Kwa nini ufuge kuku?
Kuku hufugwa kwa sababu mbalimbali za kiuchumi, lishe na kitamaduni. Ufugaji wa kuku unatoa chanzo rahisi na cha bei nafuu cha protini, fursa ya kujiajiri, na uwezo wa kujitegemea katika upatikanaji wa chakula. Ufugaji wa kuku ni maarufu kwa sababu zifuatazo:
- Mtaji wa kuanzia ni mdogo ukilinganisha na mifugo mingine.
- Hukua haraka – hasa broiler, hivyo kupata faida ndani ya muda mfupi.
- Soko la uhakika – nyama ya kuku na mayai hutumika kila siku.
- Mzunguko mfupi wa uzalishaji – mayai hutoka kila siku, broiler hukomaa ndani ya wiki 6–8.
- Chakula kuhitajika kidogo ukilinganisha na faida yake.
- Inaweza kufugwa maeneo mengi: mijini na vijijini.
- Tofauti ya bidhaa – kuku wa nyama, mayai, vifaranga, mbolea n.k.
- Hatari ndogo ukifuata chanjo na usafi.
1. Ufugaji wa Kuku wa Nyama (Broiler)
Lengo kuu: Uzalishaji wa nyama ya kuku ndani ya muda mfupi
Sifa kuu
Hukomaa ndani ya wiki 5–7.
Huhitaji chakula cha protini nyingi (starter, grower, finisher).
Wanahitaji mazingira safi, joto la kudhibitiwa, na nafasi ya kutosha.
Hawafai kutumiwa kama kuku wa kutaga mayai.
Mahitaji: Udhibiti mkali wa joto, usafi, lishe bora na usafi
Faida: Mzunguko wa haraka wa uwekezaji na mapato, mahitaji makubwa ya soko (migahawa, hoteli, na mama nitilie, na nyama choma) na kufanya mtaji urudi haraka.
- Changamoto: Wanakufa haraka bila chanjo/usalama mzuri na gharama ya chakula inaweza kuwa kubwa.
2. Ufugaji wa Kuku wa Mayai (Layers)
Lengo kuu: Uzalishaji wa mayai ya kula na ya biashara kwa muda mrefu.
Sifa: Hukua kwa kiwango cha wastani, huwa na uwezo wa kutaga mayai mengi (hadi 300 kwa mwaka)
Hutaga kuanzia wiki 18–20.
Hutaga kwa muda wa miezi 12–18 mfululizo.
Huitaji mwanga wa kutosha (masaa 14–16 ya mwanga).
Aina za chakula: chick mash, growers mash, layers mash.
Mahitaji: Taa za ziada, lishe yenye kalsiamu, mifumo maalum ya kutagia mayai
Faida: Mapato ya kila siku kutokana na mauzo ya mayai, mzunguko mrefu wa uzalishaji
- Changamoto: Gharama za chakula ni kubwa na inahitaji chanjo kamili na ratiba ya taa.
3. Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
Lengo kuu: Uzalishaji wa nyama na mayai kwa njia ya asili zaidi na wenye gharama ndogo.
Sifa: Huwa na mwili mdogo
Wanastahimili magonjwa.
Wana uwezo mkubwa wa kutafuta chakula wenyewe na hula chakula cha kawaida (vumbi, majani, mabaki ya jikoni) lakini uzalishaji mdogo.
Hutaga mayai machache (60–150 kwa mwaka).
Wanapendwa sana sokoni kwa sababu ya ubora wa nyama.
Mahitaji: Eneo la kuruka, lishe ya asili zaidi, udhibiti mdogo wa mazingira
Faida
Gharama ya uendeshaji ni ndogo (matumizi madogo ya dawa na chakula)
Bei nzuri kwenye soko na soko la uhakika/kudumu, hasa nyama ya kienyeji.
Hatari ya vifo ni ndogo ukilinganisha na kuku wa nyama (broiler).
Changamoto
Uzalishaji mdogo kama hautatumia lishe bora.
Kuku hukua taratibu kuliko kuku wa nyama (broiler).
4. Faida za Jumla za Ufugaji wa Kuku
Chanzo cha protini bora na ya bei nafuu
Fursa ya kujiajiri na kuleta mapato
Mchango katika uchumi wa kaya na taifa
Urahisi wa kuanzia (unaweza kuanza na idadi ndogo)
Uzalishaji wa mbolea ya asili kwa kilimo
3. Changamoto za jumla
Uwezekano wa magonjwa
Uhitaji wa ujuzi wa msingi
Mabadiliko ya bei za pembejeo (hasa chakula cha kuku)
Ushindani katika soko
Ufugaji wa kuku unaweza kuwa shughuli yenye tija ikiwa itafanyika kwa utaalamu na uangalifu. Kuchagua aina sahihi kulingana na malengo, uwezo wa uwekezaji na soko linakuwa muhimu kwa mafanikio ya mfugaji.

