- Kujazana
Kuku wakijazana kwenye banda lenye nafasi ndogo huanza tabia ya kudonoana.
- Kuboreka
Kuku hupenda kuparuaparua na kuzunguka zunguka. Wakikosa nafasi na vitu vya kudonoa donoa huanza kudonoana wenyewe kwa wenyewe.
- Msongo / Stress
Banda lenye joto sana na lisilo pitisha hewa vizuri huwapatia msongo/stress kuku, na kuku huweza kuanza kudonoana.
- Kunyonyoka manyoya kwa kila mwaka
Kuku wanaotaga kwa kawaida hunyonyoka manyoya kila mwaka. Wakati manyoya yanaota, huwavutia kuku wengine kuwadonoa. Kama hatua za haraka hazitachukuliwa, watadonoana ngozi na kisha nyama, na hivyo kuleta madhara kwa kuku muathirika.
- Upungufu wa protini
Upungufu wa protini kwenye chakula, huweza kusababisha kuku kudonoa manyoya ya wenzao na kuyala ili kuongeza protini kwenye miili yao.
- Kuku walioumia au kuku waliokufa bandani na kuachwa, huwafanya kuku wengine kuanza kudono donoa manyoya na ngozi ya kuku wagonjwa na mizoga na baadaye kudonoa wenzao.
- Kuku wa umri tofauti kuwekwa kwenye banda moja. Kwa kawaida kuku wakubwa huwa na tabia ya kuwadonoa kuku wadogo.
- Viota vichache na mwanga mwingi kwenye viota huwafanya kuku kudonoana.
- Njaa
Kuku wakikaa muda mrefu bila ya chakula na maji huanza kudonoana.
NINI CHA KUFANYA ILI KUTATUA TATIZO LA KUKU KUDONOANA?
- Tafuta sababu za kuku kudonoana
Chunguza kama kuna kitu kinachopelekea kuku kudonoana. Anza na maswala ya mazingira: Je, kuna msongamano?, Wameishiwa chakula au maji?, Hali ya hewa ni baridi sana au joto sana?, Je, wameingiliwa na mnyama au kitu kisichokuwa cha kawaida? Je, kuna kitu nje ya banda kinachowaletea mshituko/mfadhaiko? Baada ya tatizo kufahamika, ondoa tatizo na kila kitu kitakwenda sawa.
- Wawekee sehemu ya kuoga
Hatua nyingine ya kuzuia kuku kudonoana ni kuwaweka katika hali ya usafi. Kuku huwa wanaoga kwa kufukua shimo fupi na kuulainisha udongo wake, na kisha kujifunika na ule udongo, huku wakiendelea kujigaragaza na kujipindua pindua. Kuoga kwa kutumia vumbi ni silika inayowaweka safi.
Kama kuku wanafungiwa bandani muda wote, wawekee beseni kubwa lenye mchanga uliochanganywa na majivu na udongo wa kawaida ili kuku wajigaragaze humo na kuoga.
- Tafuta sehemu/kitu mbadala ambacho kuku wako watadonoa, mfano wafungie mboga za majani kwenye kamba ili wao wazidonoe na kuzila.
- Hakikisha banda lako lina nafasi ya kuwatosha kuku waliomo.
- Walishe chakula bora chenye virutubisho vya kutosha ili wasidonoe manyoya ya wenzao na kuyala.
- Jenga banda linaloingiza hewa ya kutosha ili kuzui kuku kupata msongo /stress.
- Ondoa mara moja mizoga iliyopo bandani. Pia watenge kuku wenye majeraha ili wasiendelee kudonolewa na wenzao.
- Kuku wenye umri tofauti wawekwe kwenye mabanda tofauti ili wakubwa wasiwadonoe wadogo.
- Hakikisha una viota vya kutosha bandani, na kwenye viota kuwe na mwanga hafifu.
- Kuku aliyezidi kudonoa wenzake mtenge kisha umchome au kumpunguza mdomo.
Imeandaliwa na Aquinus Poultry Farm.
Waweza kuwasiliana nao kwa namba hii: 0655347932