Elimu ya ufugaji bora wa samaki

1.Mambo yakuzingatia wakati wakuchagua eneo kwaajili ya ufugaji samaki.

 1. Aina ya udogo: hili nijambo muhimu kwani aina ya udogo huathiri kwenye kuchagua aina gani ya bwawa litumike. Tambua kuwa kuna aina nyingi ya mabwawa kama bwawa la udogo tupu (earthen pond) na bwawa la zege (concrete pond). Bwawa la zege hutumia gharama nyingi kulijenga ukilinganisha na bwawa la udogo tu. Hivyo ili bwawa liwe la udogo ni lazima aina ya udogo wa eneo husika uwe na sifa ya kutunza maji.
 2. Maji: samaki huishi kwenye maji hivyo nilazima uwahakikishie upatikanaji wa maji safi na salama kwa uhai wao. Maji yawe yanapatika kwa Wingi, Salama na yenye kuweza kuwekwa katika miundombinu sahihi kwaajili ya kutumika wakati wowote. Maji yanaweza kuwa ya kisima, mto, ziwa, chemchem,au bomba. Kila aina ya maji ina faida zake na changamoto zake. Kwa mfano wakati maji ya mto huwa yanaweza kupatikana kwa urahisi lakin yanachangamoto yakuweza kukuletea vijidudu vya magonjwa kama minyoo, typhoid na kipindupindu.

III. Vifaranga: usishangae! Ndiyo mbegu za samaki yaani samaki wadogo huitwa vifaranga. Nilazima ujihakikishie upatikanaji wa mbegu bora kwaajili ya matokeo mazuri. Mbegu duni huchukua muda mwingi kukuwa na hivyo kumuongezea mkulima gharama za ufugaji na kumpunguzia kipato.

 1. Chakula: ufugaji wa samaki kwaajili ya biashara humuitaji mkulima kuwapatia samaki chakula za ziada (supplementary feed) ili samaki wakue kwa haraka zaidi. Kumbuka ukuwaji wa samaki hutegemea UBORA WA MAJI + UBORA WA CHAKULA.
 2. Ulinzi na usalama: ni vyema mkulima kuepukana na migogoro yeyote kama ya umiliki wa ardhi na matumizi ya maji ili kuondoa uwezekano kukuhujimiwa katika mradi wake.
 3. Usafiri: kwa nyakati tofauti mkulima atahitajika kusafirisha ima malighafi zitumikazo kwenye ufugaji au mazao ya ufugaji baada ya kuvuna. Hivyo ni muhimu kuzingatia uwezekano wa usafiri sahihi wakati wote. Usafiri siyo mtu awe na gari hapana ila uwepo wa miundombinu safi yaweza tosha.

VII.Soko: Mwisho wa ufugaji ni kuuza mazao yako kwa faida hivyo ni vyema mkulima akafanya tafiti za kupata soko la uhakika kwa mazao yake. Mkulima huweza tumia soko la karibu kama majirani na wafanyabiashara wa karibu. Pia anaweza kutumia soko la mbali.

 

Ufugaji wa samaki unalipa endapo tu mkulima atapata mtaalamu sahihi na akazingatia kanuni za ufugaji.

 1. KWANINI NIFUGE SAMAKI WAKATI KUKU WA KISASA WANACHUKUA MUDA MFUPI ZAIDI NA WANALIPA?

Ni kweli kama tutalinganisha ufugaji wa kuku wa kisasa na ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku wa kisasa unalipa zaidi kwakuzingatia kuku wa kisasa wanachukua takriban wiki 6 mpaka kuingia sokoni ukilinganisha na samaki ambao wanatumia takriban miezi 6.

Ila ulinganishi huu hatokuwa sahihi sana kwasababu zifuatazo

 1. Kuku wa “kisasa” ni Genetically Modified Organisms (G.M.O) yaani viumbe ambao mpangilio wao wa asili wa vinasaba (genes) umebadilishwa kulingana na mahitajio mahususi. Viumbe hawa (GMO) huwa na sifa nying nzuri kama kukua haraka, ustaamili mazingira magumu zaidi kuliko asili yao na mengne. Lakin pia huweza kuwa na changamoto mbali mbali kama kushambuliwa na magonjwa kwa urahisi kama ilivyo kwa kuku wa kisasa ambao huhitaji mfuatano wa dawa kibao ili kuwawezesha kuishi. Madawa ambayo mengine yanamadhara makubwa kwa mraji wa kuku. Tukirudi katika mazingira ya kawaida natumai wengi tunajua kuwa kuku wa kienyeji anahitaji takriban miezi 7 mpaka aweze kuliwa. Kinyume na hivyo samaki wanaofugwa na wafugaji wa kitanzania ni samaki wa asili yaani siyo GMO hvyo hawasumburiwi na changamoto kama za GMO wa kuku.
 2. Soko la walaji kwasasa linapendelea chakula safi na salama chakula ambacho ukila hauhitaji kutumia madawa bali chenyewe ni chakula na pia ni tiba. Jambo hili linalazimisha walaji kuogopa kutumia GMO kama kitoweo. Jambo hili linafanya ufugaji wa samaki uwe na soko lisilo na matabaka ukilinganisha na ufugaji wa kuku wa kisasa.

III. Katika gharama za ufugaji samaki wanauwezo mkubwa sana wakukibadilisha chakula duni kuwa virutubisho vya mwili wao. Jambo hili kitaalamu linajulikana kama FOOD CONVENTION RATIO (FCR) ambayo nikipimo cha kiasi cha chakula alichokula kiumbe ukilinganisha na ukuwaji (irreversible increase in body weight and size) ambao hupimwa kwa urefu na/au uzito. Baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa samaki ana FCR ya 1:1 na kuku ana FCR ya 2.5:1 yaani samaki anauwezo wakula kilo 1 ya chakula na kuongezeka kilo 1 ya uzito (ukuwaji) na kuku anahitaji kilo 2na nusu za chakula ili aongezeke kilo 1ya uzito (ukuwaji). Hvyo mfugaji wa samaki atatumia chakula kidogo zaidi kumnenepesha samaki ukilinganisha na mfugaji wa kuku. Jambo hili huleta athari kwenye biashara ya kuku kwa kufanya uwiano wa faida na gharama za ufugaji kuwa chini ukikinganisha na biashara ya samaki. Kwa mfano mfugaji kuku anaweza fuga kuku kwa wiki sita akatumia 1,500,000  kuwakiza na baada ya mauzo akapata 4,320,000. Faida ni  2,820,000 Uwiano. Wakati huo mfugaji wa samaki anaweza tumia 750,000 kukuzia samaki na akawauza kwa 3,790,000. Faida ikawa 3,040,000.

Ukilinganisha mradi upi umerejesha uwiano mkubwa wa faida utakuta ufugaji samaki unalipa zaidi.

 

Sababu ni nyingi lakn mwisho wa siku mfanyabiashara huchagua biashara ambayo anaona anaweza imudu na itamletea faida zaidi.

 

 1. JE UMRI WA VIFARANGA (MBEGU ZA SAMAKI) UNAMCHANGO WOWOTE KWENYE MATOKEO YA UFUGAJI WA SAMAKI WAKO?

 

Vifaranga vya samaki vimegawanyika katika aina kuu mbili kulingana na hatua ya makuzi. Hatua ya mwanzo tu wakizaliwa kitaalamu huitwa “fry” na hatua ya pili huitwa “fingerlings”.

FRY ni vifaranga wadogo mno na wanakuwa na umri wa kati ya wiki 1mpaka wiki 4. Na wanakuwa na uzito wa chini ya 5gram.

FINGERLINGS ni vifaranga wakubwa na wanakuwa na umri wa kati ya wiki 4 na wiki 8. Na wanakuwa na uzito wa kati ya 5gram na 15gram.

 

JE KUNA FAIDA IPI YA KUNUNUA FRY AU FINGERLINGS?

 

Vifaranga vya FRY nirahisi sana kushambuliwa na kiumbe yeyote mualibifu kama ataingia kwenye bwawa kwa mfano chura. Pia nirahisi kudhurika kama litatokea tatizo lolote wakati wa kuwa safirisha. Faida yake kubwa huwa wana matumizi madogo ya oxygen wakati wakusafirishwa na huwa hawatoi taka nyingi (excretory wastes).

 

Kwa upande mwingine vifaranga vya hatua ya FINGERLINGS huwa na uwezo mkubwa wa kujilinda na kumudu changamoto za kimazingira japokuwa wanamatumizi makubwa ya oxygen na hutoa takanyingi ukilinganisha na vifaranga vya hatua ya FRY.

 

Mfugaji atakayenunua vifaranga vya hatua ya FINGERLINGS atapata faida ya mwezi mmoja wa ziada ambao vifaranga vilikuwa vimelelewa kabla ya kuwanunua. Hivyo kama atawafuga kwa miezi sita vifaranga wake watakuwa na ziada ya mwezi mmoja ambao huchangia katika ukubwa wa samaki. Kwani samaki wa miezi sita na miezi saba hutofautiana katika uzito. Hivyo kumfanya mfugaji auze kwa bei nzuri na kupata faida kubwa.

 

Kwahyo jibu ni NDYO umri wa vifaranga unachangia katika kukupa matokeo mazuri ya ufugaji.

 

 

 1. JE SAMAKI WANAUGUA MAGONJWA? NA NINI TIBA YAKE?

 

Naam! Samaki huugua magonjwa mbali mbali kama minyoo, fungus na kupatwa na chawa. Pia samaki wanaweza kubebe vimelea vya magonjwa kama typhoid na kipindupindu.

Ila tutazame magonjwa ya samaki katika namna ya chanzo cha ugonjwa. Kuna magonjwa ambayo yanatokana na chanzo maalum “point-source diseases” na kuna magonjwa ambayo hayana chanzo maalum “non-point-source diseases”.

Magonjwa yenye chanzo maalum mara nyingi husababishwa na maji hususani maji ya mito. Kundi hili hujumuisha magonjwa kama minyoo, chawa, typhoid na kipindupindu.

MINYOO- Humuathiri samaki katika ukuwaji wake lakin sirahisi kwa mkulima kujua kama samaki wake wanaminyoo. Minyoo hujakubainika pindi samaki wanapokuwa wameshakomaa na umewavuna. Wakati wakuwaandaa samaki ndipo unapokuta minyoo mingi tumboni! Hii hali ikijitokeza lazima ukuondolee soko la samaki wako kwakiasi kikubwa. Kwani samaki mwenye minyoo licha yakuleta picha mbaya lakin asipo pikwa vizuri minyoo huweza kuhamia kwa mlaji.

CHAWA- Athari ya chawa kwenye bwawa mara nyingi huonekana kwa samaki wakubwa lakini inadhuru samaki wote. Ikitokea samaki wamekubwa na chawa utawaona wanarukaruka kwenye maji na kujipiga piga mpaka kufa kutokana na majeraha na kuchoka.

TYPHOID na KIPINDUPINDU- Haya humuathiri mlaji wa samaki kama samaki hawataandaliwa vizuri. Na madhara yake yanafahamika kwa binadamu inakuwaje mtu akipatwa na kipindu pindu au typhoid.

CHANZO CHA MAGONJWA HAYA HUWA NI KINYESI CHA MWANADAMU AMBACHO HUSABABISHWA NA WATU KUJISAIDI KWENYE VYANZO VYA MAJI. WAKATI MWINGINE HUSABABISHWA NA KINYESI CHA KUKU AU NG’OMBE KAMA MIFUGO HIYO ILIKUWA IMEATHIRIWA NA MAGONJWA HAYO.

 

Magonjwa yasiyo na chanzo maalum ni kama Fungus.

FUNGUS ni saprophytic feeders yaani wanakila vitu vilivyokifa au oza. Kwahyo ikitokea kwenye bwawa kuna mazingira yakuruhusu waokustawi basi humshambulia samaki na maranyingi samaki huyu huwa na vidonda au majera yanayoonekana kwenye kiwiliwili cha samaki. Na jambo hili huondoa mvuto wa samaki kwa mteja.

 

Orodha ya magonjwa kwakusema tujifunze tu ni ndefu mno LAKINI NI MARA CHACHE SANA KUKUTA SAMAKI KAUGUA YEYOTE KATI YA MAGONJWA HAYA KWA MKULIMA ALIYEPATA USHAURI SAHIHI NA AKAZINGATIA TARATIBU.

 

TIBA za magonjwa zipo za aina nyingi lakin inashauriwa kwa mfugaji kuchukua tahadhari wakati wa mwanzo wa mradi na wakati wautekelezaji ikikuepukana na mlipuko wa magonjwa katika bwawa kwani ugonjwa ukishaingia kwenye bwawa inahitaji umakini wa hali ya juu ili kuuondoa kabisa.

 

 

 1. JE NAWEZAJE KUJUA IDADI YA SAMAKI WAKUWEKA KWENYE BWAWA LANGU?

 

Ni muhimu sana kwa mfugaji samaki kuweza kujua idadi sahihi ya vifaranga ambavyo anaweza kuweka kwenye bwawa lake kwaajili ya kupata matokeo mazuri kabisa kwenye bwawa lake (optimization of the pond productivity). Japokuwa kumekuwa na nadhari mbalimbali zinazoelezea idadi ya vifaranga vya kuweza kuwekwa kwenye bwawa (stocking density) nitajaribu kuelezea namna moja wapo ambayo nimeiona kuwa inafaa.

 

Kwanza tutambue mambo ambayo yanayokupelekea kwa mabwawa mawili yenye ukubwa sawa kutofautiana idadi ya vifaranga. Ndiyo, mabwawa yenye ukubwa sawa yanaweza kutofautiana idadi ya vifaranga. SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA KUTOFAUTIANA KWA IDADI YA VIFARANGA NI KAMA ZIFUATAVYO:

 

 1. Aina ya mfumo wa ufugaji.

 

Katika ufugaji samaki kuna

 1. A) Ufugaji wa samaki peke yake bila kuchanganya na shughuli nyingine kama ufugaji wa kuku au ng’ombe na ufugaji wa samaki wenye kuchanganya na shughuli nyingine kama ufugaji wa kuku au ng’ombe katika eneo moja.

 

Tafiti zimeonesha kwamba ufugaji wa samaki ukichanganywa na ufugaji labda wa kuku ambapo kinyesi cha kuku kinatumika kuongeza uzalishaji wa chakula cha asili ndani ya bwawa la samaki kunapelekea kuweza kuongeza idadi ya samaki wanaoweza kufugwa katika bwawa ukilinganisha na ufugaji usiochanganya mifugo.

 

 1. B) Ufugaji wa samaki kulingana na malengo ya mfugaji yaani mfugaji amekusudia kufanya ufugaji wa biashara au wahali ya kawaida tu. Maamuzi haya yataathiri mtazamo na jitihada za mfugaji katika kuliendesha bwawa lake husisani katika suala zima la CHAKULA. Kwa ujumla hapa kuna namna tatu za ufigaji samaki nazo ni

 

*Ufugaji wa kawaida (subsistence farming or extensive farming)

Ufugaji huu unasifa kubwa moja nayo ni kuwaacha samaki wategemee CHAKULA CHA ASILI kwenye bwawa. Kutokana na upatikanaji wa chakula cha asili kuwa mgumu kwenye bwawa, aina hii ya ufugaji humuwezesha mfugaji kufuga samaki wachache sana kutoka na uhaba wa chakula na mara nyingi samaki huitaji muda mwingi kukua ndani ya bwawa.

Ufugaji huu unamruhusu mkulima kufuga samaki 3 KWA KILA MITA MOJA YA MRABA  au chini ya hapo kulingana na uwezo wa bwawa kutengeneza chakula cha asili. Pia ufugaji huu huwa hauna tija kubwa kwa mfugaji

 

*Ufugaji wa kiwango cha kati ( semi-extensive or semi-intensive farming )

Aina hii ya ufugaji ni ile ambayo mfugaji anajishughulisha kuwapatia samaki chakula cha ziada (supplementary feed). Kwahyo hapa samaki watakuwa wanakula chakula cha asili kinachozalishwa kwenye bwawa na chakula cha ziada anachowapa mfugaji hivyo kupelekea samaki kukua kwa haraka zaidi kuliko kasi ya ukuaji katika ufugaji wa kawaida. Ufugaji huu pelekea kuongezeka kwa uwezo wa bwawa wa kukuza vifaranga mpaka kufikia kati ya VIFARANGA 4-7 KWA KILA MITA MOJA YA MRABA ya bwawa. Ufugaji huu unakuwa na tija ya wastani kwa mfugaji.

 

*Ufugaji wa kiwango cha juu (intensive farming)

Ufugaji huu unasifa moja kuu ambayo utegemezi wa samaki wa mahitaji yao yote ya chakula kutoka kwa mfugaji. Aina hii ya ufugaji hutumia pesa nyingi sana kuwekeza ili kuleta faida kubwa zaidi (unmatched investment for unmatched production). Teknolojia inayo tumika hapa pia huwa ni kubwa sana. Samaki huwa wanalishwa chakula chenye virutubisho vingi zaidi ili kuwafanya wakue ndani ya muda mfupi zaidi.

Aina hii ya ufugaji inatija kubwa sana kwa mfugaji na humuwezesha mfugaji kuwa na uhakika wakusambaza samaki mwaka mzima. IDADI YA VIFARANGA HUZIDI 8 KWA KILA MITA MOJA YA MRABA.

 

 1. C) Ufugaji wa samaki wa aina moja (monoculture) na ufugaji wa samaki mchanganyiko (polyculture)

Ufugaji wa samaki aina ya Tilapia kama sato unachangamoto kubwa moja ya samaki kuzaliana kwa wingi kwenye bwawa hivyo kupelekea samaki kuzidi uwezo wa bwawa wa kukuza samaki hali hii hupelekea samaki kudumaa au kuchukua muda mwingi sana kukua kifikia kiwango cha sokoni (market size) kwahyo njia mbadala huwa kufanya ufugaji mchanganyiko ambapo tilapia na kambale huchanganywa kwenye bwawa moja.  Kwa kawaida bwawa huanza kwa kuwekwa tilapia kisha baada ya yakriban mwezi mmoja na nusu huongezewa vifa

 

anga vya kambare (catfish). Kutokana na tabia ya kambare yakula karibia kila kitu hapa tabia yake hutusaidia katika kula vifaranga vitakavyozaliwa hivyo kufanya idadi ya samaki ndani ya bwawa kunakia kwa wastani ile ile. Ikumbukwe kuwa idadi ya tilapia katika ufugaji huu huwa ni mara 3 ya idadi ya kambare yaani uwiano wa kambare na tilapia huwa 1:3 respectively.

 

 1. Jinsia ya samaki

Jambo jingin linaloweza kuathiri idadi ya vifaranga kwenye bwawa ni jinsia ya samaki wanaofugwa. Kwa kawaida ufugaji wa samaki mchanganyiko hupelekea samaki kuzaliana na kusababisha ushindani wa chakula. Hivyo basi ufugaji wa samaki madume tupu mara nyingi hupendelewa. Madume yanasifa yakukua haraka kuliko majike. Kutokana nakutokuwa na mazaliano samaki wa jinsia moja (mono-sex) huweza kukaa wengi zaidi kwenye bwawa moja kuliko kiwango cha samaki katika hali ya kawaida.

 

Pamoja na taarifa hizi bado ni muhimu kupata ushauri wakina kutoka kwa mtaalamu wako kabla hujaamua kujiingiza katika ufugaji wa samaki moja kwa moja.

 

 1. JE NAWEZA KUFUGA SAMAKI HUKU NIKIWAPA CHAKULA CHA KISASA KAMA CHAKULA CHA ZIADA NA BADO SAMAKI WAKASHINDWA KUFIKIA UKUBWA WAKULIDHISHA?

 

Kutokana na ufugaji wa samaki kuwa jambo geni katika jamii nyingi za kiafrika, sekta hiyo pia bado haijaendelea kufikia kiwango cha kulidhisha kama ilivyokatika ufugaji mwingine.  Swala la upatikanaji wa chakula bora kwa gharama nafuu bado ni changamoto! Na pale kinapopatikana basi huwa kinauzwa kwa gharama kubwa kutokana na uwepo wa watu wanaotumia mwanya huo kujipatia pesa “kiulaini “. Hili ni jambo ambalo linaweza kutatuliwa kiurahisi kama wafugaji wa samaki wataweza kuanzisha vyama vyao vya ushirika ili kuweza kuweka nguvu ya pamoja kwenye kutatua changamoto zinazo wakabili lasivyo tutaendelea kuwanufaisha wafanyabiashara wachache wanaotuuzia chakula kwa gharama isiyo linganishi!

 

Pamoja na changamoto hiyo lakini bado kumekuwa na tatizo kubwa la uzingatiaji wa kanuni za ulishaji samaki kwa kiwango sahihi kwenye mabwawa pale mtu anapoweza kumudu gharama hizo.

 

Kwa kawaida nimekuwa nikipata malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafugaji wakilalamika kuwa wameuziwa mbegu feki za samaki yaani hazikui kufikia kiwango cha hitajio la soko kwa muda husika. Baada yakuamua kulifuatilia suala hilo kwa kina ndipo nilipokuja kugundua kuwa wafugaji wengi hawazingatii taratibu za ulishaji. Wengiwao WANAWALISHA SAMAKI WAKUBWA CHAKULA CHA VIFARANGA (hivyo wanashindwa kunenepa). Na WANAOWAPA CHAKULA CHA KUNENEPESHEA HAWAWAPI KWA KIWANGO SAHIHI!!!! Unaweza kuta samaki badala yakupewa kilo sita za chakula kwa siku samaki wanapewa kilo moja mpaka moja na nusu. Sasa huyo samaki kama huko kushiba hashibi vipi atanenepa?

 

Kitaalamu samaki anatakiwa ale 10% ya uzito wake kwa siku. Na ndyo maana inashauriwa kuwapima samaki wako angalau baada ya miezi mitatu ili uje kama kiwango cha chakula unachowapa ni sahihi.

 

ILIKUWEZA KUJUA KIWANGO CHA CHAKULA CHAKUWALISHA SAMAKI FANYA IFUATAVYO:

 

Kwa bwawa lenye samaki 1000 na kila samaki baada ya miezi mitatu amefikia 120g

 

Samaki anakula 10% ya uzito wake kwahiyo kila samaki atakuwa anakula 12g.

 

Kwasamaki 1000= 12g*1000=12000g=12kg/siku

 

Mlo huo ili ulike vizuri inashauriwa uwalishe mara tatu kwa siku.

 

Pia unaweza kupunguza kiwango cha chakula cha kisasa kwa kuwalisha samaki mboga za majani kama spinach.

 

Usipozingatia lishe bora ya samaki hata mbegu iwenzuri namna gani huwezi kuza samaki ndani ya muda mfupi na wakafikia hitajio la soko.

 

 

 1. JE KUNA TOFAUTI GANI KATI YA UFUGAJI WA KAMBALE NA SATO (TILAPIA)?

 

Kabla hatujaangalia tofauti zilizopo kati ya ufugaji wa kambale na tilapia kwanza tujikumbushe sifa chache zinapaswa kuzingatia kabla hauja chagua aina ya samaki wakufuga. vifuatazo ni baadhi ya vigezo vyakuzingatia wakati wakuchagua aina ya samaki wakufugwa:

 

 1. Ukuwaji wa haraka

2.upatikanaji wa chakula bora

 1. Kuhimili magonjwa
 2. Mvuto wa samaki
 3. Utamu
 4. Kuwahi kukomaa
 5. Uwezo mkubwa wakuzaliana
 6. Uwezo wakustaamili aina nyingi za mazingira
 7. Urahisi wakuzalisha na kulea vifaranga
 8. Aisiwe na tabia ya kula aina nyingine na awe mpenzi wa kula chakula aina ya mimea
 9. Itajio kubwa la soko na
 10. Uwezo wakuishi na samaki aina nyingine.

 

Tunapoongelea tofauti kati ya ufugaji wa kambale na tilapia kwanza tuelewe samaki hawa wametofautiana kwenye sifa moja kubwa ambayo ni UWEZO WA TILAPIA KUZALIANA WENYEWE KWENYE  BILA MFUGAJI KUWAINGILIA KATI WAKATI KAMBALE HAWAWEZI KUZALIANA WENYEWE WAKIWA KWENYE BWAWA. Jambo hili huwafanya kambale wabakie kwa idadi ile ile kwenye bwawa ambayo utawaweka (kama hakuna atakae kufa ) tofauti na tilapia ambao wanaweza kuzaliana na kuwa wengi kwenye bwawa!

Kuto kuweza kuzaliana kwa kambale kwenye bwawa kunaweza kuwa ni changamoto kwa mfugaji kwani atalazimika kila mara kununua vifaranga wapya baada ya kuvuna na kama sehemu aliyopo kuna uhaba wa vifaranga ufugaji unaweza kuwa mgumu. Kwa upande mwingine kutokuzaliana kwa kambale kwenye bwawa kuna wafanya wawetumia chakula chao karibia chote kwenye kujenga mwili hivyo kuwafanya wawe na uwezo wa kukuwa haraka mno kuliko tilapia ambao chakula hugawanywa kwaajili ya kuzaliana na kujenga mwili.

 

Tofauti nyingine kubwa kati ya kambale na tilapia ipo kwenye maumbile hususani mfumo wa upumuaji. Ukiangalia matamvua ya kambale utaona yapo kama maua fulani hivi tofauti na matamvua ya tilapia. Hali hiyo humfanya kambale aweze kuvuta hewa kavu na hewa ya kwenye maji. Na ndyo maana kambale anaweza kukaa nchikavu ukiwa umemvua hata masaa kumi na mbili inategemea na ukubwa wake. Pia jambo hili huwawezesha kambale kujichimbia chini kipindi cha kiangazi huku wakisubiria msimu mwingine wa mvua. Sifa hii yakimaumbile huwawezesha kambale kuvumilia mazingira magumu zaidi kuliko tilapia hivyo kumuwezesha mfugaji kuweza kuweka kambale wengi zaidi kwenye bwawa kuliko tilapia.

 

 

Tukiangalia kwa ujumla vigezo vyakuchagua samaki tunakuta kambale anachangamoto yakutokuwa na mvuto wa kimuonekano kwa walaji wengi hivyo kupelekea kufugwa na watu wachache kulingana na eneo na kutokuwa na soko kubwa kama tilapia.  pia kambale wanatabia ya kula samaki wengine kama tilapia hivyo mfugaji inabidi awe makini sana kama atakusudia kuwa changanya samaki hawa kwenye bwawa moja.

 

kwa ufupi hizo ni tofauti chache zilizopo kati ya samaki aina ya kambale na samaki aina ya tilapia (sato)

 

 

 1. JE NAWEZA KUKADIRIA KIWANGO CHA CHAKULA KINACHOWEZA KUTUMIKA KATIKA MSIMU MZIMA WA UFUGAJI SAMAKI?

 

Tafiti zinaonesha kuwa takriban ya 60% ya gharama zinazotumika kufugia samaki kwa msimu mmoja zinatokana na chakula. Hivyo dhana yakuweza kupunguza gharama za chakula kwa msimu ni muhimu zaidi katika kumuwezesha mfugaji kupata faida kubwa zaidi. Kumbuka gharama uliyoiokoa kwenye matumizi huongeza faida/ kipato kwenye biashara yako.

Kuna njia nyingi zinaweza kutumika katika kukadiria kiasi cha chakula ila katika darasa la leo naomba tuiangalie njia moja ambayo ni yakukadiria kiwango cha chakula kwa kutumia uwezo wa samaki wa kumeng’enya chakula ulichowapa na kuchangia katika ukuwaji wa samaki (Feed conversion ratio-FCR).

 

Kwa wastani samaki anauwezo wa kula kilo 1.2-1.8 na yeye kuongezeka uzito wa kilo moja. Kwa maana nyingine samaki anahizaji kula kilo 1.2-1.8 za chakula ili kumuwezesha kuongezeka uzito wa 1kg. Kwahiyo kama mfugaji atakusudia kumfuga samaki kwa miezi mitano na kumuuza akiwa na uzito wa robo kilo (250gram) inamaana atatumia kati ya gramu  300-450 za chakula kwa samaki mmoja. Kwa bwawa la samaki lenye samaki 1000 inamaana atavuna kilo 250 Za samaki na  atatumia kilo 300-450 Za chakula kwa kukuzia samaki hao.

 

Changamoto iliyopo wafugaji wengi wanafuga samaki kiholela yaani hawazingatii mahitajio halisi ya samaki katika kumkuza ili akupe faida. Changamoto ya pili wafugaji wengi wamekariri kuwa chakula cha samaki mpaka akanunue sehemu fulani ndyo anaamini samaki watakuwa matokeo yake wanamnufaisha mjasiriamali muuza chakula cha samaki ilhali wao wanaambulia patupu kwenye biashara yao hii ya ufugaji samaki.

 

 

EWE NDUGU YANGU MFUGA SAMAKI ZINDUKAAA KUTOKA USINGIZINI NAUANZE KUJITENGENEZEA CHAKULA CHAKO MWENYEWE!!!

 

 

9.UMUHIMU WA AFYALISHE YA SAMAKI KATIKA UFUGAJI SAMAKI”

 

 

Samaki kama ilivyo kwa aina zingine za mifugo wanahitaji makundi muhimu ya vyakula kwaajili ya kuweza kuimarisha afya yao. Ukosefu wa moja au zaidi ya aina yeyote katika vyakula hivyo muhimu huweza kupelekea kuzorota kwa ukuwaji wa samaki.

 

🍒Makundi hayo muhimu yanajumuisha:-

1⃣vyakula vya wanga (carbohydrates) kama mahindi 🌽, mpunga 🌾,muhogo na ngano

 

2⃣vyakula vya protini (proteins) kama soya na uduvi/dagaa

 

3⃣vyakula vya mafuta (fats) Kama karanga na alizeti

 

4⃣kundi la virutubisho muhimu linalojulikana kama vitamini (vitamins) ambavyo hupatikana kwenye vyakula mbali mbali kama damu na mchanganyiko maalum uliojitosheleza.

 

Hivyo utengenezaji wa chakula cha samaki lazima uwezekuzingatia upatikanaji wa makundi yote ya vyakula kwa samaki.

 

Zingatia kuwa samaki wa umri tofauti wanamahitaji tofauti ya vyakula. Kwahiyo mchanganyiko wa chakula cha samaki lazima uweze kumpatia uwiano sahihi wa makundi hayo ya vyakula.

 

Ili kurahisisha upatikani WA vyakula hivyo kwa samaki inabidi viwe katika mchanginyiko wa hali ya juu ili pindi samaki atakapo taka kula akutane na makundi yote ya vyakula.

 

Kwahiyo licha yakuvichanganya vyakula hivyo pia inabidi viwe katika mfumo mbao utamuhakikishia samaki kupata vyakula kwa urahisi.

Ili kufanikisha hili ndiyo maana wataalamu wanashauri kutumika vyakula vilivyo katika mfumo wa tambitambi (pellets). Ambapo kuna tambi zinazoelea kwenye maji na sisizoelea kwenye maji.

 

Kwa mfugaji ambaye anaanza anashauriwa kutumia njia ya ulishaji ya kawaida ambayo huwapatia samaki chakula katika mfumo wa vumbivumbi (broadcasting). Japokuwa njia hii inachangamoto ya upotevu wa baadhi ya chakula lakin ikifanywa kwa umakini inaweza kuleta matokeo mazuri katika ufugaji wa samaki na wapo wafugaji wengi walionufaika kupitia njia hii.

 

Kwa mfugaji anayeanza ambaye inabidi agharamikie gharama yakupata ujuzi kivitendo (cost of learning) inashauriwa ajaitahidi kupunguza gharama za uendeshaji kwa kutengeneza chakula chake mwenyewe. Ifahamike kuwa uwezi anza fuga samaki na ukapata faida hapo hapo tu ilhali bado hujui vizuri namna yakuendesha mradi wako. Kwahyo itakuwa ni busara kama utaachana na vyakula vya kiwandani ili kwanza ujifunze uendeshaji wa biashara yako. Ukishakuwa umeiva ndiyo unaweza kutanua njia za uendeshaji.

CHANGAMOTO KUBWA ILIYOPO WAFUGAJI WENGI WANAINGIA KWENYE UFUGAJI SAMAKI HUKU WAKITAKA KUPATA FAIDA YA MAMILION KWA GHAFLAA!!! Lau kama ingelikuwa hivyo basi kila mfanyabiashara leo hii angekuwa milionea!!

 

 

UTENGENEZAJI WA CHAKULA

 

Malighafi za kutengenezea chakula cha samaki hazitofautiani na zile zakutengenezea chakula cha kuku nazo ni:

 

Dagaa, pumba za mahindi, mashudu ya alizeti, damu, unga wa muhogo au ngano, soya na mchanganyiko maalum wa virutubisho.

 

Katika somo letu la leo tutatengeneza chakula kwa uwiano rahisi zaidi kwakuwa chakula hiki kimekusudiwa kwa mtu anaefuga samaki ambaye huwa anarutubisha bwawa lake na hivyo kuwezesha uzalishaji wa chakula asilia ndani ya bwawa na hivyo kupunguza utegemezi wa makundi yote ya chakula kutoka kwa mfugaji.

 

Kwahiyo tutatengeneza chakula chenye mchanganyiko wa DAGAA, PUMBA ZA MAHINDI, SOYA  na MASHUDU YA ALIZETI

 

 

KANUNI YETU 👉🏽👉🏽

Katika kilo 100 za chakula utachanganya

Dagaa kilo 30, pumba kilo 45, soya kilo 5 mashudu kilo 20.

 

Mchanganyiko huu utaenda kuusagisha na kuchanganywa mashineni ili kupata mchanganyiko mzuri.

 

darasa la afyalishe la samaki ni pana sana lakini kwa leo naomba tutosheke na haya machache.

 

 

 

 

 

Leave a Reply