Kitabu cha ufugaji bora wa ng’ombe wa asili

Na Augustino Chengula

Wanyama kama alivyo binadamu wanapaswa kuishi wakiwa na afya njema wakifurahia uwepo wao kwa binadamu kama ilivyoukwa siku kabla ya kuwa mikoni mwa binadamu. Wanyama wenye afya njema watakuwa tayari kustahimili magonjwa na endapo wataugua basi watapona haraka zaidi. Mnyama mgonjwa humgharimu pesa nyingi sana mfugaji kwa kumwita daktari abaini ugonjwa, kununua dawa na sindano. Hivyo ni vema kuwakinga wanyama wako kwa kuwapatia matunzo yaliyo bora.

Matibabu pia huwa na manufaa kama yakifanyika mapema kabla ya mnyama hajazidiwa kiasi ambacho dawa haina msaada tena. Hii ina maanisha kwamba mfugaji lazima awe na uwezo wa kutambua haraka kuwa myama wake anasumbuliwa na ugonjwa au tatizo fulani na kutoa taarifa kwa mtaalamu pia kwa wakati. Pia kama kuna msaada wa haraka unahitajika kabla ya matibabu sahihi kuanza.

 

Unaweza kutunza afya ya wanyama wako kwa:

 1. Kuhakikisha kwamba wanapata chakula bora na cha kutosha wakati wote
 2. Kuhakikisha wanapata maji safi ya kunywa
 3. Kwa kufuata utaratibu sahihi wa chanjo dhidi ya magonjwa
 4. Kwa kuzuia kupe wanaoshambulia nje na ndani ya mwili
 5. Kwa kutenganisha wanyama wagonjwa na wazima ili magonjwa yasienea kwa wanyama wasio na ugonjwa
 6. Kwa kuhakikisha kuwa wanyama unaoingiza shambani mwako ni wale wasio na magonjwa
 7. Kwa kuepuka kuwachanganya mifugo wako na mifugo mingine kwenye malisho au kuchungia maeneo wanaochungia wafugaji wengine
 8. Kwa kuwatunza mifugo wako na hali mbaya ya hewa
 9. Kwa kutibu mifugo yako mara moja endapo itapata magonjwa
 10. La muhimu zaidi ni utunzaji wa kumbukumbu wa matukio katika shamba lako mfano matibabu na chanjo (tarehe, dawa au njano iliyotumika), uzalishaji n.k

 

Utajuaje kama wanyama wako ni wagonjwa?

 1. Wanyma wataonekana wakiwa dhaifu au wamedhoofu na watulivu
 2. Unaweza kuona dalili za wazi za magonjwa mfano kukohoa, kuharisha, kukonda, kupungukiwa damu,
 3. Hawali chakula au kunywa maji
 4. Uvimbe kwenye mwili wa mnyama
 5. Kutoka ute mdomoni na damu mwilini
 6. Kujitenga na wenzake au kushindwa kutembea
 7. Joto la mwili wake kupanda au kushuka sana
 8. Na dalili nyingine utakazoona si za kawaida

NB: Uonapo dalili hizi ni viashiria kuwa mnyama wako hana afya njema hivyo fanya haraka kubaini tatizo kwa kumuona daktari aliye karibun nawe

 

Myama mmoja akiwa mgonjwa anaweza kuwaambukiza wanyama wengine shambani mwako na kusababisha tatizo kuwa kubwa zaidi. Hivy ni vema kumtenga na wengine kama unahisi ugonjwa unaomsumbua unaweza kuenea kwa wengine.

 

Wakati mwingine unaweza kubaini kuwa shambani mwako kuna ugonjwa na jirani yako hali kadhalika kuna ugonjwa kama wako, hii inaonyesha kuwa hali ya ugonjwa kwenye eneo husika ni kubwa sana. Kupambana na ugonjwa aina hiyo unahitaji ushirikiano na wafugaji wote wa hilo eneo mkishirkiana na mtaalamu aliyepo eneo husika ku kabiliana nao.

 

EPUKA KUBABAISHA FUGA KIBISHARA KWA MAENDELEO YAKO

Leave a Reply