Imeandikwa na
GREYSON KAHISE
Mtaalamu wa kuku
0769799728
0788011560
Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji
👉Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti.
👆 Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo.
👉 Chakula
👆Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula.
👏Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo
👉Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja
👉Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili
👉Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili
NB: Zipo shuhuda kwamba broiler 100 wanaweza kutumia mifuko minne pekee mpaka kuuza, hii inategemea sana aina ya vyakula na nafasi yao bandani.
👆Wafugaji wengi wamekua mbali na kulisha chakula wanawapa vitamin , mollases na Booster kama ifuatavyo
👉Neoxychick &multivitamin siku 1-5
👉Vitamin kama Amintoto siku ya 7-10
👉Bro-booster na Mollases siku ya 11-24
👉Avipunch booster siku zilizo salia mpaka kuuza
👉👈 Matumizi hayo ya vitamin sio sheria , kutumika ili kupunguza gharama.
👆 CHANJO
Kwa uzoefu wangu mfumo ambao nimezoea kuutumia
👉Siku ya 7 newcastle/kideri
👉Siku ya 14 Gumboro
👉Siku ya 21 Newcastle
Mfumo B
👉Newcastle siku ya 7
👉Gumboro siku ya 14
👉Gumboro siku ya 21
NB: Ndui haichanjwi kwa broiler, ila kwa wakati mwingine wamekua wakipata ndui iwapo watachelewa kuuzwa
NAFASI
👆Kitaalamu broilers 8-10 wanafaa kukaa kwenye mita moja mraba, hii itasaidia sana kupunguza case za broiler kuchafuka kwa kulowesha maranda.
👆Kiasili broiler wanakunywa sana maji, hii hupelekea banda kuloana sana, hali hii imepelekea wafugaji wengi kuwa na kawaida ya kubadilisha randa Mara kwa Mara
👈Kubadili randa mara kwa Mara kwa mtazamo si sawa, ila unaweza ukawa unatoa palipo lowana sana na kubadilisha na randa kavu, hii itakusaidia sana kupunguza ugonjwa wa Mafua.
👆👉Nashauri kama itakua lazima sana basi randa zibadilishwe Mara 2 pekee IKIBIDI
👉👆👈 MASOKO
👉Broiler wamekua wakiuzwa sana , kwa mtu mmoja mmoja, familia, supermarket, wauzaji wa nyama mitaani, mahoteli, mashule na sehemu kadha wa kadha NASHAURI tafuta soko lako la uhakika na uwe tayali kulilinda bei za broiler zinatofautiana mkoa kwa mkoa.
👆👉👆 MFUMO WA UGUGAJI
👉Ili kuhakikisha soko lako linakua lakudumu na kuepuka kupoteza wateja nashauri
👆Kama una mtaji ya kuku 500, nivema ukaingiza kuku 250 wiki hili, kisha 250 baada ya wiki 2 hii itarahisisha mzunguko wa pesa ya mradi, USIFUGE Kuku 500 kisha ukakaanao siku 28-30 ukiuza ndo uweke wengine itakua ngumu sana kukuza mradi (kutokana na research ndogo niliyofanya pindi nawatembelea wafugaji ).
UFUGAJI WA KUKU BROILER
Makadirio ya gharama za ufugaji kwa vifaranga 100
Kwa kipindi cha siku kati ya 28-32…
Vifaranga 100 @ 190000-230000
Chakula starter 1@ 70000-71000
Grower 2 @68000-69000
Finisher 2@66000-67000
Chanjo
Newcastle 6000
Gumboro 6000
Newcastle/Gumboro 6000
Neoxychick 5000
Vitamins 30000
Maranda mifuko miwili 9000
Vyanzo vya joto 20000
Hizo ni garama za lazima kwa ufugaji wa broilers
Zinaweza kuongezeka gharama za dawa iwapo kuku wataugua , Gharama hizi zinatofautiana kutoka sehemu moja Hadi nyingine
Karibu
KAHISE POULTRY SOLUTIONS FAHARI YA MFUGAJI