Kwa nini upunguze kuku wako midomo?

UPUNGUZAJI WA MIDOMO YA KUKU

 

  1. Maana.

Ni uondoaji/ukataji wa sehemu ya ncha ya mbele kwenye upande wa juu na wa chini wa mdomo wa kuku.

 

  1. Kwa nini kuku hupunguzwa mdomo?

* Kuzuia kuku kudonoana manyoya na ngozi, inayoweza pelekea vifo vya kuku kwa 25% – 30% kwenye kundi la kuku.

* Kuzuia ulaji/uvunjaji wa mayai.

* Kuzuia majogoo kuumizana wakati wa kupigana.

 

  1. Njia za upunguzaji midomo ya kuku.

* Kwa kutumia mikasi maalumu ya kukatia midomo.

* Kwa kutumia mashine ya umeme yenye wembe wa joto.

* Kwa kutumia kisu cha moto.

* Kwa kutumia mashine yenye mionzi.

 

  1. Midomo ya kuku ipunguzwe wakiwa na umri gani?

Upunguzaji wa midomo hufanyika wakiwa na umri tofauti tofauti kulingana na matakwa ya mmiliki wa kuku. Inaweza kuwa wakiwa na:

* Siku moja.

* Siku 5 – 10.

* Wiki 4 – 6.

* Wiki 8 – 12.

* Wakubwa (Wanaotaga)

 

  1. Faida za kupunguza midomo ya kuku.

* Kupunguza / kuondoa uwezekano wa kuku kudonoana manyoya na ngozi.

* Kupunguza / kuzuia kuku kula mayai.

* Kupunguza / kuzuia majogoo kuumizana wakipigana.

 

  1. Madhara ya kupunguza midomo kuku.

* Kuku wanaweza kupata stress/mshituko kutokana na maumivu wakati wa kupunguzwa midomo, hivyo kupelekea kupungua kwenye ukuaji wao au wanaotaga kupunguza kutaga.

* Kushindwa kula chakula na kunywa maji vizuri. Kuku anakula kwa kudonoa chakula, akipunguzwa mdomo vibaya anaweza kushindwa kula na kisha atadhoofika na hata kupelekea kifo.

 

  1. Nini kifanyike ili kupunguza uwezekano wa kuhitaji kuwapunguza kuku midomo?

* Kuku waachiwe kwenye eneo la kutosha ili waweze kuparua na kudonoa donoa chini. Hii itawapatia kazi ya kufanya na hivyo kutokudonoana.

* Kuku wapewe chakula bora chenye virutubisho ili kuzuia kudonoana wakitafuta protein.

* Kuku wavalishwe vifaa vinavyozuia kuona mbali, kama miwani ya kuku.

 

  1. Sheria ya upunguzaji midomo ya kuku kwenye nchi mbalimbali.

* Australia – Baadhi ya majimbo yanakataza upunguzaji midomo ya kuku, na kwenye majimbo mengine kama Victoria na New South Wales bado kuna mazungumzo kama ikatazwe au la.

* Denmark – Upunguzaji wa midomo ulikuwa unafanyika mpaka mwaka 2014 ilipokatazwa.

* Sweden, Finland na Norway – Hairuhusiwi kukata midomo ya kuku.

* Germany – Waziri wa Kilimo ametangaza kwamba Ujerumani wanaweza kutoa katazo la kupunguza midomo ya kuku mwaka huu 2017 kutokana na masuala ya ustawi wa wanyama.

 

ZINGATIA: Watu wanaotakiwa kuwapunguza kuku midomo ni wale tu wenye ujuzi huo, na watumie njia sahihi za kuwapunguza midomo, bila kumuathiri kuku mlengwa.

 

Imeandaliwa na

Aquinus Poultry Farm.

0655347932

 

 

Leave a Reply