Huu ni ugonjwa hatari sana kwa kuku na jamii nyingine za ndege pia hupata binadamu
Husababisha vifo vingi sana vya ndege na binadamu wakipatwa huweza kufa pia.
MAAMBUKIZI
Ugonjwa huambukiza kwa njia ya hewa, hewa, maji, kugusana, macho, midomo, na pua.
DALILI ZA UGONJWA
Dalili nyingi za Mafua ya ndege hufanana na ugonjwa wa kideri
JINSI YA KUDHIBITI UGONJWA
— Hakuna matibabu
— safisha Mabanda
— kunawa vizuri Baada ya kushika mzoga wa kuku aliekufa kwa ugonjwa
— kaa mbali na mizoga iliyokufa kwa ugonjwa
— tenganisha kuku wazima na wagonjwa
— fukia au choma mizoga ya kuku
— usiuze au kununua kuku wagonjwa
— usile kuku mgonjwa au aliekufa
— tenganisha kuku wageni na wenyeji kwa muda wa wiki 2
–toa taarifa ofisi ya mifugo unapoona dalili za ugonjwa
ANGALIZO
Mafua makali ya ndege mpaka sasa hayajawahi kuingia TANZANIA
Hata hivyo tunatakiwa kuwa waangalifu tunapoona ugonjwa wa Mafua ukiwapata aina tofauti ya jamii ya ndege pamoja na binadamu kwa wakati mmoja.
Kama tukiona hivyo tunatakiwa kutoa taarifa ofisi ya mifugo haraka..