Ufugaji Bora

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUWEKA JOTO KWA VIFARANGA

Ufugaji wa kuku wa mayai hatua kwa hatua: hatua ya pili

Joto guide

UTANGULIZI

Kwanza tuanze kwa kujiuliza ni kwa nini vifaranga huwa wanahitaji kuwekewa joto katika wiki za mwanzo?

Utaratibu bora wa ufugaji wa vifaranga unaelekeza kuwa katika wiki za mwanzo za ufugaji wa kuku wakiwa vifaranga inalazimu wawekewe vyanzo vya joto kwa kutumia taa za umeme au majiko ya mkaa au vyungu vya joto au taa special za umeme. Hii ni kwa sababu zifuatazo ;

 1. Kwa kawaida joto mwili la kuku huwa si chini ya nyuzijoto 40 na huenda hadi nyuzijoto 41 wakati huohuo joto la mazingira huwa linaanzia nyuzijoto 25 hadi 30/32. kwa kawaida joto husambaa kutoka sehemu lilipo jingi kwenda kule lilipo chache, kwa maana hiyo joto litatoka kwenye mwili wa kuku kwenda kwenye mazingira kupelekea kuku kupoteza joto.
 2. Wakati huohuo kifaranga anakua hana idadi kubwa ya manyoya hivyo kupelekea joto kupotea kirahisi zaidi na madhara kuwa makubwa zaidi.
 3. Si hivyo tu, bali ukaribu wa mapafu ya kuku na mazingira huchangia madhara zaidi. Mapafu ya kuku tofauti na binadamu yenyewe yapo mgongoni karibu kabisa na ngozi hivyo kupelekea kupoteza zaidi joto katika hali hiyo.
 4. Vifaranga hawana uwezo madhubuti wa mfumo wa uzalisha wa joto hii ni kwa sababu bado hawajapevuka vya kutosha.

Sababu zote tajwa hapo juu zinapelekea kuku kudhulika zaidi pale ambapo mazingira yanayomzunguka yakiwa na baridi. Hivyo kwa wiki za mwanzo atahitaji kuongezewa joto ili asiweze kupoteza joto na kumpelekea kufa, kuzorota kwa ukuaji na kudumaa.

Joto linalohitajika kwa wiki ya kwanza ni nyuzijoto 35 na joto hili huenda llikipunguzwa kwa nyuzijoto 3 kwa wiki mpaka litakapofikia nyuzijoto 26 kufikia hapo basi vifaranga hawatakuwa wakihitaji tena joto la ziada.

Swali: je, niitajuaje kama hili joto nililoweka linatosha au halitoshi?

Jibu: kuna njia mbili za kujua kama joto linatosha au halijatosha.

Njia ya kwanza inahusisha kutumia kutumia kipimajoto (thermometer) na kupima joto centimeter tano kutoka chini ya brooder na katikati ya brooder.

Njia ya pili inahusisha kutambua joto kwa kuangalia tabia za vifaranga kama ifuatavyo;

Sio lazima kutumia thermometer unaweza kuangalia tabia za kuku na kujua kama joto limezidi au ni dogo kama ifuatavyo:

 1. Kama kuku wanakaribia sana taa/jiko na wamejikusanya sehemu moja yenye chanzo cha joto basi hapo joto ni dogo basi ongeza joto au shusha taa chini.
 2. Kama kuku wanaenda mbali na chanzo cha joto na hawataki kabisa kusogelea chanzo cha joto na pia mda mwingine wanahema kwa kutumia mdomo huku wameinua vichwa basi hapo joto limezidi na yakupasa kupunguza joto/kuzima taa au kupandisha taa.
 3. Kama kuku wametawanyika bandani na wapo kila sehemu na hawana shida yoyote basi hapo jua kuwa joto lipo sawa na haiitajiki kurekebishwa.
 4. Kama kuku wamejikusanya upande mmoja wa banda na upande mwengine upo wazi basi jua kua kuna upepo mkali unatokea uelekeo wa sehemu waliojibanza.

NB: pia vifaranga wanadhurika na joto jingi sana na kupelekea heat stress mwishowe wanakufa Hivyo utambuzi wa kiasi cha joto ni muhimu sana.

Ahsante sana nawatakia utekelezaji mwema:

Pia natoa huduma zifuatazo;

 1. Matibabu kwa mifugo aina zote.
 2. Ushauli juu ya njia bora na za kisasa za ufugaji.
 3. Kutembelea shamba la mifugo na kutoa ushauri kwa chochote ntachokikuta.
 4. Nauza mbegu za azolla na kutengeneza mabwawa ya azolla.

 

Imeandaliwa na;

Rajab Awami Rajab (Bachelor of veterinary medicine (BVM)).

Kwa ushauli zaidi tuwasiliane:

Phone: 0672476889.

WhatsApp: 0672476889.

Exit mobile version