KANUNI ZA MSINGI
- Wape kuku lishe jnayofaa na maji safi haswa vifaranga wadogo.
- Wajengee mabanda/nyumba ya kujisitiri dhidi ya upepo na mvua.
- Safisha nyumba ya ndege mara kwa mara.
- Ikiwa ni lazima wapatie takataka kavu mara kwa mara.
- Usiweke ndege wengi pamoja.
- Aina tofauti za ndege kwa mfano kuku,bata mzinga na bata wanafaa kutenganishwa.
- Watenganishe vifaranga na ndege wakubwa ila tu kwa mama yao.
- Chanja vifaranga dhidi ya magonjwa muhimu na wachanje mara tena ikikulazimu. Kumbuka ni ndege tu walio na afya bora (wasio na ugonjwa) wanafaa kuchanjwa.
- Watenge ndege wagonjwa-ikiwa matibabu hayapatikani waue ndege wagonjwa.
- Choma ama zika ndege waliouliwa.