Kinengunengu

MAANDALIZI YA SEHEMU YA KULELE VIFARANGA/ BROODING AREA

 

👆Brooder (kinengunengu), hii ni sehemu ya muhimu sana, na yakuzingatia sana wakati wa malezi ya vifaranga

 

SIFA ZA BROODER

👉Joto lakutosha

👉Randa/matandazo

👉Maji

👉Chakula

👉Hewa ya kutosha

👉Mwanga

👉Nafasi ya sahihi ya kutosha

 

👉👇nini sasa ufanye kuandaa brooder/ sehemu ya kulelea vifaranga.

 

👉Kwanza angalia idadi ya vifaranga wako,

👈Brooder inaweza kuwa ya duara, kama utalea vifaranga wachache

 

👈Kama utalea vifaranga wengi unaweza kutengeneza brooder ya pembe nne kwa kuzingatia vipimo.

 

MATENGENEZO YA BROODER YA DUARA

 

👉Tafuta siling board, ikate kwa urefu vipande vitatu (standard 30-40 cm) kimo, au wengine hukata mara mbili *(katikati)*

 

👉Unganisha vipande ulivyo vikata kutengeneza duara lako, Mimi huunganisha kwa kuchana kibao kwa msumeno kitakacho shikilia siling board upande wa juu kwenye maungio.

 

👉Kitaalamu mita moja mraba hutosha vifaranga 40, ila eneo utakua unalitanua kwa kadri vifaranga watakavo kua wanaongezeka kukua.

 

👉Baada ya kutengeneza brooder yako, Weka randa za mbao au pumba ya mpunga (walau wiki 1 kabla ya kuleta vifaranga)

 

👈Tandika gazeti, au mifuko, au Ground paper.

 

👉Wakati vifaranga wanakaribia  masaa  kadhaa kabla vifaranga kufika weka chanzo cha joto ( vyungu, Bulb, Gas heater). Kama chumba nikikubwa sana na joto litachelewa kushika kwenye sakafu washa masaa 24 kabla ya vifaranga kufika, Joto la sakafu, randa, na maji vinatakiwa vifikie joto la chumba.

 

👉Ingiza vifaranga wako, tayari wakute chakula na maji bandani,

 

 

👉Hakikisha vifaranga wanapata chakula na maji muda wote ili wakue kwa uwiano, hasa wiki 2 za kwanza, ukikosea tu watapishana ukuaji

 

👉Vifaranga waanze kwa chakula cha Starter kwa wiki 6-8 za kwanza kwa kutegemea maelekezo ya chakula unacho tumia.

 

WENYE VIFARANGA WENGI

👉Andaa chumba chakulelea vifaranga, kama kawaida

 

👉Weka joto, vyombo vya maji, vyombo vya chakula

 

👉Hakikisha sana kama unatumia, mkaa madirisha yako yanakua yanaruhusu hewa kuingia , unaacha uwazi kidogo kuepusha baridi kuingia bandani

 

👉Vyanzo vya joto viwepo bandani walau Massa 24 kabla ya vifaranga kufika kuleta joto kwenye sakafu na randa

 

👉Tandika magazeti, au mifuko kwa siku 3-5 na ubadilishe kila yatakapo chafuka ( kilasiku)

 

👉Chakula na maji viwekwe masaa mawili kabla ya vifaranga kufika

 

👉Mita moja mraba vifaranga 40, eneo liongezeke kadri vifaranga watakao kua wanaongezeka

 

👉👈NB muda wa kufanya brooding unatofautiana, maeneo ya baridi wiki 3-4, maeneo ya joto wiki 1-2.

 

VIASHIRIA VYA HALI YA HEWA BANDANI

 

 

👉BARIDI IKIZIDI vifaranga wanakusanyika pamoja, au karibu na chanzo cha joto, suluhu ongeza joto

 

👉JOTO LIKIZIDI, viafaranga wanahema sana kwa kutanua mdomo, wanakaa pembezoni mwa brooder, wanaacha kula, wanakimbia vyanzo vya joto. Suluhu punguza chanzo cha joto

 

👉 Upepo mwingi vifaranga wanazunguka kwa makundi bandani, watakimbia eneo upepo unakoelekea kuja eneo upepo unapo ingilia, Kumbuka upepo unaoingia unakua na baridi

 

👉 Joto sahihi, Vifaranga hutawanyika vizuri bandani, na hula na kunywa maji, hivo ukuaji wao huwa wa kuwiana vizuri.

 

IMEANDALIWA NA

👈👉Greyson Kahise

Mtaalamu wa kuku

0769799728/0715894582

 

Leave a Reply