Ugonjwa huu husababishwa na bacteria Pasteurella multocida.
Kuenea
Ugonjwa huu huenea kutoka kwa kuku mmoja kwenda kwa mwingine kupitia maji na chakula kilichochafuka.
Wadudu kama nzi na utitiri mwekundu na wanyama kama panya pia hueneza ugonjwa huu.
Dalili
- -Vifo vya ghafla bila ya kuonyesha dalili kwa kuku wengi huwa
- – Kuku waliokufa huwa na rangi ya blue kwenye panga na ndevu zao
- – Kuku wagonjwa hunyong’onyea na kukosa hamu ya kula.
- -Ute mzito hutoka mdomoni
- -Kuharisha
- -Manyosha yasiyo na mvuto
- -Kupumua kwa kasi
- – Utagaji mayai hupungua kwa 5-15%.
- – Upanga na ndevu za kuku huvimba
Matibabu
– Dawa za antibiotics hutibu ugonjwa huu.
– Muone daktari mara tu uonapo dalili za ugonjwa huu ili akushauri dawa ya kuwapa.
– Kuku apatapo dawa mapema, hupona haraka.
Kuzuia
– Banda liwe safi muda wote.
– Vyombo vya maji viwe safi muda wote.
– Hakikisha chakula hakichafuki.
– Hakikisha wadudu kama nzi na utitiri mwekundu na wanyama kama panya hawaingii bandani.
Imeandaliwa na
Aquinus Poultry Farm
0655347932