Ufugaji bora wa samaki

MBINU MUHIMU WAKATI WA UANZISHAJI UFUGAJI WA SAMAKI

 • Mfugaji anatakiwa awe na shauku na dhamira ya kweli ya ufugaji.
 • Kufanya tathmini ya rasilimali alizonazo kwa ajili ya mradi wa ufugaji wa samaki.
 • Chanzo endelevu cha mtaji kwa ajili ya mradi.
 • Hulka ya uvumilivu na kuthubutu.
 • Tathmini ya soko la bidhaa za samaki.
 • kujipatia maarifa ya msingi ya ufugaji wa samaki

SIFA ZA ENEO LA KUFUGIA SAMAKI

 • Eneo la kufugia samaki linatakiwa liwe na maji ya kutosha kwa mwaka mzima.
 • Eneo la kufugia samaki linatakiwa liwe na udongo unaoweza kutuamisha maji.
 • Eneo zuri la kufugia samaki ni kuwa eneo lisiwe na historia ya mafuriko, kwa kuwa mafuriko yakitokea samaki waliokuwa bwawani wataondoka na maji na bwawa litafunikwa na udongo.
 • Eneo zuri la kufugia samaki ni lile linalofikika kwa urahisi.
 • Eneo la kufugia samaki pia linatakiwa kuwa ni eneo lenye amani na utulivu na watu wenye kuelewana.
 • Kuwa na soko la bidhaa.
 • kuwa na umiliki wa ardhi wa uhakika.

UTENGENEZAJI WA BWAWA LA SAMAKI

Zipo namna mbalimbali za utengenezaji wa bwawa la samaki, kulingana na aina ya bwawa lenyewe, Hali ya uchumi, wingi wa samaki watakaofugwa pamoja na aina ya samaki watakaofugwa.
Zifuatazo ni Aina za mabwawa ya kufugia samaki.

1.Bwawa la kuchimba udongo bila kujengea “Earthen Pond”.

 1. Bwawa la kuchimba udongo na kujengea kwa Matofali, Simenti na Zege.

UANDAAJI NA UPANDIKIZAJI WA VIFARANGA AU MBEGU ZA SAMAKI KATIKA BWAWA LAKO

Kabla ya kuvisafirisha vifaranga kutoka kwenye bwawa wanaloishi ni vema vikatolewa na kuwekwa kwenye vibwawa vidogo vidogo kwa muda wa kati ya saa 24 hadi 72 (kutegemeana na umbali wa safari) bila chakula

 • Wakati wa kupandikiza mfugaji anatakiwa akifika asivimwage vifaranga kwenye bwawa bali anatakiwa kuyaruhusu maji yaliyobeba vifaranga yabadilishane ujoto na maji yatakayopokea vifaranga. Hapa mfugaji anatakiwa kuliweka kontena au chombo alichobebea vifaranga kielee kwenye maji anayotaka kufugia kwa muda wa dakika kati ya 30 hadi 35, baada ya hapo chombo kilicho na vifaranga kifunguliwe na kiinamishwe ili maji hayo yaweze kukutana na yale yaliyoandaliwa kwa ajili ya kufugia na hapo ataruhusu vifaranga kuingia wenyewe kwenye bwawa husika.
 • Iwapo utafika na kuvimwaga vifaranga kwenye bwawa jipya bila kufuata utaratibu huo wa kitaalamu basi tofauti ya ujoto wa maji kati ya chombo kilichosafirishiwa vifaranga na bwawa unaweza kusababisha vifaranga wote kufa kwa muda mfupi, kitaalamu wanasema kuwa vifo vya vifaranga hivyo vinasababishwa na mshituko wa joto.
 • Jambo lingine la kuzingatia ni kuwa uandaaji na usafirishaji wa vifaranga ni vizuri ukafanywa muda ambao hali ya hewa inakuwa na ubaridi. Muda unaopendekezwa zaidi na wataalamu ni asubuhi au jioni kwa sababu muda huo samaki wanakuwa na uwezo wa kuhimili misukosuko ya safari tofauti na hali ya hewa inapokuwa ya joto.

UFUGAJI WA SAMAKI WAKATI WA KIANGAZI NA MASIKA

Kimsingi hakuna tofauti kubwa wala athari kubwa sana za ufugaji wa samaki wakati wa kiangazi ukilinganisha na wakati wa masika, tofauti zilizopo ni ndogo ndogo ambazo kitaalamu hazina madhara makubwa kwa mfugaji.

 • ulaji wa chakula wa samaki na ukuaji wao
 • uchafuzi wa maji yanayoingia kwenye mabwawa ya kufugia

ULISHAJI NA UTUNZAJI WA SAMAKI BWAWANI

 • Samaki  wapewe chakula angalau mara 2 kwa siku (saa 3-4 asubuhi  na 9-10 jioni) /hewa ya kutosha .
 • Kuwapa vyakula tofauti kutegemeana na silka ya aina ya samaki unaowafuga.
 • Kuna samaki wanaofaidika na vyakula vya nyama nyama kama vile kambale na sangara (hawa hawali pumba) na kuna samaki wengine kama sato wanakula vyakula mchanganyiko wa nyama na mboga mboga na wapo wengine wanaokula vyakula vyenye asili ya mimea tu “carps”.

TABIA ZA ULAJI WA SAMAKI

 • Samaki wanaokula nyama, (sangara na kambale).
 • Samaki wanaokula mimea ‘carps’.
 • Samaki wanaokula vyakula mchanganyiko (nyama na mimea) kama perege, sato na mwatiko (samaki wa maji chumvi).

MUONGOZO WA MAHITAJI YA VIINILISHE VYA SAMAKI

Wanga        20-25%

Mafuta                  10-15%

Vitamin       1-2%

Madini                   1-2%

Protini                   18-45%

NB; Maji – hapa ifahamike kuwa wakati tunazunguzia viwango vya maji vinavyohitajika kwa wanyama wengine wafugwao, hitaji la maji kwa samaki ni ubora wa maji anayofugiwa na sio wingi wake.

TARATIBU ZA ULISHAJI WA SAMAKI

 

MASOKO YA SAMAKI

 • Soko la awali, hili ni soko la moja kwa moja kutoka kwa muuzaji ambaye ni mfugaji kwenda kwa mlaji,
 • Soko la kati, katika soko hili kwa kawaida kunakuwa na mtu wa kati ambaye ananunua samaki kwa mfugaji kwa lengo la kwenda kuwauzia walaji.
 • Soko la kimataifa, hili ni soko linalofanyika nje ya nchi (baina ya nchi moja na nchi nyingine).

 

KWA HISANI YA

Leave a Reply