Na Martin Mhina

 

Nigusie mbinu kadhaa za ufugaji bora wa kuku
 (a) Jinsi ya kutengeneza mchwa ili kupata protini ya ziada

 

Fuata hatua zifuatazo
1: Changanya kinyesi kikavu cha ngo’mbe na majni makavu / Mabua ya mahindi/Maranda ya mbao

2: Mwagia maji mpaka mchanganyiko ulowane

3: Pakia/Weka kwenye chungu au boxes kisha uelekeze sehemu yenye dalili ya mchwa au kwenye kichuguu

4: Funika kwa muda wa masaa 25 baada ya muda huwo mchwa watakuwepo wengi chukua box lako kamwage kwenye kuku husaidia sana katika ukuaji
(b) Kutengeneza minyoo ya chakula (red worms planning)

Red worms planning ni utaratibu wa kuzalisha minyoo kwa ajili ya kuku na Samaki, Zipo hybrid Red Worms ambazo mara nyingi hununua sample kutoka nje ya nchi Kama Kenya,China au hapa Tanzania fuata hatua zifuatazo kuzalisha Red worms asilia

1a) Chukua mavi ya ngombe mapya au ngombe aliyechinjwa mavi ya tumboni
b) Kusanya Damu damu, ngozi, utumbo, magoroto, nyamanyama nk

2. Pakia kwenye kiloba au gunia kati ya chaguo A au B hapo juu

3: Chimba shimo la wastani kisha mwagia maji ndoo kubwa 4

4: Fukia hilo gunia na mwaga maji ndo 2 mara 1/2 kwa siku kwa muda wa siku  8/12

5: Baada Ya siku hizo kupita fukua na chepe utakuta minyoo mitupu ya kutosha kwa ajili ya chakula cha kuku au samaki na siku zinavyozidi kwenda ndo wanazidi kuzaliana na kuwa wakubwa

(c) Ufanisi wa ufugaji wa kuku bora hutegemeana na mambo yafuatayo

1: Ujenzi wa banda bora kwa kuzingatia vipimo sahihi

2: Uchaguzi Wa kuku wazaz wenye sifa nzuri

3: Udhibiti na tiba za magonjwa mbalimbali kwa kuzingatia Ratiba sahihi za chanjo

4: Ulishaji bora kwa waakati na chakula kiwe na viini lishe vyote

5: Uzingatiaji wa usafi wa banda na vyombo

  (d) Sifa za banda bora la kuku

1: Liingize mwanga na hewa muda wote

2: Liwe kavu daima

3: Liwe na nafasi ya kutosha kuanzia vipimo vya upana 3M na urefu 4/5M kuku wasibanane

4: Liwe la gharama nafuu lakini la kudumu unaweza ukatumia mabanzi, mbao, mianzi, matofali katika ukuta na paa tumia vigae, bati na nyasi

5: Liielekeze kuzuia upepo na mvua pia kuzuia wanyama na wadudu hatari kwa kuku

6: Liwe na nafasi ya kuweka vyombo vya chakula na ndani kuwe na maranda, bembea, vichanja

7: Kuwe na uzio mpana angalau mita 10*12 ili wapate mahala paa kuota joto

 (e) Ili kuepuka vifo vya kuku fanya yafuatayo

1: Osha banda na vyombo kwa dawa kama V-RID kila baada ya miezi 3/6 ili kuua bacteria nk

2: Chanja kuku chanjo zifuatzo Mahepe (Mareks ) kuanzia siku Ya 1-3 ,Mdondo siku 3-7 utarudia siku Ya 21,Gumboro siku 14 na Ndui siku ya 28

NOTE chanjo ya kideri utarudia kila baada ya miezi 3

3: Wape Vitamin kama Multivitamin, vitalstress au maji ya molasses ya unga

4: Usafi wa banda ni muhimu epuka watu kuingia bandani ukiweza kuwe na mavazi maalumu kama Ovaloli, magamu buti zitakazo fuliwa kwa dawa maalumu kwa ajili ya mfanyakazi na wageni wanaotembelea

5: EPUKA MAADUI HAWA HATARI KWA MIFUGO KAMA NYOKA, KENGE, PAKA, PANYA, MMBWA, KICHECHE NK KWA KUTUMIA MBINU ZIFUATAZO

1: Mwaga mafuta ya Dizel pamoja na mchanga zunguushia pembeni ya banda nyoka na kenge hatosogea

2: Chemsha mayai kisha yatege mahali kuanzia mbwa, paka, nyoka, kenge, kicheche, akimeza lazima afe maana yai halitavunjika

3: Chimba shimo refu kidogo pembeni ya kibanda au katikati kisha weka pumba, panya, mende, paka wamedumbukia ukiongeza na dagaa kidogo

4: ZUNGUUSHIA UA WA MTI WA NYOKA (Mnyonga pembe ) KAMA UZIO WA BANDA AU SHAMBA LA MIFUGO PEMBENI KWENYE MIPAKA, Mti huu harufu yake hufukuza na kudhibiti KENGE NA NYOKA hata mwizi akitaka kuiba huwa na mashaka ya kukamatwa.

Pia mti huu majani yake /magome yake yakipondwa husaidia kuponya mtu aliyengatwa/kutemewa mate na nyoka. Aidha husaidia kuku aliye dumaa au mwenye minyoo kumboosti. Mti huu hupandwa kama muhogo na unapatikana Tanga kwa wingi.
JINSI YA KULISHA NA KUTUNZA KUKU WA NYAMA  (BROILERS)

Hapa nchini kwetu Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni watu wamejikita katika biashara ya Mifugo hasa ufugaji wa kuku wa kigeni na leo hebu tuangalie lishe ya kuku wa nyama (Broilers).
Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri

a) Viinilisha vya wanga 60-65%
b) Protini 30-35%
c) Madini 2-8%

Pamoja na maji safi yenye mchanganyiko wa dawa ya vitamin.

Chakula cha vifaranga

Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hutakiwa kuwa katika punje punje ndogo ndogo. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.

Aina ya vyakula Kiasi (kgs).

Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40

Pumba za mtama au mahindi au uwele 27

Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20

Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25

Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10

Chumvi ya jikoni 0.5

Virutubisho (Broiler premix) 0.25

JUMLA = 100kgs.
Chakula cha kukuzia – growers mash.

Aina ya vyakula Kiasi (kgs).

Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25

Pumba za mtama au mahindi au uwele 44

Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17

Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 3.25

Dagaa au mabaki ya samaki (fish meal) 10

Chumvi ya jikoni 0.25

Virutubisho (Broiler premix) 0.5.

JUMLA = 100Kgs.
Chakula cha kumalizia kukuzia (Growers finishers).

Aina ya vyakula Kiasi (kgs).

Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 31

Pumba za mtama au mahindi au uwele 38

Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 18

Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25

Dagaa au mabaki ya samaki (fish meal) 13

Chumvi ya jikoni 0.5

Virutubisho (Broiler premix) 0.25.

JUMLA = 100Kgs.
UTAMBUZI WA MAGONJWA YA KUKU KUPITIA RANGI YA KINYESI

1. MUHARO MWEUPE (pullorum bacilary diarrhoea) ugonjwa huu huathiri zaidi vifaranga kabla ya wiki nne huharisha mharo mweupe,

TIBA kuu ni usafi pekee kwenye banda na kuepusha maji yasimwagike ovyo.

2. KIPINDUPINDU CHA KUKU (fowl cholera) kinyesi cha kuku ni njano tumia dawa za salfa, eg Esb3 au amprollium

3. COCCIDIOSIS
Mwanzo kinyesi cha kijivu na baadae huharisha damu iliyochanganyika
Tumia dawa ya VITACOX au ANTICOX

4. MDONDO(Newcastle)

Kuku hunya kinyesi cha kijani lakini sio kila kijani ni newcastle. Dalili zingine ni pamoja na mabawa ya kuku kutanuka anakuwa kama amevaa koti. Ugonjwa huu hauna TIBA, zingatia ratiba ya chanjo tuu.

5. TYPHOID
Kinyesi cheupe
kinagandia sehemu za nyuma au hulowana sehemu za haja
dawa ni Esb3.

6. GUMBORO
Huathiri zaidi vifaranga
kinyesi huwa ni majimaji mepesi. Hauna Dawa.
tumia vitamini na antibiotic.

Kalenda ya chanjo kama ifuatavyo.

1week- Marek’s vaccine

2week- Newcastle Gumbolobbbbbg’vg

3week- Gumbolo vaccine

4week- Gumbolo vaccine tena
PUMZISHA CHANJO THEN ENDELEA IKIFIKA WIKI YA NANE

8week-Fowl pox vaccine

9week-Newcastle vaccine
PUMZIKA TENA MPAKA WIKI YA KUMI NA NAME

18week- Fowl typhoid vaccine

BAADA YA KUMALIZA CHANJO HIZI endelea kumpa chanjo ya Newcastle vaccine kila baada ya miezi mitatu au minne na kuzingatia hasa usafi wa banda na mazingira yanayozunguka.
ULISHAJI WA KUKU WA MAYAI (LAYERS)
Kuku wa mayai ili watage vizuri wanatakiwa walishwe chakula bora kwa utaratibu unaotakiwa, ukiwazidishia au kuwaongezea hawatotaga vizuri. Wanatakiwa walishwe kati na kati kulingana na umri kama ifuatavyo:-

UMRI WA WIKI 1 -2
Katika umri huu wanapewa chakula aina ya “Super Starter” kwa ajili ya kuwatengenezea kinga mbadala ili waweze kuhimili mikiki mikiki ya vijidudu vya magonjwa kadri wanavyoendelea kukua, wanapewa chakula hicho kwa kiwango maalum kama ifuatavyo:-
Wiki ya 1: Gramu 12 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 2: Gramu 22 kwa kuku mmoja kwa siku moja

UMRI WA WIKI 3 – 8
Hapa wanakuwa bado ni vifaranga na wanapewa chakula aina ya “Chick Starter” kwa ajili ya kuendelea kuwajenga miili yao waweze kupoekea virutubisho vizuri, hii inatokana na kwamba kuna baadhi ya viinilishe vinafanya kazi ya kumeng’enya chakula na kupatikana viinilishe vingine, kwahiyo vikikosekana katika mwili wa kuku basi hata wale chakula gani bora, hawawezi kutoa mazao bora, lakini kwa kuwapa “Chick Starter” itawapelekea kuwa na virutubisho hivyo muhimu. Kiwango na ulishaji wake ni kama ifuatavyo:-
Wiki ya 3: Gram 27 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 4: Gram 32 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 5: Gram 38 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 6: Gram 42 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 7: Gram 46 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 8: Gram 50 kwa kuku mmoja kwa siku moja

UMRI WA WIKI 9 – 18
Katika umri huu kuku wanapewa chakula aina ya “Grower Mash” kwa ajili ya kuwakuza na kuwajenga mfumo wa uzazi kwa maandalizi ya utagaji. Kiwango cha chakula kinategemea na wiki kama ifuatavyo:-
Wiki ya   9: Gram 56 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 10: Gram 62 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 11: Gram 64 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 12: Gram 66 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 13: Gram 68 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 14: Gram 74 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 15: Gram 74 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 16: Gram 80 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 17: Gram 82 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 18: Gram 88 kwa kuku mmoja kwa siku moja

UMRI WA WIKI 19 – 40
Huu ni umri ambao kuku wanataga kwa kiwango kikubwa sana (85% hadi 100%) hali ambayo inawafanya kutumia nguvu nyingi mno, hivyo hupewa chakula aina ya “Layers Phase 1” kwa ajili ya kufidia nguvu ya ziada wanayotumia ili waendelee kutaga kwa kiwango hichohicho. Ulishaji wake ni kama ifuatavyo:-
Wiki ya 19: Gram 92 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 20: Gram 102 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 21: Gram 108 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 22: Gram 114 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 23: Gram 116 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 24: Gram 120 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 25 – 40: Gram 130  kwa kuku mmoja kwa siku moja

UMRI WA WIKI 41 – 80
Katika umri huu kuku wanakuwa wameanza kuchoka na huanza kutaga kwa kiwango cha kawaida (65% hadi 75%) hivyo hupewa chakula aina ya “Layers Phase 2” kwa ajili kuendeleza (maintain) kiwango chao hicho kwa muda mrefu. Kiwango chao ni “Gram 130 kwa kuku mmoja kwa siku moja”.

NB: Kuanzia wiki 81 na kuendelea unaweza kuwauza na kuweka kuku WENGINE.

 

Leave a Reply