Iili kufanikiwa kufikia malengo ya kufuga kuku wa mayai ni vyema mfugaji akapata wasaa wa kujiuliza maswali kadhaa ili awe na dira sahihi ya kile anachotarajia kufanya kutokana na mapato ya mradi huo.
Dira ni picha ya matokeo yanayotarajiwa yanayotokana na juhudi na maarifa .
Bila shaka kabla ya kuanza kufuga utakuwa umejiuliza ni kwa nini ufuge kuku wa mayai na wala sio kufanya kitu kingine ; swali kama hili litakusaidia kuwa na muelekeo wa kile unachotarajia na hivyo kuweka mkakati sahihi wa kusimamia mradi wako wa kuku wa mayai.Mfano , pengine umeamua kufuga kuku kwasababu kuna upatikanaji wa pembejeo kwa urahisi kama vile upatikanaji wa vifaranga, viinilishe, madawa na kubwa zaidi ni upatikanaji wa soko la mazao yako.
Vyovyote iwavyo mambo yafuatayo ni vizuri yakazingatiwa ili kupata mafanikio katika mradi wa kufuga kuku wa mayai;
- Uwe na uhakika wa kupata vifaranga kutoka kwa wasambazaji mahiri ( reliable Day old Chicks breeders and Suppliers)
- Zingatia ratiba ya kulisha. Lisha kuku chakula kinachopendekezwa kwa kuzingatia umri na uzito.
- kagua na na fanya usafi mara kwa mara na katika nyakati zilizopangwa(inspect and carry out specificl and periodical hygienic operations)
- toa matunzo kwa kwa kuzingatia mahitaji ya makundi.
- Tengeza viota ili kuku waweze kutaga mayai kwa faragha bila bughudha kutoka kwa wengine. Vilevile viota husaidia kuwa na mayai safi na husaidia kuepuka kuvunja kuvunjika na kuchafuka kwa mayai mara kwa mara.
- Hakikisha unasafisha mayai kwa kitambaa safi baada ya kuokota na kabla kuwauzia wateja.
- Zingatia matakwa ya wateja kwa kuainisha mayai katika makundi kama ifuatavyo;
- Rangi ya mayai
- Rangi ya kiini cha yai(egg yolk colour), wengi wanapenda kiini cha rangi ya njano.
- Ukubwa wa mayai
- Aina ya mayai( mayai ya kienyeji yanapendwa zaidi kuliko ya kisasa)
- Fanya ukaguzi wa afya za kuku na kuwa tibu kila mara. Utaratibu unaopendekezwa ni kukagua afya asubuhi unapoamka na usiku unapoenda kulala. Angalia vinyeo ili kuona wanakunya kinyesi cha rangi gani(kinyesi ni kielelezo muhimu katika kutambua ugonjwa).
- Chunguza tabia za kuku ili kuona kama wanakula mayai au la . Ukiona kuku wameanza kula mayai fanya zoezi la kukata midomo mara moja kazi hufanywa na wataalamu , kwahiyo unashauriwa kumuona mtaalmu aliye jirani.
- Tunza kumbukumbu zote mradi ili zikusaidie kufanya tathmini ya mradi unaoendesha.
CHANZO: MAJUMBENI