Site icon Ufugaji Bora

Kanuni za ufugaji bora wa kuku

Jinsi ya kuzuia kuku wako wasipate magonjwa

P

Watu wengi hapa nchini hujihusisha na ufugaji wa kuku kwa lengo la kujipatia chakula na kipato. Mazao yatokanayo na ufugaji wa kuku ni pamoja na mayai, nyama, mbolea na manyoya kwa matumizi mbalimbali. Mifumo ya ufugaji kuku ambayo hutumika hapa nchini ni huria, nusu huria na shadidi. Ufugaji wa kuku utakuwa endelevu na wenye tija kwa kufuata kanuni za ufugaji bora zifuatazo:-

 

  1. Banda la Kuku

Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali. Banda bora la kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

 

1.1  Vifaa Vinavyotumika kwa  Ujenzi wa Banda

Vifaa vya kujengea banda vizingatie gharama na upatikanaji wake katika eneo husika. Baadhi ya vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-

 

1.2 Ukubwa wa Banda

Ukubwa wa banda utategemea idadi ya kuku na aina ya kundi la kuku. Kuku wanahitaji nafasi tofauti kutegemea umri, aina na njia ya ufugaji. Eneo la mita moja ya mraba linatosha kwa vifaranga 16 wa umri wa wiki 1 – 4. Hivyo banda lenye mita za  mradi 16 linaweza  kulea vifaranga  320 hadi wiki 4. Baada ya wiki 4 eneo hili liongezwe kutegemea  aina ya kuku na njia inayotumika katika ufugaji kama inavyoonekana kwenye jedwali Na. 10

 

Jedwali Na 10: Eneo Linalohitajika Kufuga Kuku Kwenye

Sakafu ya Matandazo Kutegemea na Umri na Aina ya Kuku

 

Umri wa Kuku Idadi ya Kuku kwa mita 1 ya mraba
Kuku  wa  mayai Kuku wa nyama
Siku 1 hadi wiki 4 18 18
Wiki ya 5 hadi ya 8 9 9
Wiki ya 9 hadi 20 6
Wiki 21 kuendelea 3-4

 

Angalizo:

Mabanda yanayozungushiwa wigo kama ilivyo katika mfumo wa nusu huria, kuku mmoja huhitaji eneo la wazi lenye ukubwa wa mita za mraba 10. Mfano, kuku 100 huhitaji eneo la mita za mraba 1000

 

1.3   Vifaa na Vyombo Muhimu

 

Mfugaji anashauriwa kutumia vifaa na vyombo maalum ili kurahisisha na kuboresha  utunzaji wa makundi mbalimbali ya kuku. Vifaa na vyombo vinavyohitajika kwa ajili ya kuwekea chakula na maji, kutagia mayai na kupumzika vinapatikana kwenye maduka ya pembejeo za mifugo. Aidha, mfugaji anaweza kutengeneza mwenyewe kwa kutumia malighafi zilizopo kwenye mazingira yake.

 

2        Uchaguzi wa Kuku Bora wa Kufuga

2.1      Kuku wa Asili

Aina za kuku wa asili wanaopatikana hapa nchini ni pamaja na Kuchi (Kuza), pori  (Kishingo), Njachama, Kinyavu, Mbuni na Tongwe (Msumbiji). Mfugaji anaweza kuongeza uzalishaji kwa kuchagua kuku mwenye sifa zifuatazo:-

 

Jedwali Na 11: Masuala ya Kuzingatia Wakati wa Kumchagua Kuku

Mtagaji Asili

Viungo vya mwili Sifa
Macho Maangavu, yenye wekundu kwa mbali na

makubwa yamejaa kwenye soketi za macho.

Mdomo Wenye rangi ya njano kwa mbali
Kisunzu/Upanga Chekundu, Laini,kimelala kidogo upande na kinang’aa
Shingo Iliyosimama
Umbali kati ya kidali na nyonga Upanga wa vidole 3-4 vya mpimaji
Upanga wa nyonga Upana wa vidole 3 vya mpimaji

 

 

2.2    Kuku wa Kisasa

Kuku bora  wa kisasa kwa ajili ya mayai au nyama ni mwenye sifa zifuatazo:-

 

2.3     Uchaguzi wa Jogoo Bora wa Mbegu

Jogoo wa mbegu anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-

 

3            Mayai kwa Ajili  ya Kutotoa  Vifaranga

 

3.1          Uchaguzi wa Mayai

Mayai kwa ajili ya kutotoa vifaranga yawe na sifa zifuatazo:-

Yaliyorutubishwa na jogoo,

 

3.2                Utunzaji wa Mayai

 

Mayai ya kienyeji kwa ajili ya kutotoa vifaranga yatunzwe kwa kusimamishwa wima sehemu iliyochongoka ikiwa imeangalia chini kwa siku

3 za mwanzo na kisha yageuzwe ili sehemu iliyobutu iangalie chini. Mayai

yahifadhiwe kwenye sehemu iliyo na ubaridi kidogo na giza.

 

  1. Utunzaji wa Kuku kwa Makundi

 

  1. Utunzaji wa Vifaranga

Malezi bora ya vifaranga ni muhimu katika ufugaji wa kuku kwa sababu vifaranga hawana uwezo wa kustahimili mazingira wakiwa wenyewe mara wanapoanguliwa.Ukosefu wa malezi bora  husababisha vifaranga kuwa dhaifu,kufa kwa wingi na hivyo kupunguza idadi ya kuku wa baadaye. Malezi ya vifaranga yanaweza kufanyika kwa kutumia kuku walezi au kutumia vifaa maalum.

 

Kulea Vifaranga kwa Kutumia  Kuku Mlezi

Vifaranga wanaweza kulelewa na mama yao au kuku mlezi. Endapo kuku wengi wametotoa vifaranga kwa wakati mmoja, achaguliwe kuku mlezi

aliye na uwezo wa kulea vifaranga wengi  kati ya waliototoa aendelee kulea

na wengine waliototoa waachwe huru ili warudi kwenye mzunguko wa kutaga. Kuku mmoja anaweza kulea vifaranga 20 hadi 25. Mfugaji wa kuku,pamoja na kanuni nyingine, anapaswa kuzingatia yafuatayo:-

 

Kulea Vifaranga kwa  Kutumia  Bruda

Bruda ni chombo/sehemu iliyoandaliwa mahusus kwa ajili ya kuwapatia joto vifaranga badala ya mama/mlezi. Mfugaji anaweza kulea vifaranga wengi kwa kutumia bruda ambayo ni mduara unaweza kutengenezwa kwa kutumia mbao, karatasi ngumu au kwa kuziba pembe za chumba.Aidha, njia hii hupunguza vifo vya vifaranga vinavyosababishwa na ndege au wanyama hatari,huruhusu kuku kutaga mapema zaidi na kuwa na mizunguko mingi ya utagaji (kwa kuku wanaoatamia). Vilevile, hurahisisha udhibiti wa magonjwa.

 

Mfugaji anapaswa kufuata taratibu zifuatazo katika kulea vifaranga kwa kutumia bruda:-

 

Wiki ya  kwanza ni 35oc, wiki ya pili ni 33oc, wiki ya tatu ni 31oc na wiki ya nne  ni 29oc,

21 na kila baada ya  miezi 3) na Gumboro (siku ya 7na kurudia tena siku ya 21).Wapatiwa dawa ya minyoo (wiki ya 8) na coccidiosis(wiki ya 3-4). Siku ya 45 wapewe chanjo ya ndui ya kuku.

 

  1. Kutunza Kuku Wanaokua (Wiki 8-18)

Utunzaji wa kundi hili unategemea mfumo unaotumika.

 

Kuku  Wanaofugwa  Katika Mfumo Huria

Kuku  wanaofugwa katika mfumo huu wapatiwe matunzo bora yakiwemo yafuatayo;

 

Kuku Wanaofugwa  Katika Mfumo Shadidi

60 na kuanzia wiki ya 16 gramu 65-80 kwa wanaofugwa mfumo huria na gram 120-125 kwa kuku kwa siku kwa wanaofugwa mfumo wa shadidi,

 

  1. Kuku Wanaotaga

Mahitaji ya kuku wanaotaga ni tofauti na makundi mengine.

Mambo ya kuzingatia kwa kuku wanaotaga ni pamoja na:-

5).Viota viwekwe bandani mara kuku watakapofikisha  umri wa wiki 18 ili waanze kuzoea kuvitumia,

 

Udhibiti na Tiba  Dhidi ya Magonjwa ya Kuku

Kuku wanaopata lishe bora, kutunzwa  vizuri na kupatiwa chanjo dhidi ya magonjwa yanayotokea mara  kwa mara huwa na afya nzuri. Ni bora kuzuia magonjwa kuliko kutibu ili kupunguza vifo na gharama. Iwapo ugonjwa utatokea kuku wagonjwa watenganishwe   na kuku wasio  wagonjwa  na  wapatiwe  tiba.  Kanuni  muhimu za  kufuata ili kuzuia magonjwa ni:-

 

Dalili za Kuku Mgonjwa

Dalili  za  ujumla  zinazoonekana  kwa  kuku  mgonjwa  ni  kama zifuatazo:-

Mfugaji anapoona mojawapo ya dalili hizo atoe taarifa kwa mtaalum wa mifugo

 

Ufugaji wa Aina Nyingine  za Ndege

Aina ya ndege wengine wanaofugwa hapa nchini ni pamoja na Bata maji, Bata bukini, Bata bukini, Kanga na Njiwa. Ndege hao hufugwa kwa kiasi kidogo ukilinganishwa na kuku kwa kuwa soko lao ni dogo.Utunzaji wao hautofautiani sana na kuku;

 

Utunzaji wa Kumbukumbu

 Utunzaji wa kumbukumbu ni muhimu sana katika ufugaji wa kuku na ndege  wengine  wafugwao  ili  kusaidia  mfugaji  kujua  maendeleo  ya ufugaji wake. Utaratibu wa kuweka kumbukumbu mara tukio linapotokea ni lazima ili kuepuka kusahau.Mfugaji ahakikishe anaweka kumbukumbu ambazo ni sahihi na zinazoeleweka.

 

Aina za Kumbukumbu

Kumbukumbu zinazopaswa kuwekwa ni pamoja na:-

 

Chakula na uchanganyaji wake

Chakula ndicho huchangia sana katika gharama za uzalishaji kwa zaidi ya asilimia 60. Na gharama ya chakula huongezeka kila mwaka kuliko hata gharama za mayai au kuku wenyewe.

Mfugaji anaweza kununua chakula kilichochanganywa au kuchanganya  mwenyewe.  Ila  anapaswa  kuzingatia  virutubisho  na viini lishe vilivyopo katika chakula hicho pia kuzingatia mahitaji ya kuku wake.

Virutubisho vinavyotakiwa ni vingi lakini vimegawanywa katika makundi sita ya vyakula ambavyo ni; protin, wanga, mafuta, madini,vitamini na maji.

Protini inahitajika kujenga mwili wa kuku. Ni muhimu kwa ukuaji wa kuku,  uzalishaji wa mayai na kuimarisha afya. Wanga na mafuta vinahitajika ili kuupa mwili nguvu na joto na kuwezesha mwili kufanya kazi zake ipasavyo. Vitamini vinahitajika ili kumwezesha mwili wa kuku kufanya kazi zake vizuri. Madini yanahitajika ili kuimarisha mifupa na uzalishaji.

 

Uchanganyaji wa chakula

Vyakula Vifaranga

Nyama

Nyama

kuzia

Vifaranga

Mayai

Mayai

Kuzia

Mayai

Taga

Ng’ombe

maziwa

Mahindi 38 28 28 26 20 0
Pumba

mahindi

19 26 24 30 30 40
Pumba

mpunga

15 18 24 25 30 33
Mashudu

alizeti

8 8 6 5 6 15
Soya 4 6 6 5 6 5
Dagaa 10 7 5 3 3 0
Damu 4 5 4 3 2 0
Chokaa

mifugo

1 1 2 2 2 5
Madini 0.5 0.5 0.5 0.5 0.5 1.5
Chumvi 0.5 0.5 0.5 0.5 0.5 0.5
Jumla 100 100 100 100 100 100

 

Exit mobile version