NYUMBA YA KUISHI KUKU/POULTRY HOUSE

Kwanini nimeamua kuita nyumba ya kuishi kuku/poultry house. Sababu ni kwamba sehemu kuku anapoishi panatakiwa kuwa na vigezo vyote stahiki, ili kumpa kuku uhusu wa kuishi, na kumkinga dhidi ya magonjwa na wanyama wengine hatari kwake.

Nyumba ya kuku inatakiwa kuwa na vitu viuatavyo

👉 Paa
Liezekwe kwa Bati, nyasi, Trubai au kitu chochote kitakacho zuia maji, miale ya jua , ndege kuingia bandani.

👉 Sakafu
Iwe imara na rahisi kusafishika, kwa kutegemea uwezo na aina ya banda Sakafu pendekezwa ni ile yenye Rough Cement ili kuruhusu unyevu kufyonzwa, pia unaweza jenga na kupaka (udongo wa kichuguu) maeneo ya vijijini.

👉Madirisha
Yajengwe mapana, kwa wavu kuruhusu upepo kuingia na kutoka, hii hisaidia kuondolewa kwa hewa zisizotakiwa kama Ammonia Gas.

👆Madirisha yanatakiwa kuwepo pande kuu 2 za banda (Pande ndefu/ ubavuni).

👆Nyavu zinaweza kushikiliwa kwa mbao, miti migumu au kukajengwa tofali course nyembamba kulingana na ramani ya Banda lako.

👉 Ukuta
Banda la kuku linatakiwa kuanza kwa kizuizi cha upepo kuwafikia kuku moja kwa moja wawapo kwenye sakafu, inaweza kujengwa kwa Tofali, Mbao au Bati..na Kimo cha ukuta wa Banda kinatofautiana kutokana na sehemu, Hali ya hewa(joto au baridi) na vipindi vya mvua kwa sehemu husika.

Mambo ya kuzingatia wakati wa kujenga nyumba ya kuku.

👇Nyumba inatakiwa ijengwe kuta ndogo zielekezwe uelekeo wa mashariki kwenda magaribi( East- West direction ). Na pande ndefu zielekezwe kwa kupishana na uelekeo wa upepo.

👉Nyumba iwe na nafasi ya kuwatosha kuku wote kwa kulingana na aina ya kuku wako.

👉Iruhusu mzunguko wa hewa, yani kuingia na kutoka kwa hewa

👉Isijengwe karibu na majengo ya mifugo mingine mfn Nguruwe, Ng’ombe, mbuzi.

👉Ni vema nyumba ya kulelea vifaranga ijengwe kabla ya nyumba za kuku wakubwa au kama ni nyumba moja hutumika basi hakikisha (Upepo unavuma kutoka kwa kuku wadogo kwenda kwa kuku wakubwa )

👉Iwalinde kuku dhidi ya wadudu na wanyama hatari kama vicheche, mbwa n.k.

👉Iwe imara kuzuia kuanguka, au ajali zozote zisizo za lazima kwa kuku

👉Ijengwe karibu na chanzo cha maji ya kutumia kuku wako

👉Iwe rahisi kufikiwa , pindi unaleta chakula , au huduma zozote za msingi kwa kuku.

👉Iwe karibu na stoo ya kuhifadhia chakula cha kuku.

👉Iwe na vitagio/viota vya kutagia kuku (viwekwe pindi kuku anapokaribia kutaga wiki 5-6 kabla ya kuanza kutaga)

👉Sehemu za mazoezi kwa kuku (perches) ngazi/vichanya vya kulalia au kupumzikia kuku.

👈Iwe na huduma zote za msingi kama , vyombo vya maji, vyanzo vya mwanga

MENGINEYO
👇Isafishwe kwa dawa kabla na baada ya kuondolewa kuku

👇Iwe na sehemu ya kuweka maji ya kukanyaga yenye dawa

👇Iwe na komeo za kufungia milango
👇Iwe na mwangalizi wa karibu

KARIBU NITAFUTE NISIMAMIE UJENZI WA BANDA LAKO BORA LA KUKU LENYE VIGEZO KWA GHARAMA NAFUU SANA .*

Imeandaliwa na
Greyson Kahise
Mtaalamu wa kuku
0769799728 0715894582

Leave a Reply