ASF - JIFUNZE NAMNA BORA YA KUPAMBANA NA MLIPUKO WA HOMA YA NGURUWE

Mlipuko wa homa ya nguruwe umekuwa ukijitokeza karibu kila mwaka ndani ya nchi yetu kwa maeneo tofauti. Mara nyingi mlipuko umekuwa ukijitokeza maeneo hasa ya mikoa iliyo kwenye barabara kuu kuanzia Mbeya hadi Dar es Salaam. Maeneo mengine imekuwa ni mikoa ya Arusha na Manyara. Na hii imesababishwa kwa kiasi kikubwa na aina ya ufugaji huria unaofanywa na wafugaji na kusababisha milipuko maeneo yao. Mwaka huu mlipuko wa ugonjwa umeripotiwa mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria, maeneo mengine haujaripotiwa. Lakini upo uwezekano wa kuenea maeneo mengine endapo wafugaji wa wadau wengine wa ufugaji wa nguruwe hawatachukua hatua za makusudi za kupambana na mlipuko huo na kuuzuia maeneo ulipo.

Ili kupambana na ugonjwa huu Serikaliimetuma timu ya wataalamu wake kwenda eneo husika kwa minajiri ya kuchunguza na kuweka mikakati dhabiti ya kuzuia ugonjwa usitoka eneo husika na kusambaa maeneo mengine pamoja na kutoa elimu sahihi ya kupambana na ugonjwa huu.

Serikali imewataka wadau wote wa ufugaji wa nguruwe na wananchi kwa ujumla kuzingatia yafuatayo;

  1. Kuepuka kusafirisha nguruwe kutoka maeneo yenye mlipuko kwenda maeneo yasiyo na ugonjwa
  2. Kutokununua nguruwe au mazao yake kutoka katika maeneo yaliyoathirika na ugonjwa
  3. Wanunuzi wa nguruwe kutoruhusiwa kuingia kwenye mabanda ya nguruwe na kuchangua nguruwe kwani wanaweza kusambaza vimelea vya ugonjwa
  4. Wafugaji waepuke kulisha mabaki ya vyakula toka kwenye mahoteli au nyumba za kuuza vyakula kwani yanaweza kuwa na vimelea vya ugonjwa
  5. Wafugaji wanunue chakula kutoka maeneo yasiyo na ugonjwa
  6. Wafugaji wasiruhusi kila mtu kuingingia bandani, mhudumuni pekee ndo aruhusiwe kuingia bandani
  7. Wafugaji wapulize dawa ya kuua vimelea vya ugonjwa pamoja na dawa ya kuua kupe anayeeneza ugonjwa huu

Maelezo zaidi ya serikali yanayotoa tahadhari na hatua za kuchukua yanapatikana kwenye video hii hapa chini

MAELEKEZO YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI AKITOA MAELEKEZO YA NAMNA YA KUPAMBANA NA MLIPUKO WA HOMA YA NGURUWE

 

Tovuti hii ya ufugaji imeulezea ugonjwa wa homa ya nguruwe kwa kina sana siku za nyuma, kama ulipitwa unaweza kujielimisha kupitia viunganishi hapa chini;

  1. UJUE UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE
  2. FAHAMU NAMNA YA KUPAMBANA NA HOMA YA NGURUWE
  3. UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE

 

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!