nini sasa ufanye kuandaa brooder/ sehemu ya kulelea vifaranga.
Kwanza angalia idadi ya vifaranga wako,
Brooder inaweza kuwa ya duara, kama utalea vifaranga wachache
Kama utalea vifaranga wengi unaweza kutengeneza brooder ya pembe nne kwa kuzingatia vipimo.
MATENGENEZO YA BROODER YA DUARA
Tafuta siling board, ikate kwa urefu vipande vitatu (standard 30-40 cm) kimo, au wengine hukata mara mbili *(katikati)*
Unganisha vipande ulivyo vikata kutengeneza duara lako, Mimi huunganisha kwa kuchana kibao kwa msumeno kitakacho shikilia siling board upande wa juu kwenye maungio.
Kitaalamu mita moja mraba hutosha vifaranga 40, ila eneo utakua unalitanua kwa kadri vifaranga watakavo kua wanaongezeka kukua.
Baada ya kutengeneza brooder yako, Weka randa za mbao au pumba ya mpunga (walau wiki 1 kabla ya kuleta vifaranga)
Tandika gazeti, au mifuko, au Ground paper.
Wakati vifaranga wanakaribia masaa kadhaa kabla vifaranga kufika weka chanzo cha joto ( vyungu, Bulb, Gas heater). Kama chumba nikikubwa sana na joto litachelewa kushika kwenye sakafu washa masaa 24 kabla ya vifaranga kufika, Joto la sakafu, randa, na maji vinatakiwa vifikie joto la chumba.
Ingiza vifaranga wako, tayari wakute chakula na maji bandani,
Hakikisha vifaranga wanapata chakula na maji muda wote ili wakue kwa uwiano, hasa wiki 2 za kwanza, ukikosea tu watapishana ukuaji
Vifaranga waanze kwa chakula cha Starter kwa wiki 6-8 za kwanza kwa kutegemea maelekezo ya chakula unacho tumia.
WENYE VIFARANGA WENGI
Andaa chumba chakulelea vifaranga, kama kawaida
Weka joto, vyombo vya maji, vyombo vya chakula
Hakikisha sana kama unatumia, mkaa madirisha yako yanakua yanaruhusu hewa kuingia , unaacha uwazi kidogo kuepusha baridi kuingia bandani
Vyanzo vya joto viwepo bandani walau Massa 24 kabla ya vifaranga kufika kuleta joto kwenye sakafu na randa
Tandika magazeti, au mifuko kwa siku 3-5 na ubadilishe kila yatakapo chafuka ( kilasiku)