Site icon Ufugaji Bora

Vyakula vya Nguruwe na Ulishaji

Vyakula vya nguruwe na ulishaji

Nguruwe

A. Utangulizi

Chakula bora kwa nguruwe ni moja ya swala muhimu sana kwenye dhana nzima ya ufugaji wa nguruwe wenye tija na faida kwa mfugaji. Chakula cha nguruwe kinagarimu yapata asilimia sabini ya garama zote za ufugaji wa nguruwe. Kati ya matatizo mengi yanayosababisha tija na ufanisi duni wa uzalishaji wa nguruwe yanatokana na lishe duni. Lakini kama nguruwe wakipatiwa lishe bora, tija na ufanisi wa uzalishaji utakuwa mkubwa hivyo kuongeza faida kwa mfugaji.

 

B. Baadhi ya faida za kulisha lishe bora kwa nguruwe

 1. Lishe bora huharakisha ukuaji wa haraka wa nguruwe nahivyo kupata uzito unaohitajika kwa kipindi kifupi.
 2. Lishe bora hupunguza gharama za ufugaji na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji kwa sababu nguruwe atahitaji kiasi kidogo tu cha chakula na atachukua muda mfupi kupata uzito mkubwa
 3. Lishe bora itapunguza maambukizi ya magonjwa.
 4. Lishe bora huongeza kiasi cha mayai yatakayoivishwa na mama nguruwe na hivyo kuongeza idadi ya watoto watakaozaliwa

5.    Lishe bora huongeza kiasi cha maziwa yatakayotengenezwa na mama nguruwe kwa ajili ya watoto hivyo kuwafanya wawe na afya bora itakayo wawezesha wakue haraka na kupunguza idadi ya vifo kwa watoto.

6.    Lishe bora inaongeza ufanisi wa madume ya nguruwe na hivyo kuongeza uwezo wa kupanda

 

C.  Viini lishe muhimu kwenye lishe ya nguruwe

Nguruwe wanauwezo wa kula aina nyingi za vyakula lakini vyenye uwezo wa kumeng’enywa kwa urahisi. Chakula cha nguruwe kilichokamilika kinahitaji kuwa na mchanganyiko wa viini lishe vitano, navyo ni

 

 1. Vyakula vyenye kutia nguvu mwilini (vyakula vyenye asili ya wanga) k.m

 

 1. Vyakula vya kujenga mwili (Vyakula vyenye asili ya protini) k.m

 

 1. Vyakula vya asili ya madini

 

 1. Vyakula vya asili ya vitamini k.m

 

5*. Maji

D.        Jinsi ya kutengeneza chakula cha nguruwe

Wakati wa kutengeneza chakula cha nguruwe inabidi kuzingatia yafuatayo:

 

Mfano jedwali Na 1 linaonyesha michanganyiko mbalimbali ya vyakula vya nguruwe.

 1. Mchanganyiko namba 1: inapendekezwa kwa wafugaji  walioko kwenye mazingira ambayo pumba za mahindi na mashudu ya alizeti yanapatikana kwa urahisi
 2. Mchanganyiko namba 2: kwa wale ambao pumba za mahindi, za mpunga  machicha ya pombe  na mashudu ya alizeti yanapatikana kwa urahisi.
 3. Mchanganyiko namba 3: kwa wale ambao pumba  za mpunga    na mahindi yanapatikana kwa urahisi.

 

 

Jedwali namba 1: Michanganyiko mbalimbali ya vyakula vya nguruwe

Na

Aina ya viinilishe

Michanganyiko

Namba 1

Namba 2

Namba 4

1

Vyakula vya wanga

1. Pumba za mahindi

70.25

32

30.00

2. Pumba laini za mpunga

25

33.00

3.  Machicha ya pombe

     yaliyokaushwa

21

4. Mahindi yaliyobarazwa

10.00

2

Vyakula vya protini

A. Protini ya nafaka

1. Mashudu ya alizeti

22.00

14

22.00

2.Mashudu ya michikichi

3. Soya iliyochemswa na kubarazwa

B. Protini ya Wanyama

4.Unga wa dagaa/samaki

4.00

2.00

3.25

5.Damu iliyokaushwa

2.25

3

Vyakula viasili vya madini

1. Chumvi ya mezani

0.50

0.50

0.50

2. Chokaa ya mifugo

2.00

2.00

2.00

3.  Unga  wa mifupa

1.00

1.00

1.00

4. Madini na vitamini

    mchanganyiko

0.25

0.25

0.25

         Jumla

100.

100

100.

 

 

E.     Kiasi na namna ya kulisha

 

Jedwali na 2:  Viwango vya kulisha nguruwe wa uzito mbalimbali

Na Wakati Uzito wa nguruwe (kilo) kiasi cha chakula  (kilo kwa siku)
1. Baada ya kuachishwa kunyonya hadi uzito kiasi 10 – 17 0.75
2. Uzito uliozidi kiasi kidogo 18 – 29 1.00
3. Uzito wa kawaida 30 – 40 1.50
4. Uzito mkubwa kiasi 41 – 60 2.00
5. Uzito mkubwa 61 – 80 2.5
6. Uzito mkubwa sana 81 – 100 3.00

 

 

Jinsi ya kulisha makundi mbalimbali ya nguruwe

 

 1. Kipindi cha mamba, kuzaa hadi kuachisha kunyoyesha

 

1.1 Kipindi cha miezi mitatu baada ya kupandishwa

 

1.2 Wiki tatu kabla ya kuzaa

 

1.3 Wiki moja kabla ya kuzaa

 

1.4 Siku ya kuzaa

 

1.5 Siku ya 1 – 2 baada ya kuzaa

 

1.6 Siku ya 3 na kuendelea

Zingatia
Mfano: kama mama ana watoto 9 atahitaji kiasi gani cha chakula?
Mahitaji mama peke yake Mahitaji kutokana na watoto Kiasi cha chakula kwa siku
3kg Theluthi moja x 9 Kilo 6 kwa siku

3     +         (1/3   x  9)       =      6 Kg

 

Baada ya kuachisha kunyonya

Chakula kwa ajili ya watoto wa nguruwe (Creep feed)

 

Aina ya  viinilishe Asilimia
 

Mahindi yaliyobarazwa

 

30

Pumba za mahindi 40
Mashudu ya alizeti 18
Unga wa Dagaa 10
Unga  wa mifupa 0.5
Chokaa ya mifugo (limestone) 0.75
Chumvi ya mezani 0.5
Premix 0.25
Jumla 100
Exit mobile version