Huduma za ugani hutolewa na wataalam wa mifugo wa Serikali wa Halmashauri, pamoja na sekta binafsi katika kliniki na vituo vya mifugo.
Huduma zinazotolewa na Wataalamu wa Mifugo wa Serikali:-
- Kutoa tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya mifugo
- Kutoa elimu na ushauri kwa wafugaji kuhusu kanuni za ufugaji bora
- Uhamilishaji (A.I.) na kupima mimba
- Ukaguzi wa nyama na ngozi
- Kutoa vibali vya kusafirisha mifugo
- Kutoa vibali kwa watu walioumwa na mbwa/wanyama kuweza kupata chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kichaa cha mbwa katika hospitali za binadamu.
Huduma zinazotolewa na wataalam wa sekta binafsi:
- Kutoa tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya mifugo
- Kutoa elimu na ushauri kwa wafugaji kuhusu kanuni za ufugaji bora
- Uhamilishaji (A.I.) na kupima mimba