Utitiri na viroboto kwenye banda la mifugo

Viroboto na utitiri vinaweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa ya asili na dawa za viwandani.

Dawa za asili za kutokomeza utitiri katika banda la kuku

Imeandaliwa na John Nswima

Pengine umetumia dawa kadhaa za viwandani kwa ajili ya kupambana na viroboto na utitiri katika banda lako la kuku. Leo ninakueleza suluhisho rahisi ambalo si gharama.

 

UTITIRI

Umezoea kula kisamvu kwa ugali au wali. Kisamvu sio tu ni mboga pendwa, lakini pia ni dawa kiboko ya utitiri.

 

MAANDALI

Chuma kisamvu (majani yake) cha kutosha, kulingana na ukubwa wa banda lako.

Twanga kisamvu hadi kilainike kama kile cha mboga.

Kisha weka kwenye ndoo au chombo chochote kinachoweza kuhifadhi maji.

Kama una pump unashariwa kuchuja ili kuzuia kuziba, lkn haitafanya kazi vizuri ukichuja.

Kwa matokeo mazuri usichuje na changanya na maji.

Kiasi cha maji kiendane na uwingi wa kisamvu. Maji yakiwa mengi sana utapunguza nguvu ya dawa.

Chukua ndoo yako yenye mchanganyiko wa kisamvu na maji, ingia bandani ukiwa na ndoo mkono wa kuume na ufagio/au kwa mkono; kwa ajili ya kunyunyizia.

Nyuzia banda lote hadi ukutani.

Kama hali ilikuwa mbaya sana, fanya zoezi hili kwa siku tatu mfululizo. Itachukuwa miezi mingi Sana au miaka kusikia habari za utitiri bandani

  1. Hii pia inaondoa viroboto vilivyobandani sio vile vilivyo kwenye Kuku.

 

VIROBOTO

Kwa viroboto vilivyo kwenye Kuku, MAFUTA YA MAWESE yanafanya vizuri sana.

Hakikisha mawese hayajamaliza muda wake wa matumizi.

Wafungie kuku wote bandani. Kisha anza kushika mmoja mmoja na kumpaka maeneo yote yenye viroboto. Kwa kawaida mara moja tu inatosha.

 

Dawa za viwandani zinazoweza kutokomeza utitiri katika banda la kuku

Utitiri wa kuku wa machoni unaweza tokomezwa kwa kutumia dawa za unga kama akhery, sevin, ultravin, bakila nk hazimalizi. Tumia ectomin ya maji kuwamaliza kabisa. Unawapaka kwa kutumia pamba ya masikioni. Itakayobaki utachanganya na maji kwa uwiano wa 2 mls kwa lita moja ya maji.

 

Dawa za viwandani zinazoweza kutokomeza viroboto kwenye mifugo

 

  1. Viroboto kwenye mifugo vinaweza kutokomezwa kwa kutumia Imidacloprid (Ukipata confidor®) au dawa za kilimo zenye kiambata (active ingredient) kama itakuwemo (Imidacloprid). Ukipata hiyo imidacloprid changanya kwa uwiano wa 1:2 pulizia mnyama na mazingira HAPO HAUTAMUONA KIROBOTO TENA KWA KWA MIEZI SITA. Unaweza kuzipata Farmbase na wahindi kampuni ya POSITIVE wanayo inaitwa Septa 200®. Dawa nyingine nzuri unzaoweza kutumia kutokomeza viroboto ni pamoja na fiprofarm (off label). Hii ina fipronil ambayo ni active ingredient ya frontline.

 

  1. Anthelmintic (dawa ya minyoo) itategemea uko nchi gani ila kwa Tanzania ni Ivermectin Super (hii ina Ivermectin na Closurin. Pia unaweza kutumia Levamisole. Hizi zitahitaji mtaalamu wa kukusaidia kutibu kwa sababu ya dose na nyingine ukikosea dose utaua mfugo wako.

 

Leave a Reply