Aina, njia za ufugaji na uchaguzi wa nguruwe bora

Aina, njia za ufugaji na uchaguzi wa nguruwe boraNguruweAina, njia za ufugaji na uchaguzi wa nguruwe bora

Utangulizi
Nchini Tanzania ufugaji wa nguruwe unazidi kuongezeka siku hadi siku. Hii ni kwa sababu, nguruwe ni moja kati ya mifugo inayompatia kipato mfugaji kwa haraka, kwani huzaa mara mbili kwa mwaka na kila mzao anaweza kuzaa watoto 12. Licha ya kuzaa mara mbili, mnyama huyu hukua na kuongezeka uzito baraka. Kwa siku huweza kuongezeka uzito wa gramu 500 hadi 700 na hivyo kufikia uzito wa kuchinjwa (kilo 60 hadi 90) mapema, kati ya miezi sita hadi nane kama atatunzwa vizuri.
Vile vile gharama za kufuga nguruwe ni ndogo ukilinganisha na gharama za kuwafuga wanyama wa aina nyingine kwani nguruwe anaweza kula mabaki ya vyakula kutoka mashuleni, mahotelini, majumbani na mahospitalini. Halikadhalika huweza kula mboga na matunda ambayo yameharibikabustanini kamavilenyanya, mapapai, kabichi na maboga.
Nguruwe hufugwa kwa ajili ya nyama, mafuta na mbolea. Hatahivyo wafugaji wengi hufuga ngumwe bila kuzingatia kanuni za ufugaji bora ambazo ni pamoja na uchaguzi wa njia za ufugaji na utunzaji bora wa ngumwe, dume, jike na watoto. Ili ngumwe aweze kutoa mazao mengi na bora anatakiwa kulishwa chakula bora na kilichochanganywa vizuri, kufugwa kwenye nyumba bora, pia kumkinga na kumtibu dhidi ya magonjwa na matatizo mbali mbali. Vile vile, ubora wa mazao ya ngumwe unategemea kwa kiasi kikubwa utayarishaji wa mazao kabla ya kuuza. Ubora wa nyama unaweza kuharibika endapo taratibu za utayarishaji na hifadhi bora ya mazao hazitafuatwa. Aidha mfugaji anatakiwa kuzingatia uwekaji wa kumbukumbu.
Kitabu hiki kimetayarishwa ili kumsaidia mkulima kufuga nguruwe kitaalam. Endapo maelezo yaliyomo katika kitabu hiki yatazingatiwa wafugaji watapata mazao mengi nabora nahivyo kuwaongezeapato na kuweza kuboresha afya za familia zao na hatimaye Taifa zima.
Njia za Ufugaji
Kuna njia kuu tatu za kufuga nguruwe nazo ni:

 

  • Ufugaji huria

– Nguruwe huachwa wajitafutie chakula wenyewe.
– Hupewa hifadhi wakati wa usiku.
Faida:
– Hainagharamakubwakwamfugaji.
– Huweza kujipatia madini hasa ya chuma kwa urahisi.
– Hurutubishaudongokwakinyesinamkojowake.
Hasara:
– Ni rahisi kuibiwa au kuliwa na wanyama wakali.
– Huharibu mazao shambani na mazingira.
– Hupata magonjwa na minyoo kwa urahisi na huweza kusambaza kwabinadamu.
– Huzaliana bila mpango.
– Huhitaji eneo kubwa.

 

  • Ufugaji wa Ndani na Nje

– Ngumwe hufungiwa ndani ya uzio ambapo kuna banda maalumu.
Hupewa chakula na maji na ana uhum wa kuingia na kutoka ndani ya banda.
Faida:
– Si rahisi kuambukizwa magonjwa kutoka nje ya uzio.
– Njia hii inapunguza upotevu, wizi na kushambuliwa na wanyamawakali.
– Mazao yake ni mengi kuliko ya njia ya huria.
– Ni rahisi kuwahudumia kwa chakula na magonjwa.
– Ukusanyaji wa mbolea ni rahisi.
Hasara:-
– Gharama kubwa kuliko zaufugaji huria.
– Ni rahisi kuambukizana magonjwa na minyoo.
– Huhitaji eneo kubwa.
– Mfugaji analazimika kumpatia chakula na maji.

 

  • Ufugaji wa Ndani

Nguruwe hujengewa banda ambalo hugawanywa kufuatana na makundi; kwa mfano ngumwe dume, jike na vitoto. Katika ufugaji huu nguruwe hupewa chakula na maji ndani ya banda.
Faida:
– Ni rahisi kuwahudumia kwa chakula, kinga na tiba
– Ni rahisi kuthibiti magonjwa, minyoo na wadudu wengine.
– Ni rahisi kusimamia uzalishaji wa aina unayoitaka kwa wakati unaotakiwa.
– Hutoa mazao mapema, mengi na bora.
– Hawadhuriki na wanyama wakali na si rahisi kuibiwa
– Huhitaji eneo dogo.
Hasara:
– Huhitaji mtaji mkubwa
– Huhitaji uangalizi wa karibu na wa kitaalam
– Huweza kuambukizana magonjwa.
Aina za Ufugaji wa Nguruwe
Kuna aina nne za ufugaji ambazo mfugaji anaweza kuchagua ili kuongeza mapato yake.
(i) Nguruwe waliotenganishwa na mama yao baada ya kutimiza miezi miwili.
Mfugaji anahitaji kuwa na majike kwa ajili ya uzalishaji.
(ii) Kununua ngumwe waliotenganishwa na mama yao na kuwatunza kwa ajili ya nyama na mafuta.
(iii) Kukuzajike na dume na kutunza watoto mpaka wanapofikia umri wa kuuzwa kwa ajili ya nyama.
(iv) Ufugaji kwa ajili ya kuzalisha mbegu bora. Njiahhni ngumu ina gharama kubwa, na inahitaji utaalam zaidi.
Sifa za Nguruwe Bora
Dume:
– Asichaguliwe kutoka kwenye ukoo wenye historia ya magonjwa au kilema cha kurithi.
– Awe na miguu imara, mchangamfu na mwenye afya bora.
– Awe na umbile zuri na misuli imara itakayomuwezesha kupanda bila matatizo.
– Awe mwenye kende zilizokamilika.
– Awe anayekua haraka na mwenye uwezo mkubwa wa kubadili chakula kwa matumizi ya mwili kuwa nyama.
Jike:
– Awe na umbile la kumuwezesha kubeba mimba na kuzaa kwa urahisi.
– Awe na chuchu zisizopungua 12 na ziwe zimejipanga vizuri.
Aina Za Nguruwe
Kuna aina nyingi za nguruwe wafugwao, zifuatazo ni baadhi ya aina zinazofugwa hapa nchini.
Nguruwe Mkubwa Mweupe
– Ni mweupe, masikio yake yamesimama na paji la uso limeingia ndani kama bakuli.
– Si rahisi kushambuliwa na magonjwa.
– Wenye umri mdogo, nyama yake haina mafuta mengi.
– Hukua na kuongezeka uzito kwa haraka sana.
– Jike hutoa maziwa mengi
– Dume hutumika kwa ajili ya kuboresha aina nyingine za nguruwe.

 

Nguruwe Mrefu Mweupe (Landrace)

– Huyu ni mrefu mweupe na mwembamba kuliko yule mkubwa mweupe.
– Masikio yake yameinama kwa mbele.
– Haongezeki uzito upesi na hutoa nyama isiyo na mafuta mengi.
– Aina hii ikipandishwa na aina ya kwanza huzaa nguruwe anayetoa mnofu mzuri zaidi usiokuwa na mafuta mengi.
– Ni mfupi, mweusi na ana mstari mweupe kuzunguka mwili kwenye miguu ya mbele.

Nguruwe Mfupi Mweusi, mwenye mstari mweupe kuzunguka mwili kwenye miguu ya mbele (Wessex Saddleback)
– Masikio yameinama.
– Mgongo umepinda kidogo mfano wa upinde.
– Hutoa mafuta mengi sana.
– Hutoa maziwa mengi, huzaa watoto wengi na kuwatunza vizuri.
– Ni uzao unaotokana na kupandisha nguruwe wa aina mbili tofauti.

Nguruwe Chotara:
– Nguruwe wa kienyeji akipandishwa na wa kisasa (kigeni).
– Anastahimili magonjwa, anakua haraka na nyama yake huwa haina mafuta mengi.
– Anastahimili mazingira magumu kuliko wa kisasa.

  • Nguruwe wa Kienyeji

– Huwa ni wadogo kwa umbo.
– Wanakua taratibu hata kama wanapatiwa chakula bora.
– Hawana rangi maalum.
– Hustahimili mazingira magumu.
– Nyamayakehainamafutamengi.
– Wana uwezo wa kujitafutia chakula.

Leave a Reply