Ufanye nini ili kuku watage mayai mengi

PAKUA APP YA UFUGAJI HAPA

 

Na mwandishi wetu Sefania Kajange

 

Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya,

 

1)      Umri wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10-14) au zaidi ya hapo kwa kulingana na ufugaji wako ulivyo kwa mfano kama unafuga na kumuachia kuku mwenyewe ajicontrol na au unamcontrol kuku lini aanze kuatamia na aatamie mayai mangap na yawe yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usiozidi nyuzi joto 20ºC. Iwapo hali ya joto iko juu kuliko 20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5).

 

2)      Ili kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika.

 

3)      Ganda la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa  kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa au yai linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga vyenye afya mbaya au vilivyokufa na wakati mwingne vifaranga vikiwa having viungo vyote na kutoeleweka.

 

4)      Hifadhi mayai ya kuangua kwenye makasha makavu ndani ya shimo lililopo ardhini katika sehemu yenye ubaridi kuliko sehemu zote ndani ya chumba.

 

5)      Kabla mayai hayajaatamiwa chunguza mayai ambayo yana mbegu na yale yasiyo na mbegu. Mayai ya kuku aliyepandwa na jogoo yanakuwa na mtandao wa mishipa ya damu mapema sana ambayo inaweza kuonekana kwa kutumia mwanga mkali wa kurunzi. Au kwa njia ya kienyeji yai linapokaa zaidi ya sku 17 na kuendelea likiwa limehifadhiwa ukilipasua utaona hiyo mishipa ya damu damu kwenye yai. Na lile ambalo halina mbegu hautaona hayo.

 

7)      Baada ya mayai kuatamiwa kwa siku saba hadi kumi yanaweza kuchunguzwa mayai yasiyorutubushwa na yenye viini vilivyokufa yanaweza kutambuliwa katika siku saba baada ya kuanza kuatamiwa. Na unaweza kuyatoa ili kutomsumbua tu bure kuku.

 

8)      Wakati wa kupima kwa kutumia mwanga wa kurunzi mayai yaliyorutubishwa yanakuwa na mishipa ya damu inayoonekana, na doa jeusi ambalo ndicho kiini cha uhai.

 

9)      Iwapo kiini cha uhai kimekufa, kinaoonekana kama kitu cha mviringo mfano wa pete kuzunguka kiini hai.

 

10)  Mayai ambayo hayajarutubishwa yanakuwa na utando ambao utaonekana ni mweupe tu bila kuwa na damu damu

 

Matunzo kwa kuku anayeatamia

 

Kabla ya kuku kuanza kuatamia ni vzuri yafuatayo yanatakiwa yawe yameandaliwa au kufanyika.

 

 1. Achunguzwe kama hana dalili zozote za ugonjwa. Na kama zipo atibiwe mapema

 

 1. Apuliziwe dawa ya utitiri na kiota pia kiwekwe hiyo dawa.

 

 1. Awekewe mayai ambayo una uhakika atayamudu kulingana na umbo lake au wakati mwingine tumia uzoefu wake wa nyuma.

 

 1. Aandaliwe chakula na maji karibu na viota sina maana ya kwamba pale pale lakini angalau karibu ili akitoka tu aweze kupata kiurahisi na kwa haraka na kuweza kuendelea kuatamia.

 

 1. Mpe vitamin kwenye maji na glucose wakati mwingine sina maana kila siku angalau siku moja kwa wiki au siku 2 ili apate nguvu na vitamin kumuondolea stresi.

 

 1. Kiota kiwe na vipimo sahihi ili na yeye ajinafasi. Inashauriwa sentimeta 35 upana na urefu pia

 

Mwisho kumbuka kuwa maandalizi mazuri ya kuku wa kutaga vizuri na kuatamia huanza tokea sku ya kwanza kabisa. Hii ni kwa kuwalea kuku vzuri ili wawe na uzao mzuri

 

 

 

Zingatia yafutayo ili mayai yote yaanguliwe

Kwa kuku wanaoatamia wenyewe na wakiwa wametaga wao tatizo kubwa linakuwa ni

 

 1. Mayai kushikwa na mikono yenye malashi (perfume) au mafuta yoyote wakati wa kumuwekea kuku kwenye kiota chake.
 2. Kuyashika mayai ukiwa umetoka tu kunawa au kushika maji hivyo kusababisha unyevu nyevu. Najua unaweza jua uko sawa kumbe kiasi kidogo cha hayo maji mikononi kikaleta madhara
 3. Kumpa mayai kuku ambae hana mwili mkubwa wa kuyamudu mayai yote kuyaatamia na hivyo kutotoa joto la uhakika.
 4. Kuku mwenyewe kukosa utulivu wakati wa kuatamia yaani kushindwa kutulia kwenye kiota kwa muda unaotakiwa.
 5. Inaweza kuwa ni mayai kukaa muda mrefu lakini Mara nyingi hii kwa kuku wanaoatamia wenyewe ni kwa mara chache sana inaweza kuathiri.

 

Ushauri

 1. Kabla ya kushika mayai tumia majivu kujipaka mikononi ili kuondoa marashi na mafuta ndipo ushike mayai.
 2. Acha kabsa visababishi vnavyoweza kuleta unyevu unyevu mfano. Kuyafuta mayai machafu kwa kitambaa kilicholowana kidogo eti unayasafisha, kuku wa kienyeji hata yai likiwa chafu anatotoa tofauti na machine
 3. Mchunguze kuku anayeatamia kama muda mwingi yupo kwenye kiota au nje? Na mpe chakula karibu na eneo la kuatamia ili asisumbuke kwenda mbali ambako anaweza kulowana na anaporudi kwenye kiota akaingiza unyevunyevu hapo tunasema mchawi ni yeye mwenyewe bila Mfugaji kujua.
 4. Kuwa makini kuangalia kama kwenye kiota kuna viroboto na wadudu wengineo na je kuku hawana utitiri?

 

Huu ni msingi imara wa kupata vifaranga wengi na bora

 

Fuga KIBIASHARA kwa MALENGO timiza NDOTO yako.

🙏🇹🇿✍

 

Leave a Reply