Gari aina ya FUSO lilikuwa limebeba Nguruwe likielekea Dar es Salaam limegeongana na Lori (Semi trailer) lililokuwa limebeba vifaa vya aina mbalimbali maeneo ya Vigwaza. Ajali hiyo imesababisha vifo vya papo hapo kwa nguruwe zaidi ya 100 na kuziba njia jambo lililopelekea uwepo wa foleni kubwa sana kwa magari yanayotumia njia hiyo. Nguruwe wengi pia walikuwa katika hali mbaya.