ULEAJI BORA WA VIFARANGA
Mambo mengi yanayohusika katika uleaji wa vifaranga kwa upande wa HARSHO FEEDS tupo tayari kumhudumia mfugaji wa kuku kwa kumpatia chakula na utaalamu sahihi. Katika uleaji wa vifaranga kuna tofuati kati ya vifaranga wa nyama na wale wa mayai hasa katika chanjo na lishe.
MATAYARISHO
Banda la kuku liwe imara kuepuka wizi, panya, ndege, nyoka na kadhalika. Jenga sehemu yenye hewa ya kutosha, kavu na mbali na kuku wengi.
Kabla ya kuingiza kuku, safisha banda lote nje na ndani kwa dawa ya kuangamiza wadudu. Paka chokaa kwenye kuta zote. Hakikisha banda haliwi na joto kali, baridi, kuingiwa na mvua, jua au upepo.
Tayarisha chakula bora, maji safi, madawa-vifaa vya kutosha na tandiko safi.
KABLA YA KUFIKA VIFARANGA
Banda la kuku liwe tupu wiki moja hadi mbili baada ya kusafishwa na dawa. Vifaranga utakaopokea wawe na historia nzuri.
a) Usichanganye vifaranga wa sehemu tofauti
b ) Tengeneza mduara ndani ya banda kwa kutumia hardboards kwa urefu wa sentimeta 50 na katikati yake weka taa ya (balbu) au jiko la mkaa, hakikisha mwanga wa kutosha ili vifaranga waone chakula na maji.
c) Weak tandiko la kuku (litter) safi, vifaa vya maji na chakula kulingana na idadi ya vifaranga.
d) Masaa matano kabla ya vifaranga hawajafika washa taa za joto au jiko la mkaa kwa ajili ya kutoa joto kwa vifaranga (35oc) weak maji ndani ya vyombo ili yawe na joto kiasi. Hakikisha kuna hewa ya kutosha na hakuna upepo unaoingia.
e) Iwapo vifaranga vinatoka mbali na vimechoka, weka glucose/sukari kidogo kwenye maji (kijiko cha chakula kwa lita tano za maji)
KUPOKEA VIFARANGA
Watoe vifaranga kwenye maboksi na kuwaingiza ndani ya mduara, hakikisha unayo hesabu kamili.
Vifaranga wote wanywe maji na uwanyweshe ambao hawajakunywa maji. Baada ya masaa mawili, weka chakula kwenye vyombo vya chakula.
Hakikisha kuna mwanga masaa 24 kwa siku tano za mwanzo na joto la kutosha.
Hakikisha kuku wana nafasi ya kutosha. Panua duara la kuelekea kadri kuku wanavyokuwa na ondoa duara baada ya wiki tatu. Kuku wakibanana hawakui vizuri kwa kipindi hiki.
ULEAJI KUKU MAYAI (Layers)
Kila kuku anayetaga apate eneo la futi mbili (2) za mraba. Nyumba iwe na madirisha ya kutosha kuweza kuingiza hewa safi. Tumia kati ya vitu vifuatavyo kwenye sakafu kama godoro (litter):-
a) Maranda ya mbao
b) Maganda ya mpunga
c) Majani makavu yaliyokatwakatwa
VIFAA
Weka vifaa vya kutosha kulishia chakula na maji kwenye banda lako kama ifuatavyo.
Sinia moja litumike kulishia vifaranga 50. Vifaa vya maji tumia
Chick Fount moja kwa vifaranga 100.
Kuku wakubwa tumia “Feeder” moja kwa kuku 50 na drinker moja kwa kuku 60
CHAKULA KINACHOTAKIWA
Umri (wiki) | Aina ya chakula |
0-4 | Chick Starter |
5-8 | Chick Mash |
9-20 | Growers Mash |
21-89 | Layers Mash |
UMRI
(wiki) |
CHAKULA
(Grams) |
MAJI (ml) | WASTANI
WA UZITO (grams) |
|
1 | 12 | 13 | 20-30 | 50 |
2 | 19 | 20 | 40-50 | 100 |
3 | 25 | 25 | 50-50 | 150 |
4 | 30 | 29 | 60-70 | 200 |
5 | 35 | 33 | 70-80 | 300 |
6 | 40 | 37 | 80-100 | 400 |
7 | 45 | 41 | 100-120 | 500 |
8 | 50 | 46 | 120-130 | 650 |
9 | 54 | 51 | 130-140 | 800 |
10 | 60 | 56 | 150-160 | 900 |
11 | 67 | 61 | 160-165 | 1000 |
12 | 65 | 66 | 165-170 | 1100 |
13 | 68 | 73 | 170-175 | 1200 |
14 | 71 | 77 | 175-180 | 1300 |
15 | 74 | 75 | 180-190 | 1400 |
16 | 76 | 77 | 190-195 | 1500 |
17 | 78 | 80 | 195-200 | 1600 |
18 | 80 | 86 | 20-210 | 1700 |
19 | 83 | 95 | 210-220 | 1750 |
20 | 86 | 100 | 220 | |
Katika kilele cha utagaji kuku mmoja anahitaji gram 120-135 kila siku hii ni sawa na kilo 12 – 12/siku/kuku/100. kiasi hiki kinategemea ubora na lishe ya kuku unachotumia.
MPANGO WA KUBADILI CHAKULA
Unapobadili chakula usibadili ghafla. Badili chakula kutoka Chick Starter hadi Growers Mash na Growers Mash hadi Layers Mash kwa mpangilio ufuatao.
½ Chick Starter + ½ Growers Mash changanya vizuri na lisha kwa wiki moja. Kisha endelea na Growers Mash fuata utaratibu huo utakapobadili Growers kwenda Layers
|
MPANGO WA KINGA – KUKU WA MAYAI
CHAKULA KINACHOHITAJIKA Umri (Wiki)
Aina ya chakula
0-3 Broiler Starter
4-8 Broiler Finisher
|
Rudia chanjo ya New Castle kila baada ya miezi 3-4, chanjo ya Mareks hufanyika Hatchery kabla ya mfugaji kupewa vifaranga.
SIFA ZA KUKU BORA WA MAYAI
Kuku waliotunzwa vizuri tegemea yafuatayo:-
ª Vifo wakati wa kulea 3% – 5%
ª Vifo wakati wa utagaji 1% kwa mwezi
ª Umri wa kuanza kutaga wiki 19-20
TIBA YA MINYOO
Hii hufanyika kwenye kuku wa mayai:
Mara ya kwanza wapewe wiki ya 8 kurudiwa ya 18
Baada ya wiki 18 wasipewe tena na dawa ya minyoo hadi baada ya kupitia kiwango cha juu cha utagaji (peak production)
Baada ya Peak Production kuku wapewe dawa ya minyoo kila baada ya wiki 8-10 au minyoo inapoonekana kwenye kinyesi
KUKU WA NYAMA (BROILERS)
Kila kuku wa nyama anapaswa apate eneo la futi moja (1) ya mraba. Nyumba iwe na madirisha ya kutosha, hewa safi, sakafu iwe na godoro (litter) ya randa au maganda ya mpunga.
VIFAA
Vifaranga 100 wanaweza kutumia chombo kimoja cha kulishia
(chick plate) na chombo kimoja cha kunywea maji (chick fount) kwa wiki moja kuanzia wiki ya pili na kuendelea tumia chombo kimoja cha kulishia (feeder) chenye kipenyo cha sentimenta 38 kwa kuku 50 .
MPANGO WA KINGA – KUKU WA NYAMA
UMRI (siku/wiki) | AINA YA CHANJO | NJIA YA KUWAPA |
Siku 7 | New Castle | Maji ya kunywa |
Siku 14 | Gumboro | Maji ya kunywa |
Siku 21 | Gumboro | Maji ya kunywa |
Muhimu Zingatia
Fuata ratiba ya chanjo kama ilivyopendekezwa
Pata chanjo toka sehemu inayojulikana na yenye uhakika wa upatikanaji
Hifadhi chanjo yako kwenye fridge na sio freezer sehemu yenye nyuzijoto 4 – 8 centigrade.
Chanjo isitolewe zaidi ya saa 4.30 asubuhi kwa sababu chanjo inaweza kuharibika kutokana na joto au mwanga mkali wa jua.
Unapoona dalili za ugonjwa, kama kusinzia, kujikunyata, kuharisha, kutokula chakula, kutokunywa maji, kuhema kwa tabu au vifo, toa taarifa haraka kwa mtaalamu wa mifugo ili upate ushauri na huduma mara moja.
Jarida hili limetayarishwa na HARSHO TRADING CO. LTD
Head Office: Kawawa street. Moshi. Branch: Along Moshi Arusha Rd. Bomang’ombe P.O. BOX 810.
Moshi, Tanzania
Tel: 0784 287409 / 027 2753503
Fax: +255 27 2753505
E-mail: harshotrad@yahoo.com
Website:- www.harshotz.com