BIOSECURITY KATIKA UFUGAJI WA KUKU: SEHEMU YA KWANZA

Biosecurity katika ufugaji wa kuku: sehemu ya kwanzaFig bBiosecurity katika ufugaji wa kuku: sehemu ya kwanza
  1. UTANGULIZI
  2. a) Maana ya Biosecurity

Ni hatua zinazochukuliwa kuzuia au kudhibiti upenyezaji na kusambaa kwa visababishi vya magonjwa kwenye kundi la kuku.

 

Kwa kuwa ufugaji kuku umeongezeka kwa kasi, magonjwa yameongezeka na kutumika gharama kubwa kuyatibu. Magonjwa hayo husababisha hasara kubwa kwa wafugaji.

 

Wafugaji wanategemea zaidi chanjo na antibiotics ili kudhibiti magonjwa kwenye kuku, ambapo wakati mwingine baadhi ya magonjwa hujirudia mara kwa mara.

 

Ili kufanikiwa kudhibiti magonjwa, inabidi kubadili namna ya kufuga kuku, kwa kuangalia jinsi ya kudhibiti na kuondoa magonjwa, kwa kuweka na kutekeleza Kanuni za Biosecurity.

 

Unapoweka na kutekeleza Kanuni za Biosecurity, magonjwa yatapungua sana, na kutakuwa na uhitaji mdogo wa chanjo na antibiotics.

 

Wafugaji wanatakiwa kufanya Kanuni za Biosecurity kuwa sehemu ya ufugaji wa kuku, ili kupunguza magonjwa na kupata mafanikio na faida kwenye ufugaji.

 

  1. b) Lengo la Biosecurity

– Kuzuia uingiaji wa visababishi vya magonjwa kwenye kuku.

– Kuzuia kusambaa kwa visababishi vya magonjwa kutoka eneo moja (banda/hatchery) lenye maambukizi, kwenda eneo lingine (banda/hatchery) lisilo na maambukizi.

 

  1. c) Madhara ya kutokufuata Kanuni za Biosecurity

– Kusababisha magonjwa yanayotibika na yasiyotibika.

– Kutumia gharama kubwa kwenye kutibu magonjwa.

– Kupunguza uzalishaji wa kuku (kupunguza utagaji na uzito wa kuku).

– Kupunguza faida ya mradi wa ufugaji.

 

*d) Vitu vya kuangalia wakati wa kufanya Biosecurity*

– Eneo (location) ya banda/hatchery

– Ujenzi wa banda/hatchery

– Chanzo cha maji

– Magonjwa yaliyopo kwenye wilaya ufugaji unapofanyika

– Umbali na mashamba mengine

– Uwepo na aina ya wanyama pori na ndege pori

– Mwingiliano na watu wanaokuja shambani (wateja, wafanyakazi, wajenzi, mafundi umeme, Mashine, maji)

 

Muhimu:

Vipengele hivi vitaelezewa zaidi kuanzia kesho.

 

*e) Njia ambazo magonjwa yanasambazwa*

 

  1. i) Kuku

– Kuhamisha kuku kutoka sehemu/banda moja kwenye sehemu/banda jingine

– Kuku wa mashamba mengine wanaofugwa huria

 

  1. ii) Ndege/Wanyama wengine

– Ndege wa pori

– Wanyama pori na wanaofugwa

– Wadudu

– Wanyama wagugunaji kama panya

 

iii) Watu

– Wafanyakazi na familia zinazoishi eneo la shamba

– Mafundi wanaofanya matengenezo ya vifaa/banda

– Majirani

– Watoa huduma ya maji/umeme

– Wageni

*Magonjwa yanaweza kusambazwa kupitia mikono, mabuti, viatu, nguo, nywele chafu

 

  1. iv) Vifaa

– Vifaa vichafu

– Kuhamisha vifaa kutoka shamba moja kwenda jingine

 

  1. v) Magari machafu yanayoingia shambani

 

  1. vi) Hewa na vumbi

 

vii) Maji yanaweza kuchafuliwa na uchafu au kinyesi cha ndege na wanyama

 

viii) Chakula

– Kuchafuka kwa malighafi zinazotumika kutengeneza chakula cha kuku, wakati wa kuziandaa au kusafirishwa

– Chakula kikiguswa na kuchafuliwa na wanyama wagugunaji kama panya.

– Bacteria na kuvu kwenye chakula kisicho na ubora au kilichovunda

 

  1. ix) Mizoga ya kuku waliokufa au mayai yaliyoharibika

 

Muhimu:

Mfugaji anatakiwa kuainisha njia ambazo magonjwa yanaweza kuingia na kusambazwa bandani, ili aweke Kanuni za namna ya kuzuia magonjwa hayo yasiingie na kusambaa.

 

MAKALA HAYA YAMEANDALIWA NA:

Aquinus Farms Limited

0655347932

 

.

Leave a Reply