Uzalishaji bila uchaguzi sahihi wa dume ni kufanya kazi kwa kubahatisha

BIASHARA YA MAZAO YA NG’OMBE DUNIANI 

Mazao makuu ya ng’ombe (cattle) ni: (i) NYAMA: beef (adult cattle) na veal (calves) na  sehemu nyingine za ng’ombe zinatumika kwa chakula; (ii) MAZIWA (maziwa ya ng’ombe-diary milk na mazao makuu mengine ni: butter-siagi, yogurt-mtindi and cheese-jibini); na (iii) NGOZI (hides and skins – leather, viatu, mabegi, nguo, mikanda, viti na sofa) ndiyo mazao muhimu ya biashara kwa soko la ndani na kwa masoko ya kimataifa.

Tanzania inalazimika kufanya ufugaji wa kisasa, unaotumia sayansi, teknolojia na ubunifu (science, technology and innovation) kwa sababu watu bilioni 7.3 (2015), bilioni 8.1 (2025), bilioni 9.6 (2050) na bilioni 10.9 (2100) wengi wao watahitaji maziwa ya ng’ombe, nyama na mazao mengine ya mifugo ya aina mbalimbali. Takwimu zinaonyesha kwamba kwa zaidi ya miaka 50, uzalishaji wa nyama Duniani UMEONGEZEKA MARA NNE, kutoka tani milioni 78 kwa mwaka hadi kufikia tani milioni 308 kwa mwaka kati ya Mwaka 1963 na 2014; na wastani wa utumiaji wa nyama kwa mtu mmoja Duniani (consumption per capita) kwa sasa unakadiriwa kuwa kilo 42.9 kwa mwaka.

IDADI YA MIFUGO TANZANIA

Tanzania inakadiriwa kuwa na ng’ombe (cattle) milioni 23 na asilimia 97 (97%) ya ng’ombe hao wanafugwa kiasilia (indigenous). Sensa ya Mwaka 2012, inaonyesha kwamba kwa Mwaka 2007/08, nchi yetu ilikuwa na idadi ya mashamba makubwa ya ufugaji kama ifuatavyo: kuku-mashamba 494,866; ng’ombe 120,014; mbuzi 24,193; na kondoo 14, 609.
Idadi ya mashamba makubwa ya mifugo, kwa wakati huo, hayakuzidi 700, 000.

IDADI YA MIFUGO NA ENEO LA MALISHO DUNIANI

Mwaka 2013, idadi ya ng’ombe Duniani ilikadiriwa kufikia bilioni 1.5 ikiwa ni ongezeko la asilimia 54 (54%) ya idadi iliyokuwepo Mwaka 1963. Kati ya Mwaka 2008 na 2013, idadi ya kondoo Duniani ilikardiriwa kuwa bilioni 1.1 na mbuzi milioni 881.6. Nchi zenye ng’ombe wengi Duniani ni: (1) India– milioni 329.6; (2) Brazil- milioni 209.8; (3) China- milioni 104.2; (4) USA- milioni 89; na (5) Umoja wa Ulaya- milioni 84.8.

Idadi ya kuku Duniani wanaofugwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu wameongezeka kutoka bilioni 4.1 hadi bilioni 21.7 kati ya Mwaka 1963 na 2013.

Mifugo ndiyo inakisiwa kutumia eneo kubwa la ardhi Duniani (pasture and land dedicated to the production of feed), ikitumia takribani asilimia 80 (80%) ya ardhi yote itumiwayo kwa kilimo: Hekta bilioni 3.4 zinatumika kwa ufugaji (grazing) and theluthi moja ya ardhi inayofaa kwa kilimo Duniani inatumika kuzalisha chakula cha mifugo (The sector uses 3.4 billion hectares for grazing and one-third of global arable land to grow feed crops).

Livestock is the world’s largest user of land resources, with pasture and land dedicated to the production of feed representing almost 80% of the total agricultural land.

UZALISHAJI WA NYAMA DUNIANI 

Mwaka 2012, nyama ya takribani tani milioni 304 ilizalishwa Duniani (produced worldwide); na makadirio ya wastani wa matumizi ya nyama yalikuwa kilo 42.8 kwa kila mmoja wetu kwa mwaka (consumption per capita) kwa wakati huo – kwa nchi zinazoendelea ikiwa ni kilo 33.4 kwa mtu mmoja kwa mwaka, na kwa nchi zilizoendelea ikiwa ni wastani wa kilo 76.2 kwa mtu mmoja kwa mwaka. Kwa Mwaka 2014, FAO ilikadiria ongezeko la uzalishaji wa nyama Duniani kufikia jumla ya takribani tani milioni 311.6. FAO inakadiria kwamba ifikapo Mwaka 2050 (Idadi ya watu Duniani inakadiriwa kuwa bilioni 9.6), uzalishaji wa nyama Duniani utafikia tani milioni 455.

WAUZAJI WAKUBWA WA NYAMA DUNIANI 

Brazil na India kwa pamoja ziliuza nyama kwa kiasi cha asilimia 40 (40%) ya nyama yote iliyouzwa Duniani kote (2013). Uuzaji mkubwa Duniani kwa Mwaka 2013 ilikuwa kama ifuatavyo: (1) Brazil iliuza takribani tani milioni 1.85 (20.17% ya mauzo ya Dunia nzima), (2) India tani milioni 1.77 (19.26% ya mauzo ya Dunia nzima), (3) Australia tani milioni 1.59 (17.38%), (4) USA tani milioni 1.17 (12.79%) na (5) New Zealand, tani 528,000 (5.77% ya mauzo Dunia nzima). Kwa upande wa Afrika, muuzaji mkubwa Duniani alikuwa ni Afrika Kusini (namba 22 Duniani) – iliuza tani 13,000 (0.14% ya mauzo ya Dunia nzima).

UZALISHAJI WA MAZIWA YA NG’OMBE DUNIANI 

Uzalishaji wa maziwa Duniani unakisiwa KUONGEZEKA ZAIDI YA ASILIMIA 50 (50%) kutoka tani milioni 482 Mwaka 1982 hadi kufikia tani milioni 754 Mwaka 2012. India ndiyo inaongoza kwa kuzalisha maziwa mengi kuliko nchi zote Duniani, inazalisha karibu asilimia 16 (16%) ya maziwa yote ya Dunia, ambayo ni takribani tani milioni 122 kwa mwaka. India inafuatiwa na USA, China, Pakistani na Brazil. OECD na FAO wanakisia kwamba kati ya Mwaka 2010 na 2020 uzalishaji wa maziwa utaongezeka kwa kiasi cha tani milioni 153.

UTUMIAJI WA MAZIWA DUNIANI 

Inakadiriwa kwamba kila mmoja wetu (Jumla ya watu bilioni 7.3 Duniani) anatumia wastani wa takribani kilo 108 za maziwa kwa mwaka. Takwimu zinaonyesha utumiaji wa maziwa Duniani kwa kikanda ni kama hivi: (1) Asia: 39% ya utumiaji wa maziwa Duniani, (2) Ulaya (Europe) 29%, (3) Amerika Kaskazini 13%, (4) Amerika Kusini 9%, (5) Afrika 6%, (6) Amerika ya Kati (ikiwemo Mexico) 3%, na (7) Oceania (Australia, New Zealand , n.k.) 1%

BIASHARA YA NGOZI (HIDES & SKINS) 

Ngozi za aina mbalimbali zinatokana na wanyama wanaochinjwa au kuuawa. Kati ya Mwaka 2008 na 2013, FAO inakadiria uchinjaji kwa mwaka ulikuwa hivi: kondoo 542.5 milioni na mbuzi milioni 426.6.

Afrika inakadiriwa kuwa na asilimia 15 (15%) ya jumla ya ng’ombe na takribani asilimia 25 (25%) ya kondoo na mbuzi wote Duniani. Hata hivyo, mbali ya wingi huo wa mifugo, Afrika inazalisha asilimia 8 (8%) tu ya ngozi za ng’ombe na takribani asilimia 14 (14%) tu ya ngozi za kondoo na mbuzi Duniani – Idadi ya ngozi zinazozalishwa Duniani inakadiriwa kuwa takribani milioni 240 kwa mwaka.

MTAJI MKUBWA WA UFUGAJI WA KISASA KUTOKA KWENYE UCHUMI WA GESI 
ASILIA: Kama ilivyo kwenye KILIMO na UVUVI wa kisasa, UFUGAJI wa kisasa wenye lengo la kuuza mazao ya mifugo yetu kwenye soko la ndani na masoko makubwa ya nje, tunahitaji vitu vitano muhimu sana: (i) ardhi ya malisho kwa wafugaji, (ii) matumizi makubwa ya sayansi, teknolojia na ubunifu – wataalamu na taasisi zao za mafunzo na utafiti wa kaliba ya juu, (iii) rasilimali fedha, (iv) viwanda vya kuthaminisha (value addition) na kukamilisha utengenezaji wa mazao ya mifugo yetu, na (v) sera na sheria za kustawisha ufugaji na wafugaji.

Nchi 10 bora kwa uzalishaji mwingi wa Gesi Asilia Duniani ni: (1) USA, (2) Russia, (3) Iran, (4) Canada, (5) Qatar (GDP per capita: US$ 98,986), (6) Norway (GDP per capita: US$ 100, 579), (7) China (GDP per capita: US$ 6,959), (8) Saudi Arabia (GDP per capita: US$ 24, 953), (9) Algeria (GDP per capita: US$ 5,606) na (10) Netherlands (Uholanzi). Kwa hiyo Uchumi wa Gesi Asilia ni muhimu sana kwa upatikanaji wa mitaji ya uhakika ya kuboresha na kukuza Uchumi wa Mifugo nchini mwetu (Tanzania – GDP per capita: US$ 719).

Ushirikiano na mpangilio unaotekelezeka vizuri kati ya Uchumi wa Mifugo na Kilimo; na Uchumi wa Gesi Asilia, Viwanda na Huduma (services) ndio utakaokuza uchumi wetu kwa zaidi ya 10% kwa mwaka, boresha na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja, na hatimae kutokomeza umaskini wetu na kutufanya tuwe nchi ya kipato cha kati ifikapo Mwaka 2025 (Dira yetu ya Maendeleo).

Document No. 7
Tarehe: 18 March 2015

Prof Dr Sospeter M. Muhongo (Officier, Ordre des Palmes Académiques)
FGSAf, FAAS, FASSAf, FTAAS, FGIGE, FASI, FTWAS, HonFCAGS, HonFGSA, HonFGS, CGeol, EurGeol.

 

Chanzo: Wavuti

 

Leave a Reply