Pakua app yako ya Ufugaji HAPA ili uweze kufuatilia elimu hii kiganjani mwako

Ugonjwa huu husababishwa na protozoa. Ugonjwa huu wa kuhara damu huonekana katika sura mbili.

 

(1) Caecal coccidiosis       Sura hii ya ugonjwa  hushika vifalanga na huathiri kwa kiasi kikubwa sekamu (caecum).

 

Dalili zake

 

_Vifaranga huonekana wamezubaa, kushusha  mabawa

_Kinyesi kuonesha damu

_Vifo vingi hutokea

_Vifaranga kushindwa kula na kunywa.

_Damu huonekana kwa wingi katika kinyesi kabla ya kifo.

Katika sura hii Kifaranga chenye koksidiosisi sio lazima kionesha dalili zote au kinyesi cha damu. Unaweza kuona vifaranga wako wamezubaa, huku wameshusha mabawa vifo vingi kila asubuhi. Basi tambua vifaranga wako wamekumbwa na ugonjwa huu. Usipo kuwa makini unaweza kujiuliza ni ugonjwa gani? Kwa kuwa umezoea mpaka uione damu kwenye kinyesi ndio ujue kuwa ni coccidiosis.

 

(2) Intestinal coccidiosis      Sura hii ya ugonjwa huonekana kwa kuku wakubwa.

 

Dalili zake

 

_Kuku kupunguza ulaji wa chakula

_Kuku kupungua uzito

_ Kuku kuangusha  mabawa

_Kuku kuharisha kijivu na damu, ugoro na mala nyingi kinyesi huwa kimechanganyikana na damu damu

_ Kuku kukonda

_Utagaji wa mayai kupungua sana.

 

UKIUPASUA MZOGA

 

  1. Utumbo kuonekana na damu
  2. Utumbo butu kuwa na damu damu
  3. Utumbo butu kuvimba
  4. Utumbo sehemu za ndani kuonekana kama vile umesagika,cloaca ya kuku hubadilika rangi na kuwa na vidotidot kama vya damu [hemorrhage]

 

KUZUIA UGONJWA HUU

_ Epeka hali ya unyevu unyevu katika banda la kuku

_Ni muhimu kizingatia hali ya usafi kwenye banda la kuku ikiwa ni pamoja na usafi wa vyombo vya chakula na maji.

 

MATIBABU YA UGONJWA WA COCCIDIOSIS

 

_Ebs3

_Anticox

_Vitacox

_Amprolium

_Dawa za sulfa

Tunawatakia ufugaji mwema

Imeandaliwa na Lukas Michael (lukasmichael811@gmail.com) na Kuhaririwa na Mhariri mkuu wa Tovuti hii

Leave a Reply