Ufugaji wa kuku tangu vifaranga

ByChengula

Sep 26, 2015

ULEAJI BORA WA VIFARANGA

Mambo mengi yanayohusika katika uleaji wa vifaranga kwa upande wa HARSHO FEEDS tupo tayari kumhudumia mfugaji wa kuku kwa kumpatia chakula na utaalamu sahihi. Katika uleaji wa vifaranga kuna tofuati kati ya vifaranga wa nyama na wale wa mayai hasa katika chanjo na lishe.

 

MATAYARISHO

Banda la kuku liwe imara kuepuka wizi, panya, ndege, nyoka na kadhalika. Jenga sehemu yenye hewa ya kutosha, kavu na mbali na kuku wengi.

Kabla ya kuingiza kuku, safisha banda lote nje na ndani kwa dawa ya kuangamiza wadudu. Paka chokaa kwenye kuta zote. Hakikisha banda haliwi na joto kali, baridi, kuingiwa na mvua, jua au upepo.

Tayarisha chakula bora, maji safi, madawa-vifaa vya kutosha na tandiko safi.

 

KABLA YA KUFIKA VIFARANGA

Banda la kuku liwe tupu wiki moja hadi mbili baada ya kusafishwa na dawa. Vifaranga utakaopokea wawe na historia nzuri.

a)   Usichanganye vifaranga wa sehemu tofauti

b )  Tengeneza mduara ndani ya banda kwa kutumia hardboards kwa urefu wa sentimeta 50 na katikati yake weka taa ya (balbu) au jiko la mkaa, hakikisha mwanga wa kutosha ili vifaranga waone chakula na maji.

c)  Weak tandiko la kuku (litter) safi, vifaa vya maji na chakula kulingana na idadi ya vifaranga.

d)   Masaa matano kabla ya vifaranga hawajafika washa taa za joto au jiko la mkaa kwa ajili ya kutoa joto kwa vifaranga (35oc) weak maji ndani ya vyombo ili yawe na joto kiasi. Hakikisha kuna hewa ya kutosha na hakuna upepo unaoingia.

e)   Iwapo vifaranga vinatoka mbali na vimechoka, weka glucose/sukari kidogo kwenye maji (kijiko cha chakula kwa lita tano za maji)

 

KUPOKEA VIFARANGA

Watoe vifaranga kwenye maboksi na kuwaingiza ndani ya mduara, hakikisha unayo hesabu kamili.

Vifaranga wote wanywe maji na uwanyweshe ambao hawajakunywa maji. Baada ya masaa mawili, weka chakula kwenye vyombo vya chakula.

Hakikisha kuna mwanga masaa 24 kwa siku tano za mwanzo na joto la kutosha.

Hakikisha kuku wana nafasi ya kutosha. Panua duara la kuelekea kadri kuku wanavyokuwa na ondoa duara baada ya wiki tatu. Kuku wakibanana hawakui vizuri kwa kipindi hiki.

 

ULEAJI KUKU MAYAI (Layers)

Kila kuku anayetaga apate eneo la futi mbili (2) za mraba. Nyumba iwe na madirisha ya kutosha kuweza kuingiza hewa safi. Tumia kati ya vitu vifuatavyo kwenye sakafu kama godoro (litter):-

a)  Maranda ya mbao

b)  Maganda ya mpunga

c) Majani makavu yaliyokatwakatwa

 

VIFAA

Weka vifaa vya kutosha kulishia chakula na maji kwenye banda lako kama ifuatavyo.

Sinia moja litumike kulishia vifaranga 50. Vifaa vya maji tumia

Chick Fount moja kwa vifaranga 100.

Kuku wakubwa tumia “Feeder” moja kwa kuku 50 na drinker moja kwa kuku 60

 

CHAKULA KINACHOTAKIWA

Umri (wiki)Aina ya chakula
0-4Chick Starter
5-8Chick Mash
9-20Growers Mash
21-89Layers Mash

 

UMRI

(wiki)

CHAKULA

(Grams)

MAJI (ml)WASTANI

WA UZITO (grams)

1121320-3050
2192040-50100
3252550-50150
4302960-70200
5353370-80300
6403780-100400
74541100-120500
85046120-130650
95451130-140800
106056150-160900
116761160-1651000
126566165-1701100
136873170-1751200
147177175-1801300
157475180-1901400
167677190-1951500
177880195-2001600
18808620-2101700
198395210-2201750
2086100220

 

Katika kilele cha utagaji kuku mmoja anahitaji gram 120-135 kila siku hii ni sawa na kilo 12 – 12/siku/kuku/100. kiasi hiki kinategemea ubora na lishe ya kuku unachotumia.

 

MPANGO WA KUBADILI CHAKULA

Unapobadili chakula usibadili ghafla. Badili chakula kutoka Chick Starter hadi Growers Mash na Growers Mash hadi Layers Mash kwa mpangilio ufuatao.

½ Chick Starter + ½ Growers Mash changanya vizuri na lisha kwa wiki moja. Kisha endelea na Growers Mash fuata utaratibu huo utakapobadili Growers kwenda Layers

 

UMRI (siku/wiki)Aina ya chanjoNjia ya kuwapa
Siku 1MarkersSindano Hatchery
Siku 7New Castle-lasotaMaji ya kunywa
Siku 14GumboroMaji ya kunywa
Siku 21GumboroMaji ya kunywa
Wiki 8 – 10New CastleMaji ya kunywa

 

 

MPANGO WA KINGA – KUKU WA MAYAI

CHAKULA KINACHOHITAJIKA Umri (Wiki)            

 

 Aina ya chakula

0-3                           Broiler Starter

4-8                           Broiler Finisher

UMRI (wiki)CHAKULA (grams)MAJI (ml)WASTANI WA UZITO (grams)
12040-50130-150
23060-80260-300
350100-120460-520
470140-160750-800
590180-2001000-1200
6105210-2301300-1500
7115230-2801600-1800
8120240-3001900-2100

 

 

Rudia chanjo ya New Castle kila baada ya miezi 3-4, chanjo ya Mareks hufanyika Hatchery kabla ya mfugaji kupewa vifaranga.

 

SIFA ZA KUKU BORA WA MAYAI

Kuku waliotunzwa vizuri tegemea yafuatayo:-

ª   Vifo wakati wa kulea 3% – 5%

ª   Vifo wakati wa utagaji 1% kwa mwezi

ª   Umri wa kuanza kutaga wiki 19-20

 

TIBA YA MINYOO

Hii hufanyika kwenye kuku wa mayai:

Mara ya kwanza wapewe wiki ya 8 kurudiwa ya 18

Baada ya wiki 18 wasipewe tena na dawa ya minyoo hadi baada ya kupitia kiwango cha juu cha utagaji (peak production)

Baada ya Peak Production kuku wapewe dawa ya minyoo kila baada ya wiki 8-10 au minyoo inapoonekana kwenye kinyesi

 

KUKU WA NYAMA (BROILERS)

Kila kuku wa nyama anapaswa apate eneo la futi moja (1) ya mraba. Nyumba iwe na madirisha ya kutosha, hewa safi, sakafu iwe na godoro (litter) ya randa au maganda ya mpunga.

 

VIFAA

Vifaranga 100 wanaweza kutumia chombo kimoja cha kulishia

(chick plate) na chombo kimoja cha kunywea maji (chick fount) kwa wiki moja kuanzia wiki ya pili na kuendelea tumia chombo kimoja cha kulishia (feeder) chenye kipenyo cha sentimenta 38 kwa kuku 50 .

 

 

MPANGO WA KINGA – KUKU WA NYAMA

UMRI (siku/wiki)AINA YA CHANJONJIA YA KUWAPA
Siku 7New CastleMaji ya kunywa
Siku 14GumboroMaji ya kunywa
Siku 21GumboroMaji ya kunywa

 

Muhimu Zingatia

Fuata ratiba ya chanjo kama ilivyopendekezwa

Pata chanjo toka sehemu inayojulikana na yenye uhakika wa upatikanaji

Hifadhi chanjo yako kwenye fridge na sio freezer sehemu yenye nyuzijoto 4 – 8 centigrade.

Chanjo isitolewe zaidi ya saa 4.30 asubuhi kwa sababu chanjo inaweza kuharibika kutokana na joto au mwanga mkali wa jua.

 

Unapoona dalili za ugonjwa, kama kusinzia, kujikunyata, kuharisha, kutokula chakula, kutokunywa maji, kuhema kwa tabu au vifo, toa taarifa haraka kwa mtaalamu wa mifugo ili upate ushauri na huduma mara moja.

 

Jarida hili limetayarishwa na HARSHO TRADING CO. LTD

Head Office: Kawawa street. Moshi. Branch: Along Moshi Arusha Rd. Bomang’ombe P.O. BOX 810.

Moshi, Tanzania

Tel: 0784 287409 / 027 2753503

Fax: +255 27 2753505

E-mail: harshotrad@yahoo.com

Website:- www.harshotz.com

Leave a Reply