Ufugaji Bora wa Ng’ombe wa Maziwa

UMUHIMU WA UFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA KWA BINADAMU

  • Huongeza kipato (Familia Vs Taifa).
  • Chanzo cha ajira.
  • Huboresha lishe kwa binadamu.
  • Huongeza upatikanaji wa mbolea (20kg/siku/ng’ombe).
  • Rafiki wa mazingira.
  • Huongeza fursa ya kupata mitaji.
  • Huboresha utumiaji sahihi wa taka zisizofaa mfano mashudu ya alizeti.

 

AINA ZA NG’OMBE WA MAZIWA

Kuna aina nyingi za ng’ombe wa maziwa ambao hutofautishwa kwa sifa zifuatazo;

  • Umbo, mahali alipotokea.
  • Rangi ya ngozi
  • Uzalishaji wa maziwa nk.

Zaidi kabisa kuna aina kuu mbili ambazo ni; “Bos taurus” na “Bos indicus”.

  • Bos taurus inahusisha: Friesian, Ayrshire, Brown Swiss, Guernsey and Jersey na wengine wengi kama vile (Red Dane, Swedish Red and White, Holstein Friesian nk.)
  • Bos indicus inahusisha: Sahiwal, Red Sindhi, Kenana, Criolo, Tharpakar nk.

 

FRIESIAN/FRESHIANI

  • Asilia yao ni holand.
  • Hutambuliwa kwa kuwa na rangi nyeupe na nyeusi.
  • Uzalishaji bora wa maziwa (7800l/mwaka).

Walikuwa maalum kwa ajili ya kutengenezea “cheese”.

AYRSHIRES

  • Wanatambuliwa kwa kuwa ana rangi nyekundu na nyeupe.
  • Wanatoa maziwa yenye wastani wa fati 4%.
  • Huzalisha maziwa yenye fati nyingi (5400l/mwaka).

JERSEYS

  • Asili yao ni visiwa vya jersey katikati ya Uingereza na Ufaransa.
  • Wanatambuliwa kwa kuwa na rangi mtambuka wa nyeusi na kahawia. Maziwa 5700l/mwaka.
  • Maalum kwa ajili ya utengenezaji wa “butter”.
Mtamba wa Jersey

UTUNZAJI WA MTAMBA KATIKA SHAMBA

Kila mwaka ng’ombe wengi wa maziwa wanaondolewa katika shamba kwa sababu mbalimbali kama ifuatavyo;

  • Uzalishaji mdogo wa maziwa
  • Magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambikiza (TB).
  • Matatizo ya uzazi
  • Kuuzwa au kuchinjwa tu bila sababu maalum.

 

UNUNUZI WA HEIFER/MTAMBA

Siku zote hatushauri mfugaji atafute mtamba mbadala kwa sababu zifuatazo;

  • Hawapatikani kwa urahisi na kama wakipatikana ni ghali sana.
  • Hatari ya kuingiza magonjwa shambani kwako.
  • Ugumu wa kufuatilia historia ya wazazi.
  • Hakuna mfugaji anaeweza kuuza mtamba wake bora.

 

HATUA ZA AWALI ZA ULEAJI WA NG’OMBE MWENYE MIMBA

Ukuaji wa ndama bora huanzia pale anapokuwa ndani ya mfuko wa uzazi wa mama yake mpaka atakapokamilisha miezi tisa 9 au siku 280 ± 5.

Hivyo ili kupata ndama bora ni lazima apate chakula bora chenye mchanganyiko sawia ili kufikia mahitaji yake ya virutubisho. Pia ni vizuri kuwapa chakula cha ziada wakati wa msimu wa ukame.

 

Aina ya virutubisho Kiasi katika asilimia
Wanga 70%
Protini 25%
madini 4%
Vitamini 1%

Hivyo ulishaji wa chakula bora katika kipindi hiki una faida zifuatazo;

  • Huchochea ukuaji wa ndama akiwa tumboni kwa mama.
  • Huchochea ndama kuzaliwa na uzito unaofaa.
  • Uhakika wa kupata ndama akiwa hai baada ya kuzaliwa.

 

MADHARA YANAYOWEZA KUTOKANA NA UZITO MDOGO WAKATI WA KUZALIWA

  • Ndama kuwa dhaifu
  • Uwezo mdogo wa kujikinga na magonjwa na anaweza kufa kirahisi baada tu ya kuzaliwa.

NB; Uzito mkubwa wakati wa kuzaliwa unaweza kusababisha matatizo wakati wa kuzaa (Dystocia).

Pia unatakiwa kusimamisha ukamuaji wa maziwa miezi miwili kabla ya kuzaa ili kumfanya ng’ombe apumzike.

 

Pia unashauriwa mfugaji kumpa ng’ombe mwenye mimba chakula bora atakapo bakiza wiki 6-8 kabla ya kujifungua (steaming up) kwa ajili ya kuboresha yafuatayo;

  • Kumuandaa ng’ombe kutoa maziwa ya kutosha baada tu ya kuzaa.
  • Kuchochea utengenezaji wa maziwa kwa wingi.
  • Humsaidia ng’ombe kutunza virutubisho mwilini kwa ajili ya matumizi ya baadae.

NB; Usifanye “Steaming up” ndani ya banda la kukamulia.

 

SIFA YA SEHEMU SAHIHI YA KUZALIA

  • Inatakiwa kuwa safi na imesafishwa kwa kutumia madawa yanayoweza kuondoa vijidudu ndani ya banda.
  • Matandiko yanatakiwa kuwa safi na makavu.
  • Hakikisha sakafu inakuwa na mfumo mzuri wa mifereji kwa ajili ya kuruhusu maji na mkojo kupita.
  • Vihondi vya maji na chakula.

NB; Tumia kalenda ya uzalishaji.

 

DALILI ZA NG’OMBE KUTAKA KUZAA

  • Kukua kwa kiwele ikiashiria kuanza kutengenezwa kwa maziwa.
  • Ng’ombe kuwa katika hali isiyo ya kawaida kama vile kulala chini mara kwa mara, na kusimama.
  • Kutembea kwa shida na pande zote za tumbo kutanukaa.
  • Vulva kuwa kubwa na kutoa majimaji.
  • Kutoka kwa mfuko wa majimaji muda mfupi kabla ya kuzaa.

 

WAKATI WA KUZAA
– Wakati wa ng’ombe kuzaa mwache ng’ombe akamilishe zoezi lake la kuzaa mwenyewe, kama hataonyesha dalili za kushindwa kujifungua msaidie ng’ombe.

MARA BAADA YA KUZAA
Mara baada ya ng’ombe kuzaa zingatia vitu vifuatavyo.
– Mara baada ya kuzaa mtazimie hali ya ng’ombe kama kuna hali ya tofauti kwa ng’ombe.
– Mwache ng’ombe amrambe mtoto wake, kwa ng’ombe kuramba mtoto wake husaidia kumpa nguvu ndama.
Pia kwa msaidizi (mfugaji mwenyewe anaweza kufanya kazi hiyo ya kumsafisha ndama).

– Mwache ndama akae na mamaye kwa muda wa siku tatu (3 au 4), Baada ya hapo unaweza kumtenga kutoka kwa mama.
– Hakikisha ndama anapata maziwa ya kwanza kutoka kwa mama yake dang’a (colostrum).

Maziwa haya husaidia sana kumwongezea kinga ya mwili kwa ndama.
Pia husaidia kufungua mfumo wa chakula kwa ng’ombe.
Maziwa haya yana virutubisho muhimu sana kwa ukuaji wa ndama.

Mara baada a kuzaliwa ndama apakwe dawa ya TINCTURE OF IODINE katika eneo la kitovu hili kuzuia wadudu wa maambukizi kupitia kitovu.
Endapo ndama hatashidwa kunyonya mkamulie na umpatie.

NB; Hakikisha unatunza taarifa za ndama aliyezaliwa baada ya wiki moja kama vile jinsia, tarehe ya kuzaliwa, uzito nk.

 

MFUMO YA ULEAJI WA NDAMA

Kuna mifumo miwili ya uleaji wa ndama kama ifuatavyo;

  1. Mfumo asilia
  2. Mfumo wa kisasa.

 

MFUMO ASILIA

Humwezesha ndama kutembea na mama muda wote na hivyo humpa ndama nafasi ya kupata kunyonya muda wote kwa mama.

MFUMO WA KISASA

Mfugaji anakamua baadhi ya Chuchu na kuacha zingine kwa ajili ya maziwa ya ndama.

HATUA ZA UKUZAJI WA NDAMA

  • Mlishe ndama mara 2 kwa siku au zaidi
  • Vyombo vya chakula viwe vimetengenezwa kwa aluminiamu.
  • Weka ndama mmoja kwenye chumba kimoja.
  • Safisha banda la ndama kila siku au baada ya siku moja.

 

KUKOMA KUNYONYA KWA NDAMA

Inahusisha kumtenganisha ndama na mama yake ili asinyonye tena (Miezi 2-3).

 

WAKATI SAHIHI WA KUFANYA;

  • Inategemea na utamaduni wa shamba.
  • Uzito na hali ya kiafya ya ndama.
  • Hali ya uchumi ya mfugaji.
  • Aina ya ulishaji.
  • Aina ya breed.

 

UZITO UNAOTAKIWA KATIKA UPANDISHAJI WA NG’OMBE

Mbegu kubwa (Friesian, Brown Swiss and Friesian). Pandisha wakiwa na uzito wa 300-350 kg katika umri wa miezi 14-16.

Mbegu ndogo (Ayrshire, Sahiwal, Jersey). Pandisha wakiwa na uzito wa 230-275 kg katika umri wa miezi 13-15.

 

Imeandaliwa na International Tanfeeds limited

Leave a Reply