Ndege wa kufuga ni kama vile kuku, bata, batamzinga, kanga na bata bukini. Kuku hasa ndio wanaofugwa zaidi.
Watu wengi hufuga kuku wa kienyeji ambao huachiliwa kuzurura wakijitafutia chakula. Ingawa kuku wa kienyeji hawatunzwi vizuri, wana thamani kubwa kwa familia nyingi kwa vile mayai na nyama hutumika na familia kwa chakula na kuwapa protini na wakiuzwa huongeza kipato.
Shida zinazokumba kuku wa kienyeji zikipunguzwa, wana uwezo wa kutoa mazao ya hali ya juu.
Katika sehemu hii, jifunze jinsi ya kutunza kuku wako vizuri kwa kuwajengea kibanda chenye usalama, kuwalisha vyema na kuwazuia kutokana na magonjwa yanayoathiri kuku.
Kibanda Salama Cha Kuku
Katika kila jamii kuna njia ya kawaida ambayo kuku hupewa makao. Hifadhi njema huwalinda kutokana na:
- Hali mbaya ya hewa
- Wanyama wanaowinda
- Wezi
Makao pia yanafaa kuwatolea kuku mahali pa kutaga mayai. Hii hurahisisha upatikanaji wa mayai na huhakikisha ndege hawasumbuliwi.
Kanuni sahihi za makao mazuri
- Tumia vikapu kwa kujisetiri usiku na mchana kwa vifaranga wadogo ili kupunguza gharama na kazi inayohusishwa.
- Mara kwa mara tumia nyenzo za nyumbani kupunguza gharama.
- Tumia nyavu za nyaya kwa madirisha kuwazuia wanyamawanaowinda.
- Tayarisha chungu ama kikapu ambacho kuku wanaweza kutaga mayai na kiweke ndani ya nyumba
- Weka vitulio vya ndege na viota ndani ya nyumba bila ya kuwafanya kuku kupatwa na baridi.
- Zuia kibanda kutokana na mvua kubwa na jua kali.
- Waweke vifaranga wachanga pamoja na mama yao lakini mbali na kuku wengine wakubwa.
- Hakikisha nyumba zinafikiwa kwa urahisi na ni safi.
Kulisha Kuku
- Tumia lishe yenye viambato vya nyumbani kwa kuku wa kienyeji.
- Nunua viambato vya lishe vilivyokosekana, kama vitamini ama protini vya nyumbani.
- Badilisha aina ya lishe ukitegemea upatikanaji,ubora na bei zinavyobadilika.
- Punguza nambari ya ndege wakati wa vipindi vya kiangazi na ikiwa lishe imekuwa ghali.
- Ukibadilisha lishe na viwango vya lishe,mara kwa mara fanya hivyo pole pole.
- Changanya viambato vya lishe kwa njia ya usawa na katika viwango vidogo vidogo.
- Tumia nyenzo za nyumbani kama mikebe ya mafuta ya kupika ama vijiti vya kiberiti kupima viwango vya lishe.
- Hifadhi viambato vya lishe kwa chombo kilichoinuliwa juu ya ukuta kuzuia unyevunyevu.
- Zuia kuingia kwa panya na aina zingine za ndege dhidi ya kuingia katika chumba cha kuhifadhi lishe.
- Hakikisha kuna mzunguko wa kutosha wa hewa ili viambato vya lishe visikuwe maji maji.
- Usitumie vyakula vyenye kuvu ama vilivyo geuka rangi.
Jinsi ya kukuza funza (minyoo) ili kuwalisha kuku
Funza wanaweza kupandwa ukitumia mbinu rahisi na hutumiwa kama nyongeza katika lishe ya vifaranga wadogo.
Hivi ndivyo inavyo fanywa.
- Changanya damu na matumbo ya mnyama (kwa mfano ng’ombe ama mbuzi) na samadi ya ng’ombe katika chungu kikubwa kilicho wazi.
- Jaza chungu na 1/3 ya maji.
- Nzi watataga mayai yao katika mchanganyiko huu na funza wataula.
- Kiache chungu wazi wakati wa mchana na kifunike wakati wa usiku.
- Funza wakiwa wakubwa,wakusanye kwa kumwaga maji pole pole kwenye chungu.
- Funza wataelea na unaweza kuwaosha na kuwalisha kwa ndege moja kwa moja.
- Kumbuka kukiweka chungu mbali na maeneo ya umma kwani hunuka sana.
Jinsi ya kukuza mchwa
- Chukua chungu chenye shingo fupi kinachoweza kuhimili lieta 10 za maji.
- Kijaze na samadi ya ng’ombe na majani makavu na nyunyuzia maji kidogo.
- Kiweke chungu juu chini na mdomo kwenye ardhi.
- Baada ya mchana mmoja na usiku mmoja,chungu kitakuwa kimejaa mchwa.
- Toa mchwa katika chungu mahali ambapo ndege wanaweza kuwala.
Chanzo: The beehives