UGONJWA WA MAPELE NGOZI (LUMPY SKIN DISEASE)

Ugonjwa wa mapele ngozi (lumpy skin disease)LsdUgonjwa wa mapele ngozi (lumpy skin disease)

PAKUA APP YA UFUGAJI HAPA

Ugonjwa wa mapele ngozi (Lumpy skin disease, LSD) ni ugonjwa wa kuambukizwa unaowapata ng’ombe wa umri wowote na kusababisha hasara kiuchumi hasa kutokana na ngozi ya ng’ombe kuharibiwa na uwepo wa mapele sehemu mbalimbali za mwili. Ugonjwa huu huenezwa na virusi wajulikanao kwa jina la kitaalamu kama Lumpy skin disease virus waliopo kwenye familia ya Poxviridae.

Ugonjwa huu ulitambuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1929 nchini Zambia (iliyojulikana kama Northern Rhodesia). Kati yam waka 1943 na 1945 ugonjwa ukaripotiwa nchini Botswana (Bechuanaland), Zimbabwe (Southern Rhodesia) na Jamhuri ya Africa ya Kusini. Baadaye ugonjwa huu uliripotiwa Africa Mashariki nchini Kenya mwaka 1957, Sudani mwaka 1972 na Africa Magharibi mwaka 1974 kisha ukaenea Somalia mwaka 1983, Misri mwaka 1988 na mwaka 1989 nchini Israel. Haijulikani lini uliinngia nchini Tanzania lakini huenda uliingia baada ya Kenya kulingana na wafugaji wa Tanzania na Kenya kuchangia malisho hasa maeneo ya mipakani. Ugonjwa huu nchini umekuwepo na umekuwa ukijitokeza maeneo mbalimbali ya nchi. Ni rahisi sana kuubaini ugonjwa hu una si rahisi kuchanganya na magonjwa mengine kulinga na uwepo wa mapele mwilini.

Dalili za ugonjwa mapele ngozi

-Ng’ombe anaweza kuwa na joto kali la nyuzi joto 40 hadi 41.5 za sentigredi huku akiwa anatokwa machozi, anakosa hamu ya kula Chakula, ananyong’onyea na anashindwa kutembea.

-Muda mfupi baadaye viuvimbe vya aina yake (mapele) huanza kujitokeza, ambavyo yanaweza kuwa mwili mzima, au yakawa sehemu ya kichwa, shingo, kiwele, miguuni tu. Mapele hayo mwanzo hujionyesha kama maeneo yenye mduara yaliyozibwa na nywele zilizosimama yenye kipenyo cha milimita 5 hadi 50 hivi. Ni uvimbe mgumu uliojitokeza juu ya ngozi ya kawaida na ngozi ya uvimbe huwa nene. Endapo vimelea nyemelezi (bakteria) wakiingia kwenye uvimbe hupelekea ngozi ya juu kutoka kuwa vidonda ambavyo vinaweza kupona na kuacha kovu.

-Matezi yaliyo karibu na ngozi huvimba.

-Ng’ombe hutiririsha mafua mazito ambayo huambatana na kujitokeza kwa vidonda mdomoni na vinaweza pia kujitokeza kwenye njia yote ya chakula kunakopelekea ng’ombe kushindwa kula chakula.

-Ng’ombe hutoa mate mfululizo

-Ng’ombe hukohoa na mara nyingi huambatana na upumuaji wa haraka

-Macho pia hutoa machozi na huwa na vidonda

-Ng’ombe walio athirika sana hukonda sana na hutakiwa kuondolewa kundini maana hawezi kuleta tija. Kama ni ng’ombe wa maziwa utoaji maziwa kukoma na kama ni dume hawezi kupanda majike na endapo ni kulimia hataweza kufanya kazi tena. Ng’ombe aliye athirika sana hufa kwa kutokula Chakula kutokana na vidonda mdomoni. Vifo vya ng’ombe walio athirika havizidi asilimia 40.

-Ngo’mbe wenye mimba hutupa mimba kufuatia milipuko ya Ugonjwa wa Mapele Ngozi na ndama huzaliwa wakiwa na Uongwa wa Mapele Ngozi yaliyosambaa mwilini.

 

Kinga dhidi ya Ugonjwa wa Mapele Ngozi

Ugonjwa huu hauna dawa, matumizi ya antibiotiki husaidia tu kuua wadudu nyemelezi aina ya Bakteria. Wanyama wagonjwa watengwe na kisha wapewe dawa za kuzuia maambuki ya wadudu nyemelezi. Kuchoma sindano ya antibiotiki itasaidia vimelea vya bakteria maeneo mbalimbali yenye mapele. Matumizi ya dawa za kupulizia hasa kwenye vidonda yatasaidia kufukuza nzi wasitue kwenye vidonda na kuacha vimelea vya bakteria lakini pia kusadia kuua vijidudu vilivyopo kwenye vidonda.

Nimesema ugonjwa huu haunda tiba, hivyo kinga ndiyo njia pekee ya kuzuia ugonjwa huu usiwapate mifugo wako. Na kinga pekee ni ya kutumia chanjo. Hivyo chanja Mifugo wako kabla ugonjwa haujaingia kwenye Mifugo yako maana ukishaingia huruhusiwi kuchanja hadi pale utakapotokomea.

Afrika kuna aina mbili ya chanjo ambazo zinatumika na zimeonyesha Mafanikio: LSDV Neethling strain (Live attenuated vaccine) by Onderstepoort Biological Products (OBP) and chanjo za Sheeppox virus (SPPV). Chanjo za SPPV zinatumika Mashariki ya kati, Misri na Uturuki.

Chanjo inayopatikana nchini Tanzania kwa sasa inaitwa LAMPIVAX® kutoka Kenya (picha chini) ambayo ni ya LSDV Neethling strain

Tanzania ipo mbioni kutengeneza chanjo yake ya kupambana na Ugonjwa wa Mapele Ngozi.

Chanjo ya Ugonjwa wa Mapele Ngozi (LAMPIVAX®)

 

 

 

Leave a Reply