Site icon Ufugaji Bora

Ukweli kuhusu homa ya mafua ya ndege

 

Vipi tunaweza kujikinga na homa ya mafua ya ndege 

Homa ya mafua makali inaweza kumpata binadamu na ina uwezo wa  kukufanya ukawa mgonjwa sana au hata kukuua. Njia rahisi ya kujikinga usipate homa hiyo ni kujiepusha na kushikashika kuku/bata au ndege au kinyesi chao, kunawa mikono kwa kutumia jivu  au sabuni na maji mara tu kabla au baada ya kushika kuku/bata au ndege,  na kwa kupika kuku/bata/ndege na  mayai  vizuri kabla ya kula. Ifuatayo ni taarifa mahususi:-

 

Usafi wa jumla

 

Jiepushe na kukaribia au kugusa ndege wa aina yoyote

 

Ukiona ndege aliyekufa au mgonjwa, usimguse kama hujavaa glavu 

 

Hakikisha kuwa nyama ya kuku/bata/ndege na mayai vinapikwa vizuri

 

Usichinje au kutayarisha kuku/bata waliokufa au wagonjwa kwa ajili ya chakula

 

Chukua tahadhari ikiwa unatembelea  mashamba au maeneo mengine wanapofugwa kuku/bata na ndege

Ikiwa utagusana kwa bahati mbaya na kuku/bata  katika eneo lenye maambukizo (kama vile kuugusa mwili wa ndege au kinyesi chake, au kukanyaga udongo wenye kinyesi cha kuku/bata/ndege):

 

Anzisha majadiliano na marafiki, familia, majirani na jamii kwa ujumla kuhusu mikakati ya kuzuia kuenea kwa mafua ya ndege katika mtaa wenu

Exit mobile version