Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili Watanzania wengi. Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali . muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha  na hatimae kukuza kuku kwa wingi.

Dondoo ya 1: Usafi wa vyombo na mazingira ya kuku

 • Uchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;
 • Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji na sabuni.
 • Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku vitolowe na kuzikwa.
 • Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.
 • Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.
 • Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.
 • Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.
 • Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.

Dondoo ya 2: Magonjwa na kinga kwa kuku wote

Ndui ya kuku

Huathiri sana vifaranga wanaokua na kujitokeza kwa wingi wakati wa mvua ndefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na mnyoa.

Mdondo/kideri

Mdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari kuliko kati ya magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.

Ukosefu wa vitamin A

Ugonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mbichi.

Koksidiosisi

Huathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokuwa. Kuku hudhoofika manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.

Viroboto, chawa na utitiri

Hawa ni wadudu wa n je wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashinwa kutaga na kuatamia.

Minyoo

Minyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi. Muune mtaalaam ukihisis kuku wako wana minyoo.

Dondoo ya 3: Chakula cha ziada

 • Wapatie vifaranga nyongeza ya protini kwa kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa l vya dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba za mahindi.
 • Changanya kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia kikombe kidogo cha chai).
 • Mchwa na wadudu wengine wanaweza kutumika kam nyongeza ya protini.
 • Vuna mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa katika njia za mchwa.
 • Kutengeneza mchwa: changanya kinyesi cha ng’ombe na majani makavu, mabua ya mahindi au maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya zamani.
 • Mwagia maji hadi kila kilichomo kirowane kisha weka katika chombo kama ndoo au chunngu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa ukikigeuza juu chini na subiri hadi kesho yake asubuh, kisha beba vyote vilivyomo na uwamwagie kuku mahali walipo.

Dondoo ya 4: Utotoleshaji wa vifaranga

Chagua jogoo bora na tetea bora kuzalisha kuku.

 • Sifa za jogoo bora;
 1. Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na usioangukia upande mmoja.
 2. Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo mwenye sifa hizi muweke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini jogoo wawili wanatosha.
 • Sifa za tetea bora;

Tetea bora ni Yule mwenye umbo kubwa, mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha, kuatamia na hatimae kutotoa vifaranga na

 • Uhifadhi wa mayai;
 1. Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.
 2. Tumia box lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na safi au kasha la kuhifadhia mayai.
 3. Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile iliyochongoka itizame chini.
 4. Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.
 5. Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na moja liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.
 • Kuatamiza mayai;

–          Kuku awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa kuyaatamia na kuyatotoa yote.

–          Mayi 10 hadi 12 yanatosha kutamia.

–          Mayai ya kutamiza yasizid wilki 2 toka kutaga.

–          Yai la mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na apewe kuku kuyaatamia.

–          Mayi ya kutamiza yasafishwe kwa kitambaa kikavu  na safi au kilichowekwa spiriti

 • Kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja.

–          Kama unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;

–          Kuku wa kwanza akianza kuatamia muwekee mayai yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa kisasa au kuku asiye na jogoo.

–          Rudia zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano kasha waweke kuku wote mayai yenye mbegu.

Dondoo ya 5: Matumizi ya vifaranga ili kuzuia vifo

Vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na magonjwa, baridi na kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo vya vifarang wa siku 1 hadi miezi miwili zingatia yafuatayo;

Ulinzi dhidi ya mwewe na wanyama wengine.

Weka vifarang kwenye tega na kuwafunika ili wasinde mbali wakati wa mchana. Wape maji na chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa mvua. Wakati wa usiku walale na mama yao.

Chanjo ya mdondo kideri/lufuo

Kama tetea alichanjwa kabla ya kuanzakutaga vifaranga wanaoambuliwa huwa na kinga ya dondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hao dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.

Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku tatu baada ya kuanguliwa, rudia wakifikisha wiki tatu kasha uchanje kila baada ya miezi 3

Kinga dhidi ya kiksidiosisi

Kinga ya koksidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama ugonjwa haujajitokeza.

 • Wape dawa ya aprolium kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea waanguliwe kama kinga ya koksidiosisi.
 • Dawa inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya kiasi cha dawa kinachopaswa kuchanganwa  katika maji au pumba
 • Kama vifaranga wadoga wataonesha dalili za kuzubaa kama kuvua koti wapewe dawa ya amprolium kwenye maji kwa utaratibu ufuatao;

Dawa siku tatu mfululizo: usiwape kwa siku mbili; gawa tena kwa siku tatu

 

HITIMISHO

Hakikisha banda na vyombo vya chakula cha kuku na visafi kuepusha magonjwa.

 • Usichanganye kuku na bata katika banda moja
 • Lisha chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.
 • Kideri, koksidiosisi, ndui na upungufu wa vitamin A ni vyanzo vikuu vya vifo vya kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako dhidi ya magojwa haya.
 • Kumbuka kuchagua mayai ya kuatamiza kama ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.
 •    Vifaranga wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo mazuri fuata maelezo kuzuia vifo.
 • Kumbuka ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga kwa wingi ili upate kuku wengi baadae.
 • Muone mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa ushauri zaidi.
 • Soma maelezo haya mara kwa mara na ufanye yalioelekezwa.
 • Washirikishe wengine katika kaya yako ili nao wajifunze na kufanya, ivyo kukuza ufugaji na kipato cha familia.

 

CHANZO: Makambako Kwetu

By

Leave a Reply