Koksidiosis (coccidiosis) ni ugonjwa unaoshambulia kuku na mifugo mingine kama ng’ombe, mbuzi na kondoo kusbabisha madhara makubwa kwa fugaji yanayotokana na vifo vingi na madhara mengi ya kiafya kwa kuku. Dalili za ugonjwa huu zimelezewa kwa kina HAPA.

Kwa muda mrefu matibabu yamekuwa yakifanyika kwa kutumia dawa iitwayo amproliamu (Amprolium) ambayo huzuia vimelea vya ugonjwa visizaliane lakini pia vife. Miaka ya hivi karibuni tafiti na majaribio mengi yamefanyika kwa dawa mbadala zinatokana na mimea dawa. Zaidi ya mimea maua 300,000 imekwishatambuliwa duniani kote lakini ni chini ya asilimia moja ndo imefanyiwa utafiti kuona kama inaweza kutumika kutibu ugonjwa wa koksidiosisi kwa mifugo.

Mimea ambayo imeonesha matumaini makubwa ya kutibu ugonjwa huu ni pamoja na Mdalasini (Cinnamomum), Artemisia, kitunguu saumu (Garlic), Chai kijani (Green Tea), Majani ya mpapai (pawpaw), mbegu za zabibu (Grape Seed), Ngano (Wheat), Muwa (Sugar Cane). Tazama picha hapa chini.

This year, K.W. Bafundo kutoka New Jersey na wenzake nchini Marekani wamebaini aina mojawapo ya mimiea kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu ugonjwa wa koksidiosis. Kazi yao imechapishwa na jarida maarufu la kimataifa la sayansi ya ndege wafugwao HAPA. Lakini pia unaweza kusikiliza maelezo ya watafiti HAPA.

 

Leave a Reply