Na mwandishi wetu Sefania Kajange:
Upungufu wa vitamini A hujitokeza pale kuku atakapo kosa vitamini A mwilini.
Ukosefu wa Vitamini A,  huathiri kuku aina zote na umri wowote ila hasa zaidi kuku wadogo.
Tatizo hili limewakumba wafugaji wengi kwa kuku wao na jinsi macho yanavyo vimba hufanana sana na ugonjwa uitwao Infectious Coryza (Mafua ya kuku)
DALILI
-Dalili kuu ya ugonjwa huu ni macho kuvimba na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya kipande iliyolowa maji.
-Ukuaji wa manyoya huwa hafifu.
-Kuku kukua kwa taratibu huku panga  zikionekana kuwa dhaifu.
-Ugonjwa huu mara nyingi hujitokeza wakati wa kiangazi.
👉Vifo ni vichache kwa ugonjwa huu na vifo hivyo ni kwasababu macho yanaziba na kuku kushindwa kuona chakula.
KINGA
Ni kuwapa kuku mchicha au majani mabichi mara kwa mara.
-Pia kuku wapewe vitamini za viwandani hasa nyakati za kiangazi.
– Kwa kuku wanaofugwa ndani hata kama unawapa majani kwa wingi hakikisha na vitamini za viwandani unawapa.
TIBA
Hapa wengi ndio huwa wanakosea. Unavyo wekeza pesa zako kwenye ufugaji kuku hakikisha unawekeza na muda wako pia.
Mfano kwa tatizo hili unapoambiwa utumie vitamini za dukani kwa ugonjwa huu na kama kuku ameathirika kwa kiwango kikubwa hataweza kupona kwa kutumia vitamini tu na ili ifanye kazi ni mpaka na wew ufanye kazi ya ziada.
Kwenye kutibu ugonjwa huu hauhitajiki uwe na uwoga au kinyaa.
VITU VYA KUANDAA
_Otc 20%
_Gloves
_ Vitamini zuri mfano amin total.
_ eye wound
_ Maji ya vugu vugu yenye chumvi kiasi.
JINSI YA KUFANYA
1. Vaa gloves chukua maji ya vuguvugu yenye chumvi kiasi. Msafishe kuku na maji hayo kwenye macho hakikisha unatoa uchafu wote uliondani ya macho. Baada ya kumsafisha na kuhakikisha uchafu wote umetoka chukua eye wound hii ni ya poda (unga unga).  Eye wound utaitumia kwa kuweka kwenye macho ya kuku huyo mgonjwa na uhakikisha unga unga huo wa eye wound unaingia vizuri kwenye macho.
2. Baada ya hapo chukua otc 20% ichanganye na vitamini kwenye maji wape kuku wote hata wale ambao bado hawajapatwa na ugonjwa.
Kuku wagonjwa ni vema uwatenge..
Utafanya zoezi hilo kwa siku 5 ila zoezi hili huwa ngumu siku ya kwanza uchafu unapo kuwa mwingi kwenye macho.
🙏🇹🇿✍

Leave a Reply