Na mwandishi wetu Lucas Michael

Lengo kuu kuchagua kuku wa kuzalisha ni kupata kundi la kuku litakalofaa kwa sifa zote katika uzalishaji. Watu wengi hupenda kufuga chotara ila ukiwauliza hao chotara ni mchanganyiko wa mbegu gani hawajui.  Kwani kuna madhara makubwa pale utakapo fuga kizazi kibaya cha kuku ambacho ndani yake kuna mchanganyiko wa mbegu zaidi ya nne.  Kuku wanaweza kuwa ni wanyonge kwa umbo tu. Yaani hata pale utakapo muangalia kuku unaweza kuhisi kuwa anaumwa, kuku haeleweki kuwa ni waaina gani. Huwa wanachelewa sana kukua, tufuge kwa faida sio kwa ajili ya mapambo tu.
Vipengele vya kuzingatia katika kuchagua kuku bora

– Utoaji wa mayai kwa mwaka uwe mzuri
-Umbile la mwili na njisi aonekanavyo
-Uwezo wa kukua haraka
-Uwezo wa kuotesha manyoya haraka
-Uwezo mkubwa mwilini  wa kutengeneza chakula kuwa mayai au nyama
-Ulaji wa chakuka uwe mdogo ukilinganisha na uzalishaji wake
-Utagaji uwe wa muda mrefu kabla ya kupumzika
– Uwezo wa kuatamia na kuangua vifalanga wengi

Njia zitumikazo katika kuchagua kuku bora

1. Kwa kuangalia kuku mwenyewe kulingana na sifa tajwa hapo juu.
2. Kwa kufuatilia kumbukumbu za wazazi wa kuku unaetaka kumchukua.
3. Kwa kuangalia kumbukumbu za familia/ukoo wa kuku.

Mfugaji unataka ununue kuku kwa ajili ya kwenda kumfuga ni lazima ujue kumbukumbu ya wazazi wa huyo kuku. Je wana maumbo gani?  Je walikuwa wakitaga mayai mangapi? Walikuwa wakiatamia na kuangua vifaranga wangapi?

Ni bora kwa wewe unaeenda kununua vifaranga wa aina fulani kwani unaasilimia nyingi kupata mbegu bora katika hao vifaranga utapata majogoo wazuri, katika hao vifaranga utapata mitetea wazuri. Viranga hao ukiwatunza vizuri baadae utakuwa na kizazi bora unachokijua kumbukumbu yake kuanzia kifaranga.

Kumbuka kuwa na mbegu bora itakusaidia kuongeza kipato na kukuza mradi wako. Kwa sababu mbegu bora inasifa zifuatazo

1. Inakuwa haraka

Kama unavyo jua kuwa kuku anaekuwa haraka hutumia ghalama ndogo hivyo wakati unapo muuza utamuuza kwa bei kubwa kutokana na ukubwa wake. “Wengi sana hupaza sauti zao kusema kuwa ufugaji kuku hauna faida ” Hapana sio kuwa hauna faida ila mbegu ya kuku wanaofuga ndio haina faida. Mbegu mbaya hutumia gharama kubwa katika matunzo na bei ya kuuzwa huwa chini hivyo ni lazima faida isiwepo.

2. Niwasitahivilivu wa magonjwa

Magonjwa yamekuwa changamoto kubwa kwa wafugaji wengi, wengine huacha kabisa kufuga kwa ajili ya magonjwa kwa sababu kuku anaowafuga ni mchanganyiko wa mbegu mbaya hivyo hushindwa kujua ni jinsi gani atakavyo walinda kuku wake na magonjwa.
Endelea kufuatilia Tovuti yako uipendayo ya UFUGAJI kwa makala mpya zinazohusu ufugaji zinazotolewa na WATAALAMU wetu.

Leave a Reply

error: Alert: Imezuiliwa !!