ya vyakula.

Kuchanganya Vyakula

Chakula kamili lazima kiwe na makundi yote matatu ya kujenga mwili, kutia nguvu najoto na kulinda mwili.Vyakulavya kuchanganya vitatofautiana kutegemea na mahali au upatikanaji wa vyakula hivyo.

Mchanganyiko wa vyakula hivi uwe katika uwiano kufuatana na makundi mbali mbali kwa mfano, chakula cha kukuzia kiwe na:

Asilimia

 Vyakula vya kutia nguvu najoto

65 hadi 75

 Vyakula vya kujenga mwili

20 hadi 25

 Vyakula vya kulinda mwili

– Kalsiumu na Fosforasi

2 hadi 3

– Madini mchanganyiko na chumvi

1.5 hadi 2

Kiasi cha Viinilishe Muhimu Vinavyohitajika kwa Makundi Mbali mbali ya Nguruwe.

Viinilishe vya

Nguruwe wadogo

Nguruwe wanaokua

Majike yenye mimba na kunyonyesha

Madume

 kutia nguvu ajoto (Energy)

13

12.5

12.5

12.5

 Kujenga mwili (CP%)

20

16

14.5

14

 Kalsium (%)

0.90

0.75

0.75

0.55

 Fosforasi (%)

0.70

0.55

0.55

0.45

Mfano wa chakula cha kukuzia Kilo 100

 

Aina

Kilo

Pumba za mahindi

45

Mahindi yaliyosagwa

30

Mashudu ya pamba/Alizeti

15

Dagaa

3

Damu iliyokaushwa

5

Madini

2

100

.

Leave a Reply