Kwa kawaida mwili unahitaji vitu vikuu kama vitano kwenye chakula
- Nishati au energy
- Protein
- Vitamin
- Madini au minerals
- Maji
Hi ni sayansi ambayo hata enzi za somo la sayansi kimu tulijifunza hvo starudia kwa leo.
Sasa tukirudi kwenye mada jinsi maneno hayo yanavyotumika.
Energy: kwa kawaida kwenye chakula iko katka packge. Unapompa chakula huwa kama akikila chote mfano kilo moja kwa ubora wowote uliomo atapata kitu kinaitwa Gross energy GE. Sasa akishakila, si chote kitaingia mwilini, kuna ambacho kitańdoka na kinyesi hvyo hakitaingia mwilini. Hivyo ukichukua GE kutoa kitakachopotea kwenye kinyesi utapata kitu kinaitwa digestible energy DE.
Hicho tunatarajia kiingie kama nishati kwenye damu. Lakini hata hicho pia hakitafanya kazi chote kwa manufaa ya mwili, kuna kias kidogo kitatoka kama gas na mkojo. Hvyo digestible energy iliyoingia mwilini kutoa hyo inapotea kwa mkojo, gas nk unapata kitu kinaitwa metabolizable energy ME. Sasa hata hii ME baadhi itatumika kutoa joto mfano kupasha mwili joto mwili, mfano wakati wa baridi, kupotea wakati wa joto nk. Hivyo ukitoa hiyo nishati inayopotea kutoka kwenye ME unapata Net energy ambayo hyo ndo faida ya mwili kujenga nyama, kukua, kuzalisha maziwa kama, kutaga mayai nk kutegemea na aina ya mnyama.
Hivyo utaona hadi unafika net energy ni kiasi gani cha nishati kinakuwa kimepotea kabla ya kutumika kwa manufaa. Hvyo kama ulianza na makapi ya chakula chenye GE ndogo ni kwa kiwango gani chenji inayobaki inavyoathiri ufanisi kwa mnyama. Hata kama ni bora lakini hakijaandaliwa kwa particle ndogo sana maana yake utapata DE ndogo na kinyesi kitaondoka na chenji kubwa.
Kwa kawaida ili mnyama afanye vizuri inabidi angalau chakula kiwetna uwezo wa kutoa ME isiyopungua 11MJ/kg. Na 1MJ =239.006Kacal/kg hyo utaona kuwa michanganyiko yako unayofanya angalau upate 11*239.006=2629.066kcal/kg.
Kwa upande wa crude protein hii ni protein ghafi ambayo iko kwenye chakula chenye asili ya protein kama nafaka, mikunde, samaki, wanyama nk. Kaz ya protein ni kujenga mwili, ukuaji nk. Kila kundi la wanyama lina mahtaji maalum ya kiasi cha protein.
Mfano nguruwe, starter angalau iwe kati ya 18-23, grower iwe angalau 18% na finisher angalau si chini ya 16% , wenye mimba angalau 16-17%, umri mwingine angalau isiwe chini ya 15%.
Sasa hi unaipataje?
Lazima ujue vyanzo vyako vya mchanganyiko wa chakula shambani.
Mfano, last time nilipima vyakula vifuatavyo na CP kwenye mabano.
- Unga wa panki (38.8%)
- Soya kavu (47.59)
- Pumba mahindi (11.8)
- Mashudu alizet (22.9)
- Pumba mpunga (10.4)
Sasa hizo % zinamaanisha nini????! Mfano ukisema mashudu ya soya CP ni 47.59 maana yake kwenye kilo moja ya mashudu protein pekee ni ni 475.9g au 0.4759kg. Hivyo kama tungesema kuwa labda tunachanganya chakula cha watoto wadogo starter iwe na 20 CP mchanganyiko wote tungeanza kuangalia material zote tulizonazo tuzibalance hadi kwenye mchanganyiko kuwe na protein kiasi cha 20,000g au kilo 20.
Hyo ni homework nakuachia wewe. Ukitaka tuidadavue maana yake tukimaliza ndo utajua kama santula wako ukiwalisha hivyo watakulipa au unataka nikutie pressure bure?
Na je, pure duroc ukimlisha hivyo utamuuza kwa 65k??.