Kiasi gani cha chakula ulishe kuku wako kwa siku?

ByChengula

Oct 5, 2024

Kiasi cha chakula kwa kuku mmjoja wa nyama kwa siku

Kwa kuku mmoja wa nyama (broiler au Sasso na Kroiler kama wa nyama), kiasi cha chakula wanachohitaji kwa siku hutegemea umri wao. Hapa ni kwa kuku mmoja, hivyo utazidisha na idadi ya kuku ulionao ili kupata kiasi gani utawapa kuku wako kwa siku.

  1. Wiki ya 1 hadi ya 2: Kuku mmoja anakula takriban gramu 20 hadi 50 za chakula kwa siku.
  2. Wiki ya 3 hadi ya 4: Kiasi huongezeka hadi gramu 60 hadi 100 kwa siku.
  3. Wiki ya 5 hadi ya 6: Kuku mmoja hula takriban gramu 120 hadi 150 za chakula kila siku.
  4. Wiki ya 7 hadi kuendelea: Hapa, kuku wa nyama hula gramu 160 hadi 200 kwa siku.

 

Kiasi cha chakula kwa kuku mmjoja wa nyama kwa siku tangu vifaranga

Kiasi cha chakula kwa kuku mmoja wa mayai tangu anapokuwa kifaranga kinabadilika kadri kuku anavyokua. Hapa kuna mwongozo wa kiasi cha chakula kinachohitajika katika hatua mbalimbali za ukuaji wa kuku wa mayai.

  1. Vifaranga (siku ya 1 hadi wiki ya 8)
    • Kipimo: Gramu 30-50 kwa siku kwa kifaranga mmoja.
    • Chakula kinachotumika: “Chick starter” ambacho kina protini ya juu (18-20%) kusaidia ukuaji wa haraka.
  2. Kuku Wanaokua (wiki ya 8 hadi wiki ya 20)
    • Kipimo: Gramu 50-100 kwa siku kwa kuku mmoja.
    • Chakula kinachotumika: “Grower feed” ambayo ina protini ya wastani (16-18%).
  3. Kuku wa mayai (zaidi ya wiki 20, kuanza kutaga mayai)
    • Kipimo: Gramu 120-130 kwa siku kwa kuku mmoja.
    • Chakula kinachotumika: “Layer feed” yenye protini (16-18%) na virutubisho vya ziada kama kalsiamu kwa ajili ya mayai yenye ganda imara.

Ni muhimu pia kuhakikisha wanapata maji safi kila wakati na kuongeza madini muhimu kama vile calcium na phosphorus mara wanapoanza kutaga mayai.

Kwa ujumla, hakikisha kuwa chakula kina virutubishi vyote muhimu kama protini, wanga, mafuta, madini na vitamini ili kuhakikisha ukuaji wa haraka na afya bora.

Leave a Reply