Kuhusu Sisi

TOVUTI YA UFUGAJI  ni tovuti iliyobadilishwa kutoka blogu ya SEKTA YA MIFUGO TANZANIA iliyoanzishwa mnamo mwaka 2012 kwa lengo la kumuelimisha mfugaji au mtu anayetaka kuanza ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali namna ya kufanya ufugaji wenye tija. Mfugaji au mfugaji mtarajiwa atajifunza namna bora ya ufugaji na zaidi sana jinsi ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali yanayoikumba mifugo na kurudisha nyuma malengo ya mfugaji.

Malengo ya tovuti hii ni kuendelea na utoaji wa elimu hii ya muhimu kwa wafugaji na wale wanaotaka kuanza ufugaji wajifunze mbinu bora za ufugaji wa mifugo watakayopendelea kufuga. Machapisho yanayowekwa kwenye tovuti hii tunaamini yatawavutia sana watu wote bila kujali kiwango chao cha elimu ili mradi tu anajua kusoma kiswahili kwa maana yanatumia lugha rahisi. Kumekuwa na wimbi kubwa sana la Watanzania kupenda kufuga mifugo mbalimbali ili kujiongezea kipato chao. Changamoto kubwa wanayokutana nayo ni kutofahamu kanuni za ufugaji bora na hivyo kujikuta ndoto yao na matumiani yao yakishindwa kutimia kutokana na kuwa na mifugo yenye afya duni ikishambuliwa na magonjwa mbalimbali. Hivyo tovuti hii ni suluhisho kwa kiasi kikubwa kama ikitumiwa vema na mfugaji.

Wasomaji wetu ni jamii ya wafugaji ambao wana nia ya kujifunza zaidi juu ya kufanya ufugaji utakao saidia kubadilili hali zao za kijamii na kiuchumi na kuwafanya waonekane wenye thamani.  Tovuti hii inalenga zaidi wafugaji wote wanaotumia lugha ya Kiswahili duniani kote. Karibuni tuimarishe sekta yetu ya mifugo.

Washirika wetu ni wadau wote waliopo kwenye sekta ya mifugo wenye lengo la kuwawezesha wafugaji wetu waweze kunufaika na kazi ya ufugaji wakiwemo Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Madaktari wote wa mifugo, Maafisa ugani wa mifugo, Mashirikia yasiyo ya Serikali (mfano Mkulima Mbunifu) na Wafugaji wenyewe. Hivyo mchango wa wadau hawa unahitajika ili kuifanya tovuti hii izidi kuwa na tija kwa wafugaji na wafuatiliaji wa tovuti hii.

 

Muasisi wa Tovuti

Tovuti ya Ufugaji imeanzishwa na inamilikiwa na Dr. Augustino A. Chengula, ukitaka kufahamu Dr. Chengula ni nani na anafanya nini zaidi tembelea tovuti yake hapa

Leave a Reply