Ufugaji wa kuku wa mayai hatua kwa hatua: utangulizi

1: Maandalizi ya banda la kuku

Fagia, deki kwa maji, pulizia dawa/disinfection (Th4, V rid,Farm guard nk).

Acha banda likae zaidi ya siku 7 baada ya kutoa kuku wakubwa kabla ya kuingiza kuku wengine.

Andaa vifaa vyote muhimu kwa ajili ya kupokea kuku wapya vikae bandani angalau siku 3 kabla ya kupokea vifaranga.

Andaa sehemu ya kulelea vifaranga, weka vyanzo vya joto tayari kabla vifaranga hawajafika(Usikurupuke kuweka wakati vifaranga wameshafika).

 

2: Maandalizi ya chakula na maji

Hakikisha maji, chakula kwaajili ya kuku wako yapo bandani au sehemu ya karibu muda wote ili kurahisisha ulishaji wa kuku. Chimba kisima au weka tank la kuhifadhia maji na uwe na stoo ya kuhifadhia chakula ( *isiruhusu panya kuingia )*

Hakikisha kuku wamepewa chakula muda sahihi na kwa kiwango sahihi kulingana na umri na aina ya kuku wako.

 

3: Idadi ya kuku bandani

Ili kupelekea ukuaji murua wa kuku, zingatia nafasi sahihi *(idadi sahihi ya kuku kwa mita 1 mraba)*

Mfano( Pure layers 7-8 kwa 1m², Chotara na kienyeji 3-4 kwa 1m², Broilers 10 kwa 1m²,) *hii itakusaidia kutengeneza kuku wanao wiana uzito na maumbo* VIFARANGA 40 kwa 1m².

 

4: Idadi ya vyombo vya maji na chakula

Kwa kuzingatia aina ya na size ya vyombo unavyo tumia , hakikisha kuku wako wote wanapata nafasi sawa ya kula na maji

Mfano

Vifaranga

60-70 kwa chicken drinker 1 kwa wiki ya kwanza kisha punguza mpaka idadi ya 45-50 kwa wiki mbili mbele. Sahani pana  za kulia vifaranga (1kwa vifaranga 60-80).

Kuku wakubwa

Feeder 1 kubwa ya Lita 10 kwa kuku 20-25/30

Drinker 1 ya lita 20 au Belly drinker kubwa kwa kuku 50-60

NB Idadi ya vyombo vya maji na chakula izingatie kwamba kuku wote wanapata nafasi ya kula wakati wa kulisha wasiwepo *wanaozunguka kwa kukosa nafasi.*

 

RATIBA ZA CHANJO

 

Kuku chotara, Pure wa mayai  tumia mwongozo huu kwa chanjo kuu zilizo zoeleka

Siku ya 1 mareks

Siku ya 7 Newcastle (Lasota)

Siku ya 14 Gumboro

Siku ya 21 Newcastle

Siku ya 28 Gumboro

Siku ya 30(wiki 4-5) Ndui *inategemea ukanda ulipo*

Baada ya miezi mitatu rudia new castle.

 

 BROILERS/KUKU WA NYAMA

Siku ya 7 Newcastle

Siku ya 14 Gumboro

Siku ya 21 Newcastle au Gumboro)

Hatuchaji ndui kwakua kuku wanauzwa mapema

Kwa kutegemea eneo lako imezoeleka kuchanja kwa mfumo upi

 

 ULISHAJI WA KUKU

Kuku wa nyama kwa mujibu wa mwongozo wangu Mimi KAHISE.

 

Siku 1 hadi siku ya 13 Broilers Starter Crumble

Siku ya 14 hadi 22 Broilers Grower Pellets

Siku ya 23 mpaka kuuza Broilers Finisher Pellets

(Kuku wapewe vitamins)  Ratiba hii inatofautiana kutoka kwa mfugaji mmoja kwenda kwa mwingine *chamuhimu kuku wafikishe 1.3-1.5 kg kwa siku 30*

 

 KUKU KWAAJILI YA KUTAGA

 

Wiki 2 za kwanza (Broiler starter crumble) kuwakuza haraka na wawe na umbo kubwa mapema.

 

Wiki ya 3 mpaka wiki 7-8 Chick starter Mash.

 

Wiki ya 7-9 Layer Grower Mash mpaka watakapo dondosha yai lakwanza

 

Layers mashi kutoka pale utakapo ona yai la kwanza (kuanzia angalau wiki ya 18-20) kulingana na aina ya kuku mpaka utakapo amua kuwatoa bandani

 

NB Zingatia unapohama kutoka aina 1 yachakula kuingia aina nyingine CHANGANYA VYAKULA HIVYO KWA SIKU 3-4 ili kuwazoesha na kutowapa STRESS.

 

Wape kuku walioanza kutaga jumla ya masaa 16 ya mwanga(Nyongeza ya masaa 4 ya mwanga wa taa) au zima taa usiku saa 4.

 

IMEANDALIWA NA GREYSON KAHISE

MTAALAMU WA KUKU

0769799728/ 071589458

Leave a Reply