Na Mwandishi wetu Lukas Michael
Habari wafugaji leo ni siku nyingine tena, tukiendelea na masomo mbalimbali yanayohusu ufugaji wa kuku.
Kwa kawaida kulea vifaranga ni changamoto kwa wafugaji wengi, hivyo huamua kununua kuku wakiwa wakubwa. Endapo kuku wake wakitotoa vifaranga basi huwaachia kuku wawatunze vifaranga hao. Mfumo huu ni
(1) UTUNZAJI WA ASILI: Njia hii hutumika kwa vifaranga wachache ambao kuku jike (tetea) huachiwa kulea vifaranga wake. Wakati tetea anapo walea utagaji hukoma, hivyo huchukua muda mwingi huyo kuku kurudia kutaga.
Mfugaji kibiashara ni lazima ufuge kibiashara kwa mfumo wa
(2)KUWATUNZA VIFARANGA KWA KUTUMIA CHANZO CHA JOTO:
Mfumo huu wengi wanauona kuwa ni mgumu kutokana na kushindwa kuutumia na hatimaye vifaranga kufa.

HUU NI UTANGULIZI TU MFUGAJI KARIBU KATIKA SOMO HILI LA LEO
Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kulea vifaranga yameorodheshwa na kuelezewa kwa kina hapa chini.

BANDA BORA
Vifaranga hawahitaji eneo kubwa sana katika majuma manne ya kwanza. Nafasi inayohitajika kwa kukadiria ni meta 1 ya mraba kwa vifaranga 16. Kwa mfano nyumba yenye meta 10 za mraba inatosha kutunzia vifaranga 160 hadi wanapofikisha umri wa majuma manne. Vipimo vya nyumba yenye eneo kama hili inaweza kuwa na hatua 5 kwa 4. Utajenga banda kutegemea na eneo ulio nalo.

VYOMBO KATIKA NYUMBA YA KULELEA VIFARANGA

(1) KITALU/BROODER/BRUDA:
Bruda ya kukuzia vifaranga inatakiwa iwe ya mduara isiyopinda mahali popote, ni vizuri kutumia silingboard au mbao. Kwanini inatakiwa iwe ya mduara; tunafanya hivo kwa ajili ya kuzuia wasilundikane kwenye kona ndio maana mzunguko wa bruda unatakiwa kuwa ni mduara. Kwa maeneo ya kijijini bruda inaweza kutengenezwa kwa kutumia viroba vya magunia. Ndani ya bruda hiyo ndio kuna kuwa na chanzo cha joto, unaweza tumia jiko la mkaa, balbu, au chemli.
Katika banda la vifaranga ni muhimu kuwa na joto lisio kithiri hasa pale kwenye siku za mwanzo na nyakati za usiku. Mwanga na mzunguko wa hewa ndani ya bruda ni muhimu kwani huvutia na kuvishawishi vifaranga kuanza kula.
Weka madirisha makubwa yenye kuingiza hewa safi na kutoa ile chafu. Banda lisilo na hewa ya kutosha huchochea kuenea kwa magonjwa ya mfumo wa hewa. Andaa nafasi ya kutosha ili kuepuka vifaranga kurundikana.

UTATAMBUAJE KUWA JOTO LIMEZIDI AU LIMEPUNGUA.
(1) Kama joto linatosheleza utaona yafuatayo.
_Vifaranga vitalia kwa furaha
_Vitakimbia kimbia
_Vitakunywa maji
_ Vita chagua chagua na kuonesha shughuli nyingi

Zote ni dalili zuri za kuonesha kuwa joto linatosheleza
(2) Kama joto halitoshelezi utaona yafuatayo;
_Vifaranga wakiona baridi hujikusanya kalibu sana na chanzo cha joto.
_Au hujikusanya  wenyewe kwa pamoja na kulia kwa sauti.
Dalili hizi huonesha kuwa joto ni pungufu hivyo kuna ulazima wa kuongeza joto.
(3) Kama joto limezidi utaona yafuatayo
_ Vifaranga hukaa mbali na chanzo cha joto.
_Husinzia na kuzubaa
_ Kama ni kwenye chumba vifaranga hukimbilia mlango ili vipate upepo.
Katika hali hii ni dalili za kuonesha kuwa joto limezidi hivyo unatakiwa kupandisha taa juu, kupunguza vyanzo vya joto na kuwapa vifaranga maji mengi.

VYOMBO VYA KUWEKEA MAJI
Vifaranga wanahitaji maji na katika kuwapa maji hakikisha kuwa hayo maji ni safi.  Unaweza ukayachemsha kisha ukayachuja kama utakuwa na wasi wasi nayo.
Tukumbuke kuwa kuna magonjwa yanayo ambukiza kupitia yale maji wanayokunywa vifaranga wako hivyo kwa kuhakikisha usalama wa maji utakuwa umewanusuru vifaranga wako dhidi ya magonjwa hayo.
Unaweza kununua vyombo vya kuwekea maji (drinkers), lakini kwa vifaranga ni vema katika hayo maji yaliyomo kwenye drinkers ile sehemu ya kunywea uweke kokoto safi ndogo ndogo ili kuwafanya vifaranga wasilowe wakati watakapo kuwa wanakunywa maji. Kama hauna uwezo wakununua drinker basi unaweza ukatumia njia yeyote ya kutengeneza chombo cha kuwekea maji ila hakikisha kuwa hakivuji.
Hakikisha kuwa banda ni safi na kavu wakati wote ili kuzuia maladhi kwani  chanzo cha maambukizi hutokana na unyevunyevu pia.

VYOMBO VYA KUWEKEA CHAKULA
Wafugaji wengi hutumia feeders kuwalishia vifaranga wao chakula. Na wengine hutengeneza vyombo mfano wa feeders kwa kulishia vifaranga wao. Yote sawa ila cha muhimu ni kuzingatia usafi wa hivyo vyombo.
Kuna wengine huamua kuwamwagia vifaranga chini chakula mle mle wanapo lala. Hii ni hatari kubwa kwa vifaranga hao kuambukizana magonjwa kiurahisi. Kwani kinyesi cha kifaranga kinacho umwa kikichanganyika kwenye hiko chakula kisha akaja kifaranga mzima akala chakula hiko kuna uwezekano wa kuambukizwa ugonjwa kiurahisi sana. Hapo ndio utakuta mtu vifaranga wake wanaumwa kuhara damu (coccidiosis), amewapa dawa hawaponi. Atajiuliza kwanini hakuna cha kwanini hapo hiyo ni kwasababu banda lako, matunzo yako ni mabaya. Banda lako limekuwa banda la maambukizi wala sio uponyaji tena.

Sifa za banda bora
_Banda lenye kuingiza hewa safi na ya kutosha
_Banda lenye kuingiza mwanga wa kutosha
_Banda lenye kuzuia upepo mkali
_Banda lisio ruhusu maji kusimama na kuingia ndani na kwamba liwe imara.
_Banda liwe rahisi kusafisha
_Banda liwe na eneo la kutosha kulingana na idadi ya kuku.
_Banda liwe sehemu salama, kwa wezi na wadudu.

Ahsante

Tovuti ya UFUGAJI inawatakia ufugaji mwema na wenye mafanikio

 

Leave a Reply