Mambo ya msingi mifugo na kilimo viendelee hapa nchini

Ili mifugo na kilimo viendelee Tanzania ( Mazao, Mifugo na Uvuvi) vinahitaji yafuatayo;

 

Mifugo
Lazima tuwe na mitamba ya mifugo wa kisasa wa maziwa na nyama ili kupata tija kubwa kutokana na kundi dogo

Pili lazima tuwe na maeneo ya malisho ambayo mifugo itakaa kwa uwiano wa kitaalam huku na huduma kama maji, majosho na wataalam yakipatikana hapo, commercial livestockkeeping
Tatu lazima tuwe na viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo ili kuongeza tija ili kuweza kugharamia ufugaji wa kisasa, ufugaji wa kisasa sio holela

Nne Lazima viwepo vituo vya uhimilishaji wa mbegu za kisasa kwa kila kanda na mbegu za majani

Uvuvi

Kwanza; Uvuvi endelevu, lazima kukomesha uvuvi haramu

Pili lazima kuwepo ufugaji wa samaki ili kuondoa over fishing

Tatu lazima kuwe na viwanda vya kuchakata samaki

Nne lazima kuwe na bandari ya uvuvi; Pana safari hapa

Tano lazima kuwe na meli za uvuvi wa bahari kuu.

 

Kilimo

Kwanza; Kilimo cha kutumia Matrekta; Ni lazima kubadili mlinganyo uliopo wa watu wengi kutumi jembe la mkono kwenda watu wengi kutumia matrekta na kidogo kutumia Wanyama kazi. Jembe la mkono linatakiwa kuonekana Makumbusho ya Taifa yaani Miessiums na makaburini.

Pili; Kilimo cha Umwagiliaji, lazima serikali kuunganisha Mikoa kwa mifereji ya Umwagiliaji ili wakulima wayatoe maji kwenye hiyo mifereji kwenda mashambani mwao, pana safari ndefu hapa

Tatu; Matumizi ya Pembejeo, ni lazima mbolea, mbegu bora na dawa zipatikane madukani kama Coca cola inayopatikana popote na kwa wakati, kwa tajiri na masikini na kwa bei ya kumudu kila mtu

Nne Lazima yawepo maghala na viwepo viwanda kwa ajili ya kuyapokea mazao haya kwa kila zao lichakwatwe na kupata by product,mfano kwa Pamba tupate nguo hapahapa nchini, kwa ngozi tupate viatu na mikanda, begi hapahapa, matunda tupate juice hapa hapa nk ili kuondoa post harvest loses

Tano Lazima tuwe nabwataalam na uimara wa vyuo vya utafiti. Lazima wakulima walime kwa kufuata utaalam

 

Mambo haya sio ya mwaka mmoja , sio ya bejeti ya mwaka mmoja, na sio ya serikali pekee yake.  Tutakwenda kwa hatua. Hakuna miujiza na hakuna njia ya mkato bali ni uamuzi wa kuwekeza kwenye kilimo.

“KAMA MNATAKA MALI MTAZIPATA SHAMBANI” by Mwigulu Nchemba WKMU

Mwigulu

Leave a Reply