Site icon Ufugaji Bora

JINSI YA KUTENGENEZA SEHEMU YA KULELEA VIFARANGA/ BROODER

Kinengunengu

Kinengunengu

MAANDALIZI YA SEHEMU YA KULELE VIFARANGA/ BROODING AREA

 

Brooder (kinengunengu), hii ni sehemu ya muhimu sana, na yakuzingatia sana wakati wa malezi ya vifaranga

 

SIFA ZA BROODER

Joto lakutosha

Randa/matandazo

Maji

Chakula

Hewa ya kutosha

Mwanga

Nafasi ya sahihi ya kutosha

 

nini sasa ufanye kuandaa brooder/ sehemu ya kulelea vifaranga.

 

Kwanza angalia idadi ya vifaranga wako,

Brooder inaweza kuwa ya duara, kama utalea vifaranga wachache

 

Kama utalea vifaranga wengi unaweza kutengeneza brooder ya pembe nne kwa kuzingatia vipimo.

 

MATENGENEZO YA BROODER YA DUARA

 

Tafuta siling board, ikate kwa urefu vipande vitatu (standard 30-40 cm) kimo, au wengine hukata mara mbili *(katikati)*

 

Unganisha vipande ulivyo vikata kutengeneza duara lako, Mimi huunganisha kwa kuchana kibao kwa msumeno kitakacho shikilia siling board upande wa juu kwenye maungio.

 

Kitaalamu mita moja mraba hutosha vifaranga 40, ila eneo utakua unalitanua kwa kadri vifaranga watakavo kua wanaongezeka kukua.

 

Baada ya kutengeneza brooder yako, Weka randa za mbao au pumba ya mpunga (walau wiki 1 kabla ya kuleta vifaranga)

 

Tandika gazeti, au mifuko, au Ground paper.

 

Wakati vifaranga wanakaribia  masaa  kadhaa kabla vifaranga kufika weka chanzo cha joto ( vyungu, Bulb, Gas heater). Kama chumba nikikubwa sana na joto litachelewa kushika kwenye sakafu washa masaa 24 kabla ya vifaranga kufika, Joto la sakafu, randa, na maji vinatakiwa vifikie joto la chumba.

 

Ingiza vifaranga wako, tayari wakute chakula na maji bandani,

 

 

Hakikisha vifaranga wanapata chakula na maji muda wote ili wakue kwa uwiano, hasa wiki 2 za kwanza, ukikosea tu watapishana ukuaji

 

Vifaranga waanze kwa chakula cha Starter kwa wiki 6-8 za kwanza kwa kutegemea maelekezo ya chakula unacho tumia.

 

WENYE VIFARANGA WENGI

Andaa chumba chakulelea vifaranga, kama kawaida

 

Weka joto, vyombo vya maji, vyombo vya chakula

 

Hakikisha sana kama unatumia, mkaa madirisha yako yanakua yanaruhusu hewa kuingia , unaacha uwazi kidogo kuepusha baridi kuingia bandani

 

Vyanzo vya joto viwepo bandani walau Massa 24 kabla ya vifaranga kufika kuleta joto kwenye sakafu na randa

 

Tandika magazeti, au mifuko kwa siku 3-5 na ubadilishe kila yatakapo chafuka ( kilasiku)

 

Chakula na maji viwekwe masaa mawili kabla ya vifaranga kufika

 

Mita moja mraba vifaranga 40, eneo liongezeke kadri vifaranga watakao kua wanaongezeka

 

NB muda wa kufanya brooding unatofautiana, maeneo ya baridi wiki 3-4, maeneo ya joto wiki 1-2.

 

VIASHIRIA VYA HALI YA HEWA BANDANI

 

 

BARIDI IKIZIDI vifaranga wanakusanyika pamoja, au karibu na chanzo cha joto, suluhu ongeza joto